Header Ads

ANAYEDAIWA KUUMUA TRAFIKI KORTINI


Na Happiness Katabazi 

ANAYEDAIWA kumuua askari wa kikosi cha Usalama Barabarani wiki iliyopita, Elikiza Nnko, Jakson Stephen Fimbo jana alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na makosa ya matatu likiwemo kosa la kuingilia msafara wa kiongozi.

Mbele ya Hakimu Mkazi Kwey Lusema wakili mwandamizi wa serikali Lasdilaus Komanya alilitaja kosa la kwanza  ni la kusababisha  kifo cha trafiki huyo  kupitia kwendesha gari kwa hatari  na kwamba Machi 18 mwaka huu,  katika barabara ya Bagamoyo katika mataa ya Bamaga jijini Dar es Salaam,  mshitakiwa akiwa ni dereva  kiongozi wa gari lenye namba za usajili  T328 BML aina ya Land Lover Discovery.

Wakili Komanya alidai mshitakiwa huyo  aliendesha gari hilo ka mwendo wa hatari  katika barabara hiyo ambayo ni ya umma Mshitakiwa huyo jambo ambalo  lina hatarisha  usalama wa raia  na kutokana na mshitakiwa huyo kuendesha gari hilo kwa mwendo huo wa hatari alimgonga askari huyo ambaye amezikwa alhamisi iliyopita.

Alidai kosa la pili ni  kuingilia msafara  wa kiongozi,kuwa siyo ya Machi 18 mwaka huu, katika eneo hilo la mataa ya Bamaga,mshitakiwa huyo hakutii  maelekezo yaliyokuwa yakitolewa kwa ishara ya askari huyo Elikiza,ambaye alikuwa na wajibu wa kuyasimamisha magari kwa njia ya ishara.

Wakili Komanya alidai shitaka la tatu ni la kushitwa kutoa  taarifa za kusababisha ajali katika barabara hiyo ya umma na kwamba alishindwa kutoa tarifa za kusababisha ajali hiyo katika kituo chochote cha jirani.

Hata hivyo mshitakiwa huyo alikanusha mashitaka hayo na wakili Komanya alidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na anaomba tarahe ya kuja kumsomea maelezo ya awali mshitakiwa.
 Kwa upande wake  hakimu Lusema alisema ili apate dhamana ni lazima awe na wadhamini wawili ambao kila mmoja atasaini bondi ya Sh.milioni mbili ,hata hivyo mshitakiwa huyo alitimiza masharti hayo ya dhamana na akapata dhamana na hakimu huyo akaiarisha kesi hiyo  Aprili 15 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya upande wa jamhuri kumsomea maelezo ya awali.

Katika hatua hutua nyinge, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea kusikiliza kesi ya kuchapisha makala ya uchochezi inayomkabili aliyekuwa Mharii Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima na wenzake,kwasababu Kibanda bado amelazwa katika hospitali moja nchini Afrika Kusini kwaajili ya matibabu na hivyo ameiarisha hadi Aprili 29 mwaka huu.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 26 mwaka 2013.

No comments:

Powered by Blogger.