Header Ads

Dk.BILAL AWAFARIJI WAFIWA MSIBA WA TRAFFIKI

Na Happiness Katabazi

MAKAMU wa rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Mohamed Gharib Bilal jana aliongoza ujumbe wa serikali kufika kwenye msiba wa aliyekuwa  askari wa  kikosi cha Barabarani Elikiza Lokisango alifariki dunia juzi akiwa kazini eneo la Bamaga jijini Dar es Salaam.

Mbali na Makamu wa rais, viongozi wengi waliofika kuhani msiba ambao unafanyika nyumbani kwa marehemu eneo la Boko Shule, ni Waziri wa Mambo ya Ndani dk.Emanuel Nchimbi, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema,Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mpinga  na maofisa wengine wa jeshi hilo la polisi.
Viongozi hao wakiwa nyumbani kwa marehemu walimfariji mume wa marehemu ambaye ni askri wa jeshi la polisi mkoa wa kipolisi Kinondo, Daudi Luhala na watoto wake Rehema ,Mwombeki.
Kwa upande wake kaka mkubwa wa mume wa marehumu, Mhadhiri wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk.Christian Alphonce  aliishukuru serikali na viongozi wote walifika kwenye msiba na kuwafariji na kwani kitendo hicho kimedhihirisha wazi serikali inavyowajali wananchi wake na kwamba msiba huo umkuwa pigo kwenye familia na jeshi la polisi.

Dk.Alphonce alisema marehemu anatarajiwa kuzikwa kesho katika mchana katika makaburi ya Mbweni Malindi Estate.

Marehemu alifariki juzi mchana wakati akiongoza msafara wa rais, ambapo dereva wa gari moja aliendesha gari kwa mwendo kasi kabla ya kuruhusiwa na trafiki huyo na kisha kumgonga Lokisango  ambaye alikuwa barabarani akifanyakazi yake ya kuongoza magari.

Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.   

Chanzo;Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 20 mwaka 2013.

1 comment:

Anonymous said...

My coԁer is trying to peгsuаde me to
mοvе to .net from PHP. I hаvе alwaуs
dislіked the idea becаuse of the eхpensеs.
But he's tryiong none the less. I'νе been using WordΡress οn a variety оf websites for аbout a
year аnd am аnxiοus about swіtching to anоther
ρlatform. I haνе heard veгy gоod thіngs about blogengine.
net. Is thегe a ωay I can import all my wordpгess сontent into it?

Any kind of hеlp wοuld be greаtlу apprесiatеԁ!my web page - Watch Mike & Molly Season 3 Episode 17 St. Patrick's Day Online Free Stream

Powered by Blogger.