KESI YA KUPINGA NDOA YA DK.SLAA YAANZA KUNOGA
Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam,imemtaka Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Dk.Willbrod Slaa na mchumba wake Josephine Mushumbusi ambao ni wadaiwa katika kesi ya kupinga wasifunge ndoa Julai 21 , wawasilishe utetezi wao kwa njia ya maandishi Julai 30 mwaka huu.
Hivi karibuni mke wa Dk.Slaa, Rose Kamili nee Sukum anayetetewa na wakili wa kujitegemea Joseph Thadayo alifungua kesi hiyo ya madai ya ndoa Na.4/2012 dhidi ya wadaiwa hao akiomba mahakama hiyo itoe amri ya kuzuia wadaiwa hao wasifunge ndoa inayokusudiwa kufungwa Julai 21 mwaka hu,kwasababu yeye bado ni mke halali wa Dk.Slaa na jana kesi hiyo ilikuja kwaajili ya kutajwa.
Amri hiyo ilitolewa jana na Jaji Laurance Kaduri ambapo alisema kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya kutajwa na kwamba anawataka wadaiwa wawasilishe utetezi wao kwa njia ya maandishi Julai 30 na mlalamikaji awasilishe hoja zake kama inaona inafaa Agosti 7 na kwamba Agosti 14 mwaka huu, kesi hiyo itakuja kwaajili ya kuanza kusikilizwa.Hata hivyo mlalamikaji wala waidaiwa ambao wanatetewa na wakili wa kujitegemea Mutakyamilwa Philemoni hawakuwepo mahakamani.
Kwa mujibu wa hati ya madai ya kesi hiyo ya masuala ya ndoa,. Rose anaiomba mahakama isikubali shauri hilo lipelekwe kwenye Bodi ya Maridhiano ya Masuala ya Ndoa ya kwaajili ya kupatanishwa. Dai la pili, Rose anaiomba mahakama itanganze yeye na Dk.Slaa bado ni wanandoa.
Dai la tatu anaiomba mahakama itamke kuwa ndoa baina yake na Dk.Slaa bado halali kisheria na kwamba ndoa nyingine itakayofungwa kinyume na sasa ndoa hiyo itakuwa ni batili.
Katika dai lake nne, mlalamikaji ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum(Chadema) huyo anadai mdaiwa wa pili(Josephine) alimshawishi mumewe(Dk.Slaa) kuivuruga ndoa yake na mumewe ambaye ni mdaiwa wa kwanza.
“Pia nia ya wadaiwa hao wawili ya kutaka kufunga waliyopanga ifungwe Julai 21 mwaka huu katika eneo lolote lile,ndoa hiyo ihesabike kuwa ni batili.
Aidha anaiomba mahakama iwaamuru wadaiwa wamlipe fidia ya shilingi 50,000,000 kama gharama za matunzo ya watoto watoto wawili ambao Emiliana Slaa na Linus Slaa aliyezaliwa mwaka 1987 na kwamba walianza kuishi pamoja na Dk.Slaa kama mume na mke, ambao amekuwa akiwahudumia kwa tangu mwaka 2009 baada ya mume wake kumkimbia. Pia anaiomba mahakama imwamuru mdaiwa wa pili(Josephine) amlipe fidia ya shilingi 500,000,000 kwasababu alimsababishia usumbufu mkubwa na kumharibia ndoa yake na kuongeza kwa kuimba mahakama hiyo impatie nafuu nyingine ambazo itaona inafaa
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Julai 13 mwaka 2012
No comments:
Post a Comment