WAFUASI 53 WA SHEIKH PONDA WAFUNGWA JELA MWAKA MMOJA
Na
Happiness Katabazi
HATIMAYE
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es
Salaam, imewahukumu kwenda jela mwaka mmoja wafuasi 53 wa Katibu wa
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Sheikh Issa Ponda waliokuwa wakikabiliwa na kesi
ya kula njama na kufanya maandamano
haramu.
Hukumu
hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Sundi Fimbo ambapo alianza kwa kuikumbusha
mahakama kuwa mshitakiwa Salum Bakari Makame na wenzake 52 wanaotetewa na
wakili wa kujitegemea Mohamed Tibanyendera walikuwa wakikabiliwa na jumla ya
makosa manne ya kuandamana kwenda ofisi ya Mkurugenzi wa
Mashitaka(DPP),Dk.Eliezer Feleshi kumshinikiza ampatie dhamana Ponda kwani DPP
ndiye ameifunga dhamana ya Ponda.
Hakimu
Fimbo alilitaja kosa la kwanza ni la kula njama kutenda kosa kinyume na kifungu
384 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002, kosa la pili ni la kufanya
mkusanyiko haramu kinyume na kifungu cha 74 na 75 cha sheria hiyo ambavyo vinasomwa pamoja na kifungu cha
43(2)(4) na 46 cha Sheria ya Jeshi la Polisi ya mwaka 2002.
Kosa
la tatu ni la kukaidi amri ya jeshi la polisi iliyowataka watawanyike ambalo ni
kinyume na kifungu 79 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu na kinachosomwa pamoja na
kifungu cha 44 cha Sheria ya Jeshi la Polisi
ya mwaka 2002 na kosa la nne ni
la uchochezi ambalo lilikuwa likiwakabili washitakiwa watatu tu ambao ni
Makame, Said Idd, Ally Nurdin Nandumbi
ambao wote hawa Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), aliwafungia dhamana tangu
walipofikishwa kwa mara ya kwanza mahakama ni hapo Februali 18 mwaka huu.
Hakimu
Fimbo alisema ili kuthibitisha kesi yao upande wa jamhuri uliokuwa
ukiwakilishwa na mawakili waandamizi wa
serikali Serikali Bernad Kongora,Peter
Ndjike,Zuberi Mkakatu na Joseph Mahugo na Nassor Katuga walileta jumla ya
mashahidi 10 na upande wa utetezi
walileta jumla ya mashahidi 54.
Hakimu
Fimbo alisema mahakama yake kabla ya kutoa hukumu yake mahakama ilijiuliza
maswali manne kuwa je washitakiwa walikula njama kutenda kosa?,walifanya
mkusanyiko haramu?,walikaidi amri ya jeshi la polisi iliyowataka
wasiandamane?na je walifanya uchochezi?
“Baada
ya kujiuliza maswali hayo mahakama hii imefikia uamuzi wa kuwaona washitakiwa
52 walitenda kosa la kula njama isipokuwa mshitakiwa wa 48 (Waziri Omar Toli)
hakutenda kosa hilo kwa sababu alikutwa akitoka kununua mabeseni, mahakama hii
imewatia hatiani kwa kosa hilo kwani kwa mujibu wa vielelezo vilivyoletwa
mahakamani yaani barua iliyoandikwa na Taasisi ya Jumuiya ya Maimamu kwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam kuomba kibari cha maandamano na polisi
wakawakataza ila wakaandamana, washitakiwa wengine walikamatwa na vipeperushi,
mabango,vipaza sauti vinavyosema ‘Dpp ukristo utakuponza’:
“Kwa vielelezo hivyo mahakama hii imeridhika
kwamba walitenda kosa la kwanza, la pili na la tatu na kosa la nne ambalo ni la uchochezi mahakama hii imeona
upande wa jamhuri umeshindwa kulithibitisha na kwasababu hiyo mahakama hii imewatia hatiani kwa washitakiwa wote kwa
makosa matatu isipokuwa mshitakiwa 48 ametiwa hatiani kwa kosa la tatu tu” alisema
Hakimu Fimbo.
Akilichambua
kosa la pili ambalo ni la kufanya mkusanyiko haramu, hakimu huyo alisema pia
mahakama inamuachilia huru mshitakiwa wa 48 ,isipokuwa washitakiwa wengine wote
wametiwa hatiani kwa kosa hilo kwasababu walikutwa katika maeneo tofauti
wakitenda kosa hilo na katika utetezi wake walitoa walitoa ushahidi unaopishana
ambao wengine walidai kuwa wa walikuwa wameenda kununua bidhaa,na walikuwa na
fedha mfukoni lakini hata hivyo kiwango cha fedha walichokitaja polisi,na
mahakamani ni tofauti ‘alisema hakimu Fimbo.
Hakimu huyo alisema
kila kosa alilowatia nalo hatiani watalitumikia kifungo ha gerezani kwa mwaka
mmoja,hivyo washitakiwa hao watatumikia adhabu ya mwaka mmoja jela.
Kabla ya
hakimu kutoa adhabu, wakili wa serikali Komonya aliomba mahakama itoe adhabu
kwa washitakiwa hao ili iwefundisho kwa wengine na kwamba upande wa jamhuri hauna
rekodi zozote zinazoonyesha washitakiwa hao waliwai kushitakiwa kwa makosa ya
jinai.
Kwa upande
wake wakili wa utetezi Tibanyendera aliomba mahakama iwapatie adhabu ndogo
washitakiwa hao kwani ni watu wanaotegemewa na familia zao na wengine tangu
wakamatwe Februali 15 mwaka huu, wapo gerezani hadi leo hivyo muda wote
waliokaa gerezani ni adhabu tosha na kwamba washitakiwa wengine ni wagonjwa na
kwamba idadi ya washitakiwa ni kubwa na endapo ikipelekwa wote gerezani
watakuwa wanatumia gharama kubwa za fedha za serikali kwaajili ya kuhudumiwa.
Kwa upande
wake hakimu Fimbo alisema amezingatia maombi ya pande zote mbili na kwamba
badala ya kuwahukumu kwenda jela miaka saba, anawahukumu kwenda gerezani mwaka
mmoja na akasema yoyote ambaye ajaridhika na hukumu hiyo anaruhusiwa kwenda
kukata rufaa mahakama ya juu.
Baada ya
kumuliza kutoa hukumu hiyo, ndugu na jamaa wa washitakiwa hao waliigeuza
mahakama na viunga vyake ni sehemu ya
msiba kwani walianza kuangua vilio kwa sauti ya juu.
Kesi
hii ya kihistoria ilifunguliwa rasmi
Februali 18 mwaka huu na siku hiyo hiyo upande wa jamhuri ukasema upelelezi wa kesi hiyo
umekamilika na Februali 19 mwaka huu,upande
wa jamhuri uliwasomea maelezo ya awali washitakiwa hao na shahidi wa kwanza wa
upande wa Jamhuri ambaye ni Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Hemed Msangi alianza kutoa ushahidi wake hadi Februali 26 mwaka huu, upande wa
jamhuri ulipofunga ushahidi wake ,washitakiwa wakaanza kujitetea na Februali 19
mwaka huu, upande wa utetezi ulipofunga utetezi na jana mahakama ikatoa hukumu
hiyo.
Chanzo:Gazeti
la Tanzania Daima la Ijumaa, Machi 22 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment