Header Ads

MAHAKAMA KUU YAIPA NAMBA KESI YA LULU


 

Na Happiness Katabazi

HATIMAYE uongozi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, umeipatia namba jarada la kesi ya mauji ya bila kukusudia inayomkbaili msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kama ‘Lulu’.

Habari za kuaminika toka ndani ya Mahakama Kuu zimeeleza kuwa jarada hilo tayari limepwa namba 125/2012 ila bado halijapangiwa jaji wa kuanza kusikiliza.

Desemba 21 mwaka huu, mahakama ya Hakimu Mkazi iliifunga rasmi kesi hiyo iliyokuwa ikiendeshwa katika hatua za awali  na kuiamishia katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kwababu mahakama hiyo ndiyo yenye mamlaka ya kuisikiliza kufuatia wakili mwandamizi wa serikali Shadrack Kimaro siku hiyo kumsomea mashtaka yake kwa mapana mshtakiwa huyo ambapo alieleza kuwa wanakusudia kuleta mashahidi tisa.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Desemba 28 mwaka 2012.

No comments:

Powered by Blogger.