Header Ads

NDOA YA DK.SLAA,JOSEPHINE YAPINGWA KORTINI

Na Happiness Katabazi ALIYEKUWA mke wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Rose Kamili Slaa nee Sukum amefungua kesi ya madai kati ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akiomba mahakama hiyo imzuie mumewe Dk.Willibrod Slaa asifunge ndoa na mchumba wake Josephine Mushumbusi. Kwa mujibu wa hati ya madai ya kesi hiyo ya masuala ya ndoa iliyopewa na Na.4/2012 ambayo gazeti hili inayo nakala yake ambayo tayari imepangwa kusikilizwa na Jaji Laurence Kaduri ilifunguliwa mahakamani hapo hivi karibuni na wakali wa mlalamikaji Joseph Thadayo dhidi ya Dk.Slaa na mchumba wa Dk.Slaa, Josephine Mushumbusi. Rose anaiomba mahakama isikubali shauri hilo lipelekwe kwenye Bodi ya Maridhiano ya Masuala ya Ndoa ya kwaajili ya kupatanishwa. Dai la pili, Rose anaiomba mahakama itanganze yeye na Dk.Slaa bado ni wanandoa.Dai la tatu anaiomba mahakama itamke kuwa ndoa baina yake na Dk.Slaa bado halali kisheria na kwamba ndoa nyingine itakayofungwa kinyume na sasa ndoa hiyo itakuwa ni batili. Katika dai lake nne, mlalamikaji ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum(Chadema) huyo anadai mdaiwa wa pili(Josephine) alimshawishi mumewe(Dk.Slaa) kuivuruga ndoa yake na mumewe ambaye ni mdaiwa wa kwanza. “Pia nia ya wadaiwa hao wawili ya kutaka kufunga waliyopanga ifungwe Julai 21 mwaka huu katika eneo lolote lile,ndoa hiyo ihesabike kuwa ni batili. Aidha anaiomba mahakama iwaamuru wadaiwa wamlipe fidia ya shilingi 50,000,000 kama gharama za matunzo ya watoto watoto wawili ambao Emiliana Slaa na Linus Slaa aliyezaliwa mwaka 1987 na kwamba walianza kuishi pamoja na Dk.Slaa kama mume na mke, ambao amekuwa akiwahudumia kwa tangu mwaka 2009 baada ya mume wake kumkimbia. Pia anaiomba mahakama imwamuru mdaiwa wa pili(Josephine) amlipe fidia ya shilingi 500,000,000 kwasababu alimsababishia usumbufu mkubwa na kumharibia ndoa yake na kuongeza kwa kuimba mahakama hiyo impatie nafuu nyingine ambazo itaona inafaa. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Julai 12 mwaka 2012.

No comments:

Powered by Blogger.