Header Ads

HUKUMU KESI YA MTIKILA AGOSTI 27

Hukumu kesi ya Mtikila Agosti 27 Na Happiness Katabazi MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imesema Agosti 27 mwaka huu, itatoa hukumu ya kesi ya kusambaza waraka wa uchochezi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Democratic(DP), Mchungaji Christopher Mtikila dhidi ya Rais Jakaya Kikwete. Hayo yalisemwa jana na Hakimu Mfawidhi Ilvin Mugeta muda mfupi baada ya shahidi wa pili wa upande wa utetezi katika kesi hiyo ambaye ni Mpiga Picha wa Gazeti la Mwananchi, Mpoki Bukuku kumaliza kutoa ushahidi wake na Mtikila mwenyewe kumaliza kujitetea. Hakimu Mugeta alisema anakubaliana na ushauri wa Mtikila uliosema ameamua kufunga ushahidi wake jana licha hapo awali aliahidi kuleta mashahidi wake 10 ili waje kumtetea kwasababu endapo mashahidi hao angewaleta wangezungumza mambo ambayo ameishayazungumza yeye na Bukuku na kwamba hukumu ya kesi hiyo ataitoa Agosti 27 mwaka huu. Mtikila akimaliza kutoa utetezi wake jana alidai kuwa mashitaka aliyoshitakiwa nayo siyo sahihi na kwamba waraka aliousambaza wenye kichwa cha habari kisemacho “Kikwete kuungamiza kabisa ukristo! Ambao ndiyo umesababisha ashitakiwe , siyo wa uchochezi kwani umejaa maneno ya kumsifu mungu. Kwa upande wake shahidi wa pili, Bukuku akitoa ushahidi wake jana, aliieleza mahakama kuwa ni kweli kampuni yao ya uchapaji ya Mwananchi Communication Ltd ilichapisha gazeti la Mwananchi ambalo lilikuwa limenukuu baadhi ya maneno yaliyokuwa kwenye waraka huo unaodaiwa kuwa ni wa uchochezi ila hadi sasa si jeshi la Polisi au Mtikila mwenyewe alishafika ofisini kwao kuilalamikia habari hiyo kuwa imepotoshwa. Awali ilidaiwa kuwa kati ya Januari mwaka 2009 na Aprili 17, mwaka 2010 jijini Dar es Salaam, kwa nia ya uchochezi mshitakiwa alisambaza kwa umma nyaraka zilizosema ‘Kikwete kuuangamiza Kabisa Ukristo', ‘Wakristo wasipounga upesi kuweka Mkristo Ikulu” Katika shitaka la pili, Aprili 16, mwaka 2010 eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam, bila kibali alikutwa akimiliki waraka huo wa uchochezi kwa jamii. Wakati huo huo Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Agnes Mchome jana aliiarisha kesi ya kumteka na kumjeruhi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari , Dk.Steven Ulimboka , raia wa Kenya ,Joshua Mulundi(21) kwasababu kesi hiyo iliku jana jana kwaajili ya kutajwa na wakili wa serikali Mwanaisha Komba alieleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Julai 13 mwaka huu, ilidaiwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Lasdlaus Komanya kuwa Mulundi ambaye ni mkazi wa Murang'a nchini Kenya anadaiwa kuwa Juni 26 mwaka huu, akiwa eneo la Leaders Club alimteka Dk. Ulimboka. Komanya alidai shitaka la pili ni kuwa Juni 26 mwaka huu, akiwa katika eneo la Msitu wa Mwabepande Tegeta, Dar es Salaam kinyume na sheria na mshitakiwa alikana mashitaka hayo na yupo rumande. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Julai 26 mwaka 2012.

3 comments:

Anonymous said...

Hi this iѕ somewhat of off topic but I was wonԁering if blogs uѕe WYЅIWYG
editorѕ or if уou have to manuallу сode with НTML.
I'm starting a blog soon but have no coding skills so I wanted to get guidance from someone with experience. Any help would be enormously appreciated!http://soundcloud.com/user757299359/watch-alex-cross-hd-online
my web page > Alex Cross 2012 Movie

Anonymous said...

Good dау! Do you knοw if they make anу plugins to
safeguaгd against hаckers? I'm kinda paranoid about losing everything I'νe workеd
hard on. Any suggestions?Watch The Office (US) Season 9 Episode 8
My website: Watch The Office (US) Season 9 Episode 8

Anonymous said...

My brother ѕuggеѕted Ι would possibly like this blog.
Hе was totally right. This publish actually mаde my day.
Yοu cаnn't imagine just how a lot time I had spent for this info! Thank you!Silver Linings Playbook Movie Online
Here is my blog post Silver Linings Playbook HD Free Streaming

Powered by Blogger.