Header Ads

WALIOKUWA ASKARI POLISI KORTINI KWA WIZI WA SH.MIL.150
Na Happiness Katabazi

HATIMAYE waliokuwa askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam,watano jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kosa  la wizi wa Sh. Milioni 150  mali ya Mire Artan Ismail.

Mbele ya Hakimu Mkazi  Emilius Mchauro wakili mwandamizi wa serikali Bernad Kongola aiwataja washitakiwa hao kuwa ni Sajenti Dancan Mwasabila (43) mkazi wa Kiwalani, Koplo Geofrey (39) Mbezi Luis, Koplo Rajab Nkurukwa (46) mkazi wa Buguruni, Kolpo Kawanani Humphrey (34) mkazi wa Kijitonyama na Koplo Kelvin Mohamed (49) mkazi wa Gongo la Mboto.

Wakili Kongola alidai kuwa Desemba 18 mwaka jana katika eneo la Kariakoo Wilaya ya Ilala Dar es salaam, walitenda kosa hilo  na akadai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na washitakiwa wote walikanusha shitaka hilo.

Hakimu Mchauro alisema ili washitakiwa wapate ni lazima washitakiwa hao kila mmoja awe na wadhamini wawili wanaofanyakazi katika ofisi zinazotambulika ambapo watasaini pia bondi ya Sh.milioni tano kwa kila mmoja.

Aidha hakimu huyo alisema pia washitakiwa wenyewe kila mmoja wao atatoa fedha taslimu au kuwasilisha hati ya mali isiyoamishika yenye thamani ya Sh.milioni 15.

Hata hivyo ni washitakiwa wanne tu kati ya watano ndiyo walitimiza masharti ya dhamana jana na kufanya mshitakiwa Mohamed alishindwa kutimiza masharti hayo na hivyo hakimu kuamuru apelekwe gerezani  na arejeshwe leo mahakamani hapo kwaajili ya kuja kutimiza masharti hayo ya dhamana na akaiarisha kesi hiyo hadi Machi 27 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamis, Machi 14 mwaka 2013.


2 comments:

Anonymous said...

http://www.4006002833.com
[url=http://www.4006002833.com]太阳城娱乐城[/url],太阳城,菲律宾太阳城

Anonymous said...

Hey Theгe. Ι found your blog the use of msn.
That iѕ an extremely smartly writtеn artіcle.

Ӏ'll be sure to bookmark it and come back to read extra of your useful info. Thanks for the post. I'll defіnitеly comeback.


Taκe a look at my website; Watch Two and a Half Men Season 10 Episode 19 Big Episode. Someone Stole A Spoon Online Free Stream

Powered by Blogger.