WASHITAKIWA KESI YA PONDA WAZIDI KUKANA MAELEZO WALIYOYATOA POLISI
Na Happiness Katabazi
WASHITAKIWA
nane wa kesi ya uchochezi na wizi wa malighafi za sh.milioni 59 inayomkabili
Sheikh Ponda Issa Ponda jana wameendelea kujitetea na kuyakana maelezo
waliyoyatoa polisi wakati walipokamatwa.
Mbele ya
Hakimu Mkazi Victoria Nongwa washitakiwa
hao ambao ni mshitakiwa 22,23,24,25,27,26,29 jana ambao walikuwa wakiongozwa na
wakili wao Juma Nassor kutoa utetezi wao walidai kuwa wao hawakuwahi
kuchukuliwa maelezo polisi na kwamba polisi walichofanya nikuwauliza majina yao
tu.
Wakitoa
utetezi wao walidai kuwa wao Oktoba 16 mwaka jana, walikuwa msikiti wa Shule ya
Changombe Markas kwaajili ya kuudhurulia
ibada ya Itikafu ambapo walidai taarifa za kufanyika kwa ibada hiyo walizipata
kupitia misikiti mbalimbali.
Hata hivyo
wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka baada ya kusikiliza utetezi wa
washitakiwa hao, alikuwa akiwauliza washitakiwa hao kama wana maradhi yoyote au
wanaugonjwa wa kusahau ambapo washitakiwa hao wote walidai hawana tatizo
lolote.
‘Hivi nyie
mashahidi wote leo hii mnadai kuwa kabla ya kufikishwa mahakamani hapa Oktoba
18 mwaka jana, hakumchukuliwa maelezo polisi, hapa mahakamani kuna maelezo ya
onyo ambayo mliyatoa polisi Kijitonyama wakati mkihojiwa na maelezo haya
yanataja maelezo yenu binafsi, kazi zenu:
“Na
washitakiwa wengine katika hizi nakala za maelezo yenu mlikiri kukamatwa katika
eneo la Chang’ombe Markas ambapo mlikuwa
mkijenga msikiti wa muda , na mlikuwa na vifaa vya ujenzi kwaajili ya kujengea
msikiti huo ambao mlieleza kabisa mlifikia uamuzi wa kuweka kambi katika eneo
hilo kwasababu mlipata taarifa kuwa kiwanja hicho mali ya waislamu kilikuwa
kimeibwa na hivyo mliamasishwa kwenda kukikomboa kiwanja hicho”alidai shahidi
wa 34, Salima Abdukadirfu.Kesi hiyo inaendelea tena leo.
Wakili Kweka
aliwahoji washitakiwa hao kuwa inakuwaje sasa polisi ambaye alikutana na
washitakiwa kwa mara ya kwanza siku hiyo wakati wakiwahoji, kisha mapolisi hao
waweze kufahamu hata maelezo binafsi ya washitakiwa hao ambapo washitakiwa hao
walikuwa wakikubali majina yao na saini
yaliyokuwa yameanishwa kwenye maelezo hayo ya onyo lakini wakakanusha maelezo ya
kina yaliyokuwa yameandikwa katika nakala hiyo ya maelezo ya onyo ambayo
waliyayotoa polisi na yameifadhiwa mahakamani hapo kama vilelelezo.
Hata hivyo
washitakiwa hao walishindwa kujibu maswali hayo ya wakili Kweka na kuishia
kudai kuwa hawafahamu polisi hao wameyapata wapo maelezo yao binafsi
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Machi 12 mwaka 2013.
1 comment:
One thousand Online Payday Loan Loans-Get Online Payday Loan proper Into
Your Topper AR financeStamp Recipients: win over food Stamps To Online payday loan A
Growing security departmentStalked By 450-Year-Old debt Payday Advance Today Is Payday streamdistaff
Prison ship's officer 33 Who fell In dearest With Drugsundefendable Flipping: tender Your website And Get agile Results CanObama Online Payday Loan MADE comfortable Duff Mckagan - Maybe The Coolest
my website > payday loan
Post a Comment