HUKUMU YA KESI YA PONDA NI APRILI 18
Na Happiness
Katabazi
MAHAKAMA ya
Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imesema kuwa Aprili 18 mwaka huu,itaoa
hukumu ya kesi ya uchochezi wizi wa malighafi za sh.milioni 59 inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu,
Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49.
Hakimu Mkazi
Victoria Nongwa aliyasema hayo jana saa kumili alasiri muda mfupi baada ya
mashahidi wa tano wa upande wa utetezi waliopanda wote jana kizimbani kutoa
utetezi na hivyo kufanya upande wa utetezi weleta mashahidi 52.
Hakimu
Nongwa alizitaka pande mbili katika kesi hiyo kuwasilisha kwa maandishi
majumuisho ya mwisho ya kesi hiyo Aprili 3 mwaka huu, na kwamba kesi hiyo
itatajwa Aprili 4.
Kabla ya
kuyasema hayo Ponda jana alipanda
kizimbani na kuanza kutoa kujitetea ambapo alidai kuwa
ni kweli yeye ndiye aliyetoa maagizo kwa maimau
wa misikiti wawatangazie waumini wao ili waje kwenye kiwanja cha
Chang’ombe Markas kwaajili ya kuja kuongeza nguvu ya kujenga msikiti wa muda
katika kiwanja hicho.
Itakumbukwa
kuwa mashahidi watatu wa kesi hiyo ya uchochezi na wizi wa malighafi zenye
thamani ya Sh.milioni 59 inayomkabili Ponda na wenzake 49 jumla ya mashahidi wa
tatu ambao ni viongozi wa Bakwata na mkurugenzi wa kampuni ya Agritanza,
walitoa ushahidi wao na kusema kuwa awali kiwanja hicho kilikuwa kikimilikiwa
na Bakwata ambayo ndiyo yenye dhamana ya kumiliki mali zote za waislamu lakini
Bakwata ikaamua kuipatia kiwanja hicho Agritanza na Agritanza ikaipatia Bakwata kiwanja
kikubwa kilichopo Kisarawe kwahiyona kusema kuwa kiwanja cha Markas siyo mali
ya waislamu wala Bakwata lakini washitakiwa katika utetezi wao wanadai kiwanja hicho ni mali ya waislamu.
Sheikh Ponda
aliyekuwa akiongozwa kutoa utetezi wake na wakili wake Juma Nassor na Njama
mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa alieleza
ni yeye ndiye aliyetoa maelekezo hayo ya kuwataka waislamu wote wafike
katika eneo hilo ili wajenge msikiti wa muda na kwamba waislamu hao waliitikia
wito na kwamba kuanzia asubuhi ya saa
moja hadi saa 12 jioni ya Oktoba 12-14 yeye na waislamu hao walikuwa wakijenga
msikiti huo ndani ya kiwanja hicho ambacho ni mali ya waislamu.
“Kiwanja
hicho ni mali ya waislamu na kiwanja hicho tulipewa sisi waislamu na serikali
ya Misri tena wakati huo waislamu wote tulikuwa chini ya East Africa Muslim
Welfare,lakini baadae taasisi hiyo ilifutwa na serikali ndiyo ikaanzishwa
Bakwata…kwahiyo kufutwa kwa taasisi ile hakumaanishi mali zilizokuwa chini ya
taasisi zake nazo zimefutwa,kinachofanyika pale ni majukumu ya taasisi yale
yanakuwa yamesimama na mali zake zinabaki kuwa ni za wanachama wake wa taasisi
hiyo iliyofutwa ”alidai Sheikh Ponda
Hata hivyo
alikanusha mashitaka yote yanayomkabili na kusema hafahamu ni kwanini upande wa
jamhuri umemfungulia mashitaka hayo kwasababu hata hilo kosa la wizi wa
malighafi ,mahakama ilipaswa iamie eneo la tukio iende kashuhudie kama wale
waislamu niliokuwa nao kama walichukua malighafi za kampuni ya Agritanza
kujengea msikiti wa muda.
Akielezea
jinsi alivyokmatwa na askari ,Ponda alidai Oktoba 16 mwaka jana ,saa nne
kasoro wakati akiingia ndani ya msikiti
wa Tungi uliopo Temeke kabla ya kuingia ndani alisikia sauti ya mtu
ikimuita na mtu huyo alikuwa ndani ya gari, akawataka watu hao wamfuate nyuma.
“Nilipoingia
msikitini nikasikia sauti ya magari nikatazama nikaona magari matatu aina ya
Land Cruser zina askari wa kikosi cha
FFU wakiwa na silaha na mabomu na wale
askari walingia ndani ya msikiti wakiwa wamevaa viatu wakanivamia na
kuniangusha chini na wakanitoa ndani ya msikiti kwa mtindo wa kuniteka nyara na
kunikimbiza kwenye gari lao kwa
kasi”alidai Sheikh Ponda.
Alidai kisha
walimepeleka katika kituo cha polisi Chang’ombe na wakanieleza kosa langu na
wakaniambia mimi siyo raia wa Tanzania, na ni kwanini nisiende kufanya vurugu
Burundi minikawaambia ni rais wa Tanzania’alidai Ponda.
Akijibu
maswali ya wakili Mwandamizi wa Serikali Tumaini Kweka kuwa hakuona ni kosa kwa
yeye kuita waislamu waende kujenga msikiti wa muda katika eneo lile ambalo si
mali ya waislamu , Ponda alijibu kuwa ‘Sikiliza Kweka mimi nimeanza mijadala
tangu enzi serikali ya rais Julias Nyerere
kwahiyo nina uzoefu na huo siyo uchochezi’alidai Ponda.
Kwa upande
wake mshitakiwa wa tano, Mkadamu Abdallah akijitetea yeye alidai kuwa hafahumu
hicho kiwanja kiliuzwa kwanani, na wala hajawai kutoa maelezo polisi na
hafahamu kama Ponda alienda kwa Mufti wa Tanzania Sheikh Simba kumuuliza kuwa
kiwanja hicho kimeuzwa.
Hata hivyo
wakili Kweka alipomtaka Mkadamu areje maelezo yake aliyoyatoa polisi ambayo
yamepokelewa mahakamani kama kielelezo ambapo ndani ya maelezo hayo Mkadamu
alikiri kufahamu kuwa kiwanja kile kimeuzwa kwa Agritanza na Bakwata na kwamba
yeye na waislamu wenzake walienda katika kiwanja hicho na kuanza kujenga
msikiti wa muda, mkadamu alishia kwa kudai kuwa maelezo hayo si yake.
Oktoba 18
mwaka jana, kesi hiyo ilifunguliwa mahakamani hapa kwa mara ya kwanza ambapo
washitakiwa wanakabiliwa na jumla ya makosa matano ambayo ni kula njama kutenda kosa, kuingia
kwa jiani, kujimilikisha kwa nguvu kiwanja hicho, wizi wa malighafi zenye
thamani y ash.milioni 59 na uchochezi.
Chanzo:Gazeti la
Tanzania Daima la Ijumaa,Machi 22 mwak 2013.
1 comment:
Hmm is anуonе else hаѵing problеms with the pictures on
this blog loаding? I'm trying to determine if its a problem on my end or if it's the
blog. Anу ѕuggеѕtions woulԁ be
gгeatly appгeсiatеd.
Here is mу blog: yookos.com
Post a Comment