LWAKATARE WA CHADEMA KORTINI KWA UGAIDI
Na Happiness Katabazi
HATIMAYE
Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, Dk.Eliezer Feleshi amemfikisha katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo(Chadema),Wilfred Lwakatare na mwenzake kwa makosa ya
ugaidi.
Mbali na Lwakatare
mshitakiwa mwingine ni Ludovick Rwezaula Joseph ambao wanatetewa na mawakili wa
kujitetemea Profesa Abdallah Safari, Tundu Lissu na Nyaronyo Kichere.
Washitakiwa
hao wakifikishwa jana saa mbili asubuhi mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali
wa askari kanzu walikuwa wakiongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai
Mkoa wa Ilala, Duwani Nyanda na kuifadhiwa nyuma ya jengo la mahakama hiyo
tayari kwaajili ya kufikishwa kizimbani kosomewa mashitaka yanayowakabili.
Washitakiwa
hao waliingizwa ndani ya ukumbi namba moja wa mahakama hiyo saa 7:06 mchana
chini ya ulinzi mkali wa wanausalama , huku Lwakatare akiwasalimu wafuasi wa
Chadema, kwa kuwaonyesha ishara ya vidole viwili ambapo wafuasi hao walikuokuwa
wamefurika mahakamani hapo tangia asubuhi jana wakimjibu kwa kumuonyeshea
ishara ya vidole viwili juu.
Baada ya
kupanda kizimbani, jopo la mawaikili wakuu wa seriakali linaloongozwa na
Mwanasheria Kiongozi wa Serikali Kanda ya Dar es Salaam, Ponsian Lukosi,
Purdence Rweyongeza na Peter Mahugo
ambapo walidai hati ya mashitaka ina jumla ya makosa manne.
Wakili
Rweyongeza alililata kosa la kwanza ambalo linawakabili washitakiwa wote kuwa
ni la kula njama kutenda kosa la jinai kinyume na kifungu cha 284 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002
, na kwamba mnamo Desemba 28 mwaka jana, huko Kimara King’ong’o Stopover, wote kwa pamoja walitenda kosa hilo
kwa kutaka kutumia sumu kwa lengo la
kumdhuru Denis Msaki ambaye ni Mwanahabari wa Gazeti la Mwananchi
ambalo ni kinyume na kifungu cha 227 cha sheria hiyo.
Wakili
Rweyongeza alilitaja kosa la pili kuwa
ni la kula njama ambalo pia ni kwaajili
ya washitakiwa wote ambalo ni kinyume na
kifungu cha 24(2) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi Na.21 ya mwaka 2002, ambapo
washitakiwa hao walitenda kosa la ugaidi la kutaka kumteka Msaki kinyume na kifungu cha 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi
ya mwaka 2002.
Aidha
alilitaja kosa la tatu kuwa ni kutenda
kufanya mkutano wa kupanga kufanya makosa ya ugaidi kinyume na kifungu cha 59(a) cha Sheria ya
Kuzuia ugaidi kwamba Desemba 28 mwaka jana,walishiriki katika mkutano wa kupanga
kufanya vitendo vya kumteka nyaraka Msaki
kinyume na kifungu 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi.
Wakili
Rweyongeza alilitaja shitaka la nne ambalo linamkabili Lwakatare peke yake ni
aliwezesha kutendeka kwa kosa la ugaidi kinyume na kifungu cha 23(a) cha sheria
ya kuzuia ugaidi , kwamba Desemba 28 mwaka jana, Lwakatale akiwa ni mmiliki
nyumba hiyo ilipo Kimaraka King’ong’o kwa makusudi
aliliruhusu kufanyika kwa kikao hicho
baina yake na Ludovick cha kutenda kosa
la ugaidi la kutaka kumteka nyara Msaki hata hivyo walikanusha mashitaka hayo.
Wakili
Rweyongeza alidai kuwa makosa hayo yameletwa chini ya sheria mbili tofauti
yaani kosa la kwanza linaangukia katika sheria ya Kanuni ya Adhabu lakini kosa
makosa yaliyosalia yanaangukia kwenye Sheria ya Kuzuia ugaidi na kwamba makosa
yanaoangukia kwenye sheria ya ugaidi huwa
hayana dhamana na kwamba ni Mahakama Kuu peke ndiyo yenye mamlaka ya
kusikiliza kesi hiyo.
Wakili
Rweyongeza aliieleza mahakama kuwa jamhuri inawasilisha ombi la pili ambapo
wanaiomba mahakama imruhusu mshitakiwa wa pili(Ludovick) aende kukaa chini ya
ulinzi wa jeshi la polisi kwasababu Jeshi la polisi linamuiitaji kwaajili ya
hatua za kiupelelezi zaidi.
Hata hivyo
mawakili wa utetezi Peter Kibatara aliomba mahakama iwapatie wateja wake
dhamana na kwamba suala la washitakiwa kupatiwa dhamana au kunyimwa ni la
mahakama.
Kwa upande
wake wakili Lissu alidai aliita hati ya mashitaka kuwa ni kipande cha karatasi
kilichowasilishwa na DPP-Dk.Feleshi ambacho akionyeshi nembo ya serikali, mhuri
na wala hiyo hati ambayo aliipachika jina la kipande cha karatasi kuwa
hakikuletwa mahakamani hapo kwa ridhaa ya DPP na kwamba anaiomba mahakama hiyo
isiiamini hicho kipande cha karatasi kuwa ni nyaraka halali ya serikali..
Kwa upande wake wakili Profesa Abdallah Safari
aliomba mahakama irejee kesi za kupambikiwa zilizowai kufunguliwa mahakamani
hapo na ofisi ya DPP miaka ya nyuma ikiwemo kesi ya mauji ya fundi majeneza wa
Manzese ya mwaka 2002, iliyofunguliwa na jamhuri dhidi ya Sheikh Issa Ponda na
Sheikh Kundecha ambapo yeye alikuwa akiwatetea washitakiwa hao ambapo
alilazimika kwenye kuonana na DPP wa wakati huo ambaye ni Jaji mstaafu kwa sasa
Juxon Mlai na kumueleza kuwa kesi ile ya mauji ni ya kubambikwa ambapo Mlai
alitumia mamlaka yake kuifuta kesi ile.
“Katika kesi
hii ya Lwakatare ninachokiona ni matumizi mabaya ya sheria na wale waliombakizia
kesi Lwakatare wanastarehe na kufurahi kuona Lwakatare anaenda kuishi
gerezani”alidai Profesa Safari.
Akipangua
hoja za mawakili hao wa utetezi, wakili wa serikali Rweyongeza alidai kuwa hoja
hizo tatu zilizowasilishwa na mawakili wa utetezi ni dhaifu na kwamba anaomba
mahakama isiione kesi hii ni ya macho ya chama fulani ya kisiasa,tunaomba
mahakama itambue kuwa kesi hii imefunguliwa na upande wa jamhuri na wala
haijafunguliwa na chama cha siasa.
Kuhusu hoja
ya kuwabambikizia kesi washitakiwa hao,Rweyongeza ambaye alikuwa akionyesha
kujiamini alidai kesi hiyo siyo ya kubambikiziwa na kwamba ofisi ya DPP inafanyakazi yake kwa
mujibu wa sheria na haipo kwaajili ya
kubambikia watu kesi na kwamba kama Profesa Safari anaushahidi Lwakatare
kabambikiwa kesi basi aende kuonana na DPP na ampatie huo ushahidi unaonyesha
washitakiwa wamebambikiwa kesi.
Akiijibu
hoja ya Lissu kuwa DPP amewasilisha kipande cha karatasi kisicho na kibali cha
DPP, wakili Rweyongeza alimtaka Lissu aache kasumba ya kuongea mambo bila ya
kufanya utafiti kwani DPP amefungua kesi hiyo na amewasilisha kibali chake
mahakamani hapo ambapo wakili huyo aliklitoa kibali hicho kama kielelezo hali
iliyofanya watu kuanza kuangua vicheko.
Aidha kuhusu
hoja ya kutaka washitakiwa wapatiwe dhamana, wakili Rweyongeza alidai kuwa
sheria ya ugaidi imetungwa na bunge na bunge
ambapo kifungu cha 49 cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi kinakataza kabisa
mshitakiwa anayeshtakiwa kwa makosa yanayoangukia kwenye sheria ya ugaidi
kupewa dhamana na kwamba washitakiwa hao makosa yanayowakabili yanaangukia
kwenye ya ugaidi hivyo mahakama haiwezi kuwapa dhamana.
“Sasa
nawashangaa hawa mawakili wa washitakiwa leo hii wanajifanya hawajui matakwa ya
kifungu cha 49 cha sheria ya ugaidi kinasema nini.Sheria ya ugaidi imetungwa na
bunge hivyo ni sheria halali na kama mawakili wa utetezi wanaona sheria hiyo ni
mbaya basi haraka sana nawashauri waende mahakama kuu wafungue kesi ya kikatiba
ya kupinga kifungu hicho cha sheria ya ugaidi
lakini kwasasa sisi tunasema sheria ya ugaidi ipo kihalali na ndiyo
imetumika kuwashitaki washitakiwa hawa”alidai wakili Rweyongeza.
Kwa upande
wake hakimu mkazi Emilius Mchauru alisema amesikiliza hoja za pande zote mbili
na kwamba atatolea uamuzi kesho na kuamuru washitakiwa wote wapelekwe gerezani,huku
akiikataa hoja ya wakili Kibatara iliyotaka Lwakatare
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Machi 19 mwaka 2013.
2 comments:
Happiness, kalamu yako inaonekana haikunyooka katika habari hii.
Happiness, kalamu yako inaonekana haikunyooka katika habari hii.
Post a Comment