LWAKATARE AFUTIWA KESI,AFUNGULIWA KESI TENA YA UGAIDI
Na Happiness
Katabazi
MAHAKAMA ya
Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,jana ilimfutia kesi ya makosa ya ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph kwa sababu ya Mkurugenzi wa
Mashitaka( DPP), Dk.Eliezer Feleshi kuwasilisha hati ya kuwafitia kesi hiyo
washitakiwa kwa sababu hana haja ya kuendelea nayo.
Sambamba na
hilo, DPP ilimfungulia kesi ya makosa ya ugaidi
upya Lwakatare na mwenzake ambapo kesi hiyo mpya namba Na.6/2013 ambapo imepangiwa kwa hakimu mpya
Aloyce Katemana.
Katika kesi
ya ugaidi Na.37/2013 iliyofunguliwa na Jamhuri dhidi ya Lwakatare na wenzake
Machi 18 mwaka huu, ambayo ilifutwa jana saa tatu asubuhi na ambayo jana
ilikuwa imekuja kwaajili ya hakimu mkazi Emilius Mchauru kutolea uamuzi wa ama
wa kuwapatia dhamana washitakiwa au la, hakimu Mchauru alijikuta jana
akishindwa kutoa uamuzi wake kwa sababu
mawakili viongozi wa serikali Ponsian Lukosi, Prudence Rweyongeza na
Peter Mahugo waliwasilisha hati hiyo ya
DPP chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya
mwaka 2002, ambapo kifungu hicho kina mpa mamlaka DPP, kuifuta kesi yoyote ya
jinai muda wowote kabla ya haijatolewa hukumu na uamuzi huo wa DPP haujahojiwa
na mtu yoyote.
‘Kwa kuwa
kesi hii Na.37/2013 ilifunguliwa na upande wa jamhuri MAchi 18 mwaka huu, na
leo kesi hii ilikuja kwaajili ya mahakama kutolea uamuzi wa maombi ya
washitakiwa kupatiwa dhamana au la
pamoja na maombi mengine…mahakama hii inasema haitaweza kutoa uamuzi
wake kwa sababu DPP amewasilisha hati ya kutotaka kuendelea kuwashitaki
washitakiwa na hivyo mahakama hii
inawafutia kesi washitakiwa wote”alisema hakimu Mchauru.
Baada ya
hakimu Mchauru kuwafutia kesi, askari kanzu waliwakamata tena washitakiwa hao
na kuwaweka chini ya ulinzi wa gari la polisi na ilipofika saa 4:20 asubuhi
,washitakiwa hao wakiwa chini ya ulinzi mkali wa wana usalama waliingizwa tena
katika ukumbi namba mbili wa mahakama hiyo mbele ya hakimu mkazi mwingine Alocye
Katemana.
Mawakili
Wakuu wa Serikali Wakuu Ponsian Lukosi, Prudence Rweyongeza na Wakili
Mwanadamizi wa serikali Peter Mahugo walidai kuwa kesi hiyo nimpya na imepewa
Na.6 ya maka huu, ambapo washitakiwa ni Lwakatare na Ludovick wanaotetewa na
mawakili wa kujitegemea Profesa Abdallah Safari na Peter Kibatara na kwamba
hati hiyo mashitaka ina jumla ya
mashitaka manne ambapo shitaka la kwanza linaangukia kwenye Sheria ya
Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 na makosa matatu yote yanaangukia kwenye Sheria
ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002.
Wakili Rweyongeza alililata kosa la kwanza ambalo
linawakabili washitakiwa wote kuwa ni la kula njama kutenda kosa la jinai
kinyume na kifungu cha 284 cha Sheria ya
Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 , na kwamba mnamo Desemba 28 mwaka jana, huko
Kimara King’ong’o Stopover, wote kwa
pamoja walitenda kosa hilo kwa kutaka kutumia
sumu kwa lengo la kumdhuru Denis
Msaki ambaye ni Mhariri wa habari wa Gazeti
la Mwananchi ambalo ni kinyume na kifungu cha 227 cha sheria hiyo.
Wakili
Rweyongeza alilitaja kosa la pili kuwa
ni la kula njama ambalo pia ni kwaajili
ya washitakiwa wote ambalo ni kinyume na
kifungu cha 24(2) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi Na.21 ya mwaka 2002, ambapo
washitakiwa hao walitenda kosa la ugaidi la
kutaka kumteka Msaki kinyume na
kifungu cha 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya
Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002.
Shitaka la
tatu ni la washitakiwa wote ambapo wanashitakiwa kwa kosa la kupanga kufanya makosa ya ugaidi kinyume na kifungu cha 59(a) cha Sheria ya
Kuzuia ugaidi kwamba Desemba 28 mwaka jana,walishiriki katika mkutano wa kupanga
kufanya vitendo vya kumteka nyaraka Msaki
kinyume na kifungu 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi.
Shitaka la
nne, Rweyongeza alidai linamkabili Lwakatare peke yake ni aliwezesha kutendeka kwa kosa la ugaidi
kinyume na kifungu cha 23(a) cha sheria ya kuzuia ugaidi , kwamba Desemba 28
mwaka jana, Lwakatale akiwa ni mmiliki nyumba hiyo ilipo Kimaraka King’ong’o kwa makusudi
aliliruhusu kufanyika kwa kikao hicho
baina yake na Ludovick cha kutenda kosa
la ugaidi la kutaka kumteka nyara Msaki hata hivyo walikanusha mashitaka hayo.
Hata
hivyo Hakimu Katemana alisema
washitakiwa hao hawatakiwi kujibu chochote kwasababu mahakama hiyo haina
mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na akaiarisha kesi hiyo hadi Aprili 3 mwaka
huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa.
Lakini hata
hivyo Wakili Kibatara aliomba mahakama
isikilize ombi lake alilokuwa akitaka kuliwasilisha,hata hivyo Hakimu Katemana
alisema yeye ndiye kiongozi na mawakili wa utetezi, jamhuri wapo chini yake na
akamweleza Kibatara mahakama ni mhimili unaongozwa kwa taratibu zake na
nilazima Kibatara azifuate,hivyo yeye hakimu ana majukumu mengine hivyo leo
hayupo tayari kusikiliza ombi hilo la Kibatara wale ombi la upande wa jamhuri
lilokuwa linaomba mahakama imruhusu Ludovick aendekushikiliwa na jeshi la
polisi kwaajili ya hatua zaidi za
kipelelezi na kuieleza kuwa mkutaratibu zake za kuwasilisha ombi la linalotaka
Ludovick aende kukaa chini ya uangalizi wa polisi na akaamuru washitakiwa
wapelekwe gerezani.
Itakumbukwa
kuwa Machi 18 mwaka huu, Hakimu Mchauri alitoa fursa kwa washitakiwa ya
wakubali au wakanushe mashitaka hayo yanayowakabili washitakiwa licha makosa
yanayowakabili washitakiwa hao kwa mujibu wa Sheria za nchini, Mahakama ya
Hakimu Mkazi haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo wala hakimu haruhusiwi kutoa
fursa kwa washitakiwa wakubali au
wakanushe mashitaka yanayowakabili kwani ni Mahakama Kuu peke yake ndiyo yenye
mamlaka ya kusikiliza kesi za makosa ya
tuhuma za ugaidi.
Baada ya
kesi hiyo kuairishwa wafuasi wa Chadema wengine wakiwa wamevalia sare walipaza
sauti na kusema ‘Peoples Power’….hakuna kulala hadi kwanza walale wao’.
Hali
iliyosababisha wanausalama waliokuwa wamevalia sare na wale waliovalia kiraia
walikuwa ndani ya kumbi wa kesi ilipokuwa ikiendeshewa kuwataka watu wote
watoke ndani ya ukumbi huo haraka ili waweze kuwapitisha washitakiwa amri
ambayo wafuasi hao waliitii bila shuruti.
Msafara wa
magari nane ukiongozwa na magari ya jeshi la magereza, polisi waliondoka ndani
ya viwanja hivyo kwaajili ya kumpeleka gereza la Keko ,washitakiwa hao, huku
askari wa kikosi cha mbwa wakiwa bado
katika eneo la mahakama hiyo kwaajili ya kuimarisha ulinzi hata hivyo hali
ilikuwa ni shwari kwasababu hakukuwepo na vitendo vya uvunjifu wa amani kwani
wafuasi wa Chadema waliondoka mahakamani hapo kwa utulivu wa hali ya juu huku
wengine wakiangua vilio kwa uchungu wa mashitaka yanayomkabili washitakiwa
ambao ni wachama wa chama chao.
Mbwa
waliokuwepo wakiimarisha ulinzi eneo hilo ni Kino,Pd Kambi Simba, Giro,Pd Roja,
Pd Ivo,pd undra,Pd Bobi ambapo Mbwa hao wamepata mafunzo ya kuimarisha ulinzi
toka nchi mbalimbali ikiwemo Lebanoni.
Akizungumza nje ya viwanja vya mahakama baada ya kesi kuairishwa, Mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe alisema kwanza asingependa kuingilia mtiririko wa
mahakama na kuwataka waandishi wa habari wamuhoji wakili wa washitakiwa lakini
akasema wao wanafanyakazi za mageuzi kwaajili ya kuwatetea raia wanyonge na
maskini na kwamba kilichompata Lwakatare siyo geni ni mtiririko kwa mabavu ya
dola dhidi ya wanamageuzi.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Machi 22 mwaka 2013.
1 comment:
Pretty gгeаt post. I just stumbled upon yοur
ωeblog and wаntеd to ѕау that I have really lоved brоwsing
your weblog ροsts. After all I'll be subscribing to your feed and I'm hopіng you
wrіte onсe mοrе very soon!
Heге is mу homepage - Watch Murdoch Mysteries Season 6 Episode 10 Twisted Sisters Online Free Stream
Post a Comment