Header Ads

MATUKIO MAKUBWA MAHAKAMANI MWAKA 2012


 LEO ndio Jumatatu ya mwisho ya  mwaka 2012. Kesho panapo majaliwa tunaukaribisha mwaka mpya wa 2012.

Ungana nami mwandishi wa habari za mahakamani wa Gazeti la Tanzania Daima  ili uweze kupata mtiririko wa matukio makubwa yaliyotokea mahakamani kuanzia Januari hadi Desemba mwaka huu.

Na Happiness Katabazi
Desemba 31: Kesi ya Ponda kuendelea leo
 Shahidi wa nne wa upande wa Jamhuri katika kesi ya uchochezi na wizi wa Sh milioni 59 inayomkabili  Katibu wa Taasisi na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu(T), Sheikh Issa Ponda na wafuasi wake 49  leo anatarajia kuanza kupanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuanza kutoa ushahidi wake.
Desemba 28: Korti Kuu yaipa namba kesi ya Lulu
Hatimaye  uongozi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, umeipatia namba jarada la kesi ya mauji ya bila kukusudia inayomkbaili msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kama ‘Lulu’.
Desemba 27: Upelelezi kesi ya Papa Msoffe bado
Upande  wa Jamhuri katika kesi ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Marijani Abdubakari Msoffe(50) maarufu kwa jina la “Papa Msoffe chuma cha reli akishiki kutu’ ’ jana umeieleza tena Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na Hakimu Agnes Mchome akaiarisha kesi hiyo hadi Januari 9 mwaka huu,itakapokuja kwaajili ya kutajwa.
 
Desemba 24; Mahakama Kuu yamnyima dhamana Hassanor
Jaji wa Mahakama Kuu Zainabu Mruke ametupilia mbali ombi la Mwenyekiti wa  Chama Cha Soka Mkoa wa Pwani(COREFA), Hassan Othman Hassan ‘Hassanoo’ lilokuwa likiomba mahakama impatie dhamana.Jaji Mruke alisema mahakama yake imefikia uamuzi wa kumnyima dhamana Hassanoor ambaye kwasasa anakabiliwa na kesi ya Sh. bilioni 1.1  kwa kusafirisha pembe za ndovu  toka Tanzania kwenda Hong Kong nchini China.
Jaji Mruke alisema anamnyima dhamana kwasababu yupo nje kwa dhamana ya kesi Na.209/2011 ya wizi wa Shaba zenye thamani ya milioni 400 na wakati yupo nje ya dhamana ya kesi hiyo amefunguliwa kesi nyingine ya usafirishaji wa pembe za ndovu.
 Desemba 21: Godbles Lema arejeshewa ubunge wake
Mahakama ya Rufaa Tanzania, imetengua hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ,Aprili 15 mwaka huu, iliyokuwa imemvua ubunge Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini(Chadema), Godbles Lema, kwasababu imebaini hukumu ile ilikuwa na mapungu ya kisheria.
Desemba 21: Kesi ya Lulu yaamishiwa Mahakama Kuu:
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, uliifunga rasmi kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ambaye anadaiwa kumuua bila kukusudia msanii mwenzake Steven Kanumba,baada ya upande wa jamhuri kumaliza kumsomea kwa mapana shtaka linalomkabili mshtakiwa huyo(Comittal Procedings), ambapo hakimu huyo alisema hatua hiyo ya upande wa jamhuri kumsomea maelezo hayo kumeifanya mahakaa ya Kisutu kuifunga kesi hiyo na kuiamishia mahakama kuu kwaajili ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa kwasababu mahakama kuuu ndiyo yenye mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo na akaamuru Lulu arudishwe gerezani hadi pale mshtakiwa huyo atakapokea wito wa Mahakama Kuu.
Desemba 21: Mahakama Kuu yasikiliza ombi la Hassanor
Jaji Zainabu Mruke wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, alisikiliza ombi la dhamana lilowasilishwa mbele yake ya Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Pwani(COREFA), Hassan Othman Hassan ‘Hassanoo’ na wenzake sita wamaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa Sh bilioni 1.1 kwa kusafirisha pembe za ndovu toka Tanzania kwenda Hong Kong nchini China.
Desemba 20;Hakimu akwamisha kesi ya Vigogo Suma JKT
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu , Alocye Katema ameshindwa  kutokea mahakamani kwa sababu alikuwa na udhuru na kusababisha shahidi wa kwanza wa upande wa jamhuri katika kesi ya matumuzi mabaya ya madaraka inayomkabili Mkurugenzi wa Shirika la Kujenga Taifa (SUMA JKT), Kanali Ayoub Mwakang’ata na maofisa wengine wa jeshi hilo kushindwa kuanza kutoa ushahidi wake.
Desemba 18:Sangoma anaswa na matunguli mahakama ya Kisutu
Kifaa maalumu kinachotumiwa na wanausalama kuwapekua watu wanaoingia kwenye eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, siku ya kesi ya uchochezi na wizi wa Sh milioni 59 inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49 inapokuja kusikilizwa mahakamani hapo, kimefanikiwa kumnasa mganga wa kienyeji Rajabu Zuberi(30) akiwa na vifaa vyake vya kiganga ‘ matunguli’ ambaye alikuja kufanya mambo ya kishirikina mahakamani hapo ambayo yangeweza kumsaidia mteja wake anayekabiliwa na kesi ya jinai mahakamani.
Desemba 17: Jaji Mkuu awataka mawakili wajikite vijijini
Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman amewataka wamawakili wakujitegemea wapya waende kutoa huduma ya sheria vijijini kwani huko vijijini kuna wananchi wanaoitaji huduma hiyo.
Wito huo ulitolewa leo na Jaji Othman katika sherehe ya 47 ya kuwakubali na kuwasajili mawakili wapya 618 katika viwanja vya Shule ya Sheria Tanzania iliyopo Sinza ‘C’ jijini Dar es Salaam, ambapo alisema hata huko mikoani kuna mahakama pia ambapo wananchi wanataka kuwakilishwa na mawakili wa kujitegemea mahakamani.
Desemba 18: Sheikh Ponda mgonjwa.
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49 ambaye wanakabiliwa na kesi ya uchochezi na wizi wa malighafi zenye thamani ya Sh 59,wakili Mwandamizi wa Serikali Tumaini Kweka alisema kesi hiyo ilikuja kwaajili ya kutajwa na kuendelea kusikilizwa lakini amepokea taarifa toka kwa maofisa wa Jeshi la Magereza kuwa Ponda anayeishi katika gereza la Segerea ni mgonjwa hivyo wameshindwa kumleta mahakamani.
Desemba 11:Mahakama ya Rufaa yakwamisha Rufaa ya DPP v Zombe
Mahakama ya Rufaa nchini jana ilishindwa kuanza kusikiliza rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP), Dk.Eliezer Feleshi dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam (ACP), Abdallah Zombe na wenzake kwa sababu jaji mmoja Semistockles Kaijage anayeunda jopo la majaji watatu anaumwa.
Desemba 7: Chadema yailiza CCM Ubungo
Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam, imetoa amri ya kuiondoa rufaa iliyokuwa imekatwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Ubungo(CCM), Hawa Ng’umbi dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo(Chadema) na wenzake bila gharama baada ya kuridhia maombi ya pande zote mbili zilizokuwa zimeiomba mahakama hiyo iiondoe rufaa hiyo mahakamani.
Desemba 4:Lema atoa sababu 18 kutetea ubunge wake
Aliyekuwa  mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini(Chadema),Godbles Lema ,amewasilisha sababu 18, kuiomba Mahakama ya Rufaa nchini, itengue hukumu ya mahakama kuu Kanda ya Arusha iliyolewa Aprili 15 mwaka, ambapo ilitengua ubunge wake. yotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili mwaka huu ambayo ilitengua ubunge wake.yotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili mwaka huu ambayo ilitengua ubunge wake.
Novemba 29: Katibu Bakwata amruka Ponda
Katibu Mkuu wa Baraza la Kuu la Waislamu(BAKWATA), Suleman Said Lolila(61),amekanusha madai yaliyotolewa na Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49 wanaokabiliwa na kesi uchochezi na wizi wa Sh milioni 59 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kuwa Baraza Kuu la Waislamu nchini(BAKWATA), siyo chombo cha kuwakilisha waislamu wote hapa nchini.
Suleiman ambaye ni shahidi wa kwanza wa upande wa jamhuri katika kesi hiyo, alitoa maelezo hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa wakati akiongozwa na wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka kumuongoza kutoa ushahidi ambapo jana shahidi huyo alimaliza kutoa ushahidi wake.
Novemba 28: Hatiwa atiani kwa makosa ya kufanyabiashara haramu ya kusafirisha binadamu
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,imemtia hatiani mfanyabiashara wa ngozi nchini, Salim Ally (61) kwa makosa ya kusafirisha binadamu na kuwatumisha na kumhukumu kwenda jela miaka 10 au kulipa fidia ya jumla ya milioni 17.
Hukumu hiyo ya kesi hiyo ya ki historia na ya kwanza kutolewa katika Mahakama hiyo tangu Sheria ya Usafirishaji haramu binadamu ya mwaka 2008 ilipotungwa na bunge, ilitolewa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Ilvin Mugeta.
 
Novemba 28:Mahakama yambwaga Hamad Rashid
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali ombi lilotaka mahakama hiyo itoe amri ya kuliita Baraza la Wadhamini wa Chama cha Wananchi(CUF) na wenzake waje wajieleze ni kwanini walikaidi amri ya mahakama na ni kwanini wasitiwe hatiani kwa kosa la kudharau amari ya mahakama ambalo liliwasilishwa mahakamani hapo na Mbunge wa Wawi(CUF), Hamad Rashid na wenzake 10.
Rashid na wenzake waliwasilisha maombi mahakamani hapo Januari 10, 2012,na walikuwa wakiiomba mahakama iwaite Wadhamini wa Cuf wajieleze ni kwa nini wasitiwe hatiani kwa kukiuka amri ya mahakama hiyo kutokana na uamuzi wa Baraza la Taifa la Uongozi la Cuf kumfukuza uanachama Hamad na wenzake.
 
Novemba 23:Maranda,Farijala wahukumiwa tena
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu , imemhukumu kwenda jela miaka miwili kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rajabu Maranda, na wenzake waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya kughushi na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 3.8 katika Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu ya Tanzania (EPA) .
Novemba 27: Hassanor sasa akimbili Mahakama Kuu
Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Pwani (Corefa), Hassani Othman maarufu kama Hasanoo (43) na wenzake watano ambao wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo kosa la uhujumu uchumi na kusafirisha Pembe za ndovu zenye thamani ya Sh.bilioni 1.1 kwenda Hong Kong nchini China, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, amewasilisha ombi la kuomba apatiwe dhamana na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Novemba 23 mwaka huu ; Pembe za ndovu zamfikisha mahakamani Hassanor
Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Pwani (Corefa), Hassani Othman maarufu kama Hasanoo (43) na wenzake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo kosa la uhujumu uchumi na kusafirisha Pembe za ndovu zenye thamani ya Sh.bilioni 1.1 kwenda Hong Kong nchini China.

Novemba 22: Maranda,Farijala wafungwa tenaMahakama ya Kisutu imemhukumu kwenda jela miaka miwili Kada wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Rajabu Maranda,Farijala Hussein na maofisa watatu wa Benki Kuu, waliokuwa wakikabiliwa na makosa kugushi, kuisababishia serikali hasara na wizi wa sh bilioni 3.3 katika akaunti ya EPA.
ya kughushi,na kuisababishia serikali hasara ya Sh.bilioni 3.8 katika Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu ya Tanzania .ya kughushi,na kuisababishia serikali hasara ya Sh.bilioni 3.8 katika Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu ya Tanzania .iliwa na kesi ya kughushi,na kuisababishia serikali hasara ya Sh.bilioni 3.8 katika Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu ya Tanzania .
Novemba 20: Askari wa JWTZ waliomua Swetu Fundikira wahukumiwa kifo
 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imewahukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa askari wawili wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mmoja wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kumuua kwa kusudia, Swetu Fundikira.Askari hao MT 1900 Sajenti Roda Robert (42) wa JKT, Kikosi cha Mbweni, MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ, Kikosi cha Kunduchi na MT 85067 Koplo Mohamed Rashid wa JKT Mbweni.
Oktoba 22: Sheikh Farid aburutwa kortini ,anyimwa dhamana
Mwenyekiti wa Jumuia ya Maimamu Zanzibar Sheikhe Farid hadi Ahmed(41) na wenzake sita wamefikishwa katika  Mahakama ya wilaya ya Mwanakwelekwe,Zanzibar wakikabiliwa na makosa ya  kufanya mikutano na kupelekea ghasia zilizoleta uvunjifu wa amani na uhalibifu wa miundombinu ya barabara.
Oktoba 19:Korti Kuu  yamgomea Dk.Slaa
Hatimaye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali kwa gharama pingamizi lilowasilishwa mbele yake na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Dk.Willbrod Slaa lililokuwa likiomba mahakama hiyo ifute kesi ya madai iliyofunguliwa na mkewe Rose Kamili Slaa nee Sakum akiomba mahakama hiyo imzuie mumewe Dk.Slaa asifunge ndoa na mchumba wake Josephine Mushumbusi.
Oktoba 18: Sheikh Ponda kortini kwa uchochezi, wizi
Sheikh Issa Ponda na wafuasi wake 49 jana walifikishwa katika Mahakama ya Kisutu chini ya ulinzi mkali wa wanausalama kwa kosa la uchochezi na wizi wa malighafi zenye thamani ya Shilingi milioni 59.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP),Dk.Eliezer Feleshi aliwasilishwa mahakamani hapo hati ya kuzuia Ponda asipewe dhamana chini ya kifungu cha 84(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002, ambapo kifungu hicho kinampa mamlaka DPP kufunga dhamana kwa mshtakiwa anayekabiliwa na makosa yanayodhaminika na mahakama inakuwa imefungwa mikono hivyo mahakama inakuwa haina mamlaka ya kuipinga hati hiyo ya DPP hadi pale siku DPP atakapojisikia kuiondoa mahakamani hati hiyo.
Oktoba 15: Shabani Mitanga ashinda kesi
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemwachilia huru  Rais wa zamani wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT), Alhaji Shabani Mintanga, baada ya kuona hana kesi ya kujibu katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya iliyokuwa inamkabili.
Mintanga alikuwa anakabiliwa na kesi ya kula njama na kusafirisha dawa za kulevya kilo 4.8, kupeleka nchini Mauritius, ambapo Mwaka 2008 alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na kesi hiyo, kutokana na mashtaka yaliyokuwa yanamkabili kwa kutokuwa na dhamana kisheria, alikuwa mahabusu miaka yote hiyo.
Oktoba 11:Maofisa elimu kortini kwa wizi
Makaimu Afisa elimu wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Clara Nyongeja, Elizabeth Thomas,Mercy Nyalusi,Simon Pilla na Joseph Kaika wamefikishwa katika Mahakama ya Kisutu mbele ya Hakimu mkazi Agnes Mchome wakikabiliwa na makosa ya matumizi mabaya ya madaraka ya kuibia serikali jumla ya shilingi milioni11.8.
Oktoba 11:Mramba ayasuta mashtaka yake
Waziri wa fedha wa zamani, Basil Mramba ameendelea kuyasuta mashitaka yanayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, na kudai kuwa siyo yeye aliyeiarika nchini kampuni ya Alex Stewart,wala kuiongezea mkataba wa nyongeza kampuni hiyo na wala kuiarifu kuwa ilikuwa imeteuliwa na serikali ya Tanzania kuwa imeshinda tenda na kwamba inahitajika kuja kufanyakazi hapa nchini wala kuingia mkataba na kampuni hiyo.
Mramba aliyasema hayo mbele ya jopo linaongozwa na Jaji John Utamwa, Sam Rumanyika na Hakimu Mkazi Saul Kinemela wakati alipokuwa akihojiwa na wakili wa Waziri wa Nishati na Madini wa zamani, Daniel Yona na Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja, (Elisa Msuya na Profesa Leonard Shaidi), baada ya juzi wakili wa Mramba (Peter Swai) kumaliza kumuongoza mshitakiwa huyo kutoa utetezi wake.
Oktoba 9:Rais Mwinyi apanda kizimbani kutoa ushahidi katika kesi ya kuibiwa Sh.Mil.37
Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ally Hassan Mwinyi amefuata nyayo za Rais wa awamu ya tatu,Benjamin Mkapa kwa kufika katika Mahakama ya Hakimu MKazi Kisutu Dar es Salaam, na kupanda kizimbani na kutoa ushahidi katika kesi za jinai zilizofunguliwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini(DPP), Dk.Eliezer Feleshi dhidi ya washitakiwa wa kesi hizo za jinai.
Rais Mwinyi jana alitua katika mahakama hiyo huku akiongozwa na maofisa Usalama wa Taifa(TISS) kuja kutoa ushahidi katika kesi ya jinai Na. 201/2012 iliyofunguliwa na upande wa Jamhuri dhidi ya wakala wa Mwinyi Abdallah Nassoro Mzombe(39),mbele ya Hakimu Mkazi Genivitus Dudu ambapo mshitakiwa huyo ambaye ni Mfanyabiashara na mkazi wa Kinondoni Mkwajuni anashitakiwa kwa makosa ya kumuibia Rais Mwinyi Sh. 37,440,000 zikiwa ni kodi ya pango katika nyumba mbili zinazomilikiwa na rais huyo mstaafu.
Septemba 27:Kesi ya Dk.Mkopi yafika patamu
Upande wa jamhuri katika kesi ya kudhalau amri ya Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi inayomkabili Rais wa Chama cha Madaktari nchini(MALT), Dk.Namala Mkopi ulimsomea maelezo ya awali mshitakiwa huyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam
Septemba 25: Mtikila ambwaga Kikwete kortini
Hatimaye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam ,imemfutia kesi ya uchochezi ya kuchapisha na kumiliki waraka wa uchochezi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete iliyokuwa ikimkabili Mwenyekiti wa Chama cha Democratic(DP), Mchungaji Christopher Mtikila badaa ya upande wa jamhuri kushindwa kuleta ushahidi wa kuthibitisha kesi hiyo.
Hukumu hiyo ya kesi hiyo ya jinai Na.132/2010 ilitolewa jana mchana na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo,Elvin Mugeta ambapo alianza kwa kuikumbusha mahakama hiyo kuwa mshitakiwa huyo alikuwa akikabiliwa na makosa mawili.Kosa la kwanza ni kusambaza waraka wa uchochezi kinyume na kifungu cha 32(1),(c) cha Sheria ya Magazeti ya mwaka 2002 na kosa la pili ni la kumiliki waraka huo wa uchochezi kinyume na kifungu cha 32(2) cha sheria hiyo.
Oktoba 21:Kesi ya Kibanda yaanza kuunguruma
 
Shahidi wa kwanza wa upande wa jamhuri katika kesi ya kuandika na kuchapisha makala ya uchochezi inayomkabili aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima,Absalom Kibanda, Mkurugezni Msaidizi anayesajili Magazeti, Rafael Hokororo (57) ameieleza Mahakama ya Kisutu kuwa waraka uliondikwa na Mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Samson Mwigamba ulikuwa unashawishi askari wagome na wasipokee amri kutoka kwa wakuu wao.
 
Oktoba 16: Mtoto aliyekojolea Korani Mbagala kortini
Mtoto(jina tunaliifadhi), amefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Devota Kisoka kwa kosa kudhalilisha na kukojolea kitabu kitakatifu cha dini ya Kiislamu ,Oktoba 10 mwaka huu, huko Mbagala.
 
Oktoba:16:Walichoma makanisa Mbagala watinga kortini
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), amefungua kesi nne kwa mpigo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa washtakiwa tofauti ambao wanakabiliwa na makosa ya kuchoma moto makanisa Mbagala, wizi,uharibu wa mali za watu na unyang’nyi wa kutumia silaha katika vurugu za kidini zilizotokea Oktoba 10 mwaka huu huko Mbagala.

Septemba 10: Kesi ya Kibanda yashika kasi
Hatimaye upande wa Jamhuri katika kesi ya kuandika na kuchapisha makala ya uchochezi inayomkabili Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda na wenzake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, uliupatia upande wa utetezi nakala ya mlalamikaji katika kesi hiyo kama ulivyokuwa umeamriwa na mahakama hiyo kufanya hivyo.
 
Septemba 10: Mpendazoe amgwaya Dk.Mahanga
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman ameliondoa Mahakama ya Rufani nchini,ombi la kusudio la kukata rufaa iliyowasilishwa Mahakama hapo, na Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Fredy Mpendazoe lilokuwa likitaka kupinga hukumu ya Mahakama Kuu ambayo ilitamka kuwa Mbunge wa jimbo la Segerea(CCM), Dk.Makongoro Mahanga kuwa ni mbunge halali, kufuatia wakili wa Mpendazeoe, Peter Kibatala kuwasilisha ombi la kuiomba mahakama hiyo iondoe kusudio hilo lilokuwa limewasilishwa na mteja wake.
 
Septemba 6: Dowans yaibwaga tena Tanesco
 
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia ombi la Shirika la Umeme (TANESCO) lilolokuwa likiomba mahakama hiyo iwapatie ruhusa ya kwenda kukata rufaa mahakama ya rufaa ya kupinga itoe amri ya kuzuia utekelezwa wa ukazaji wa hukumu ya mahakama hiyo ambayo iliruhusu tuzo ya Dola za Kimarekani 65,812,630.03 iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa migogoro ya Kibiashara (ICC) Novemba 15 mwaka 2010 kwa kampuni ya Dowans Hodlings SA(Costa Rica)Dowans Tanzania LTD isajiliwe hapa nchini.
 
Septemba 5: Serukamba aibwaga Chadema

Mahakama ya rufaani nchini, imetupilia mbali kwa gharama maombi ya kufanyiwa mapitio ya hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Tabora Machi 28 mwaka huu, ambayo ilisema kuwa taratibu za sheria ya uchaguzi na matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 yaliomtangaza Peter Serukamba (CCM), kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini, hayakukiuka sheria.
 
Agosti 21:Mahakama yatengua  ubunge wa Dk.Kafumu
 
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imemvua ubunge aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Igunga(CCM), Dk.Dalali  Kafumu kwa maelezo kuwa taratibu za sheria za uchaguzi zilikiukwa katika kampeni za uchaguzi wa jimbo hilo.
 
Septemba:  Polisi alimua Daudi Mwangosi kortini
Askari polisi  Pasificus Cleophace Simon (23) amefikishwa  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Iringa kwa tuhuma ya kumuua mwandishi huyo katika hafla ya ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa, uliofanyika Septemba 2, mwaka huu.

Agosti 22:Mramba nilisamehe kodi kwa amri ya Rais Mkapa
Basil Mramba (71), Waziri mwandamizi aliyetumikia awamu nne zote za nchi hii katika wizara mbalimbali, jana alianza kujitetea dhidi ya kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kumtaja Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, kuwa ndiye aliyemuagiza kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart.
 
Agosti 10: Papa Msoffe kortini kwa mauji

Mfanyabaishara maarufu jijini Dar es Salaam, mfanyabaishara maarufu jijini Marijani Abdubakari Msoffe(50) maarufu kwa jina la “Papa Msoffe chuma cha reli akishi kutu’ amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la kumuua kwa kukusudia Onesphory Kitoli.Hadi sasa Msoffe ambaye ameamishiwa gereza la Ukonga anaendelea kusota rumande kwasababu kesi inayomkabili haina dhamana.
 
Agosti 9:Mahalu, Mkapa wambwaga Kikwete
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu , imemwachilia huru aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na aliyekuwa Meneja Utawala na fedha Grace Martin waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa Euro milioni mbili kutokana na ushahidi wa jamhuri kushindwa kuwatia hatiani.
 
Hukumu hiyo inaweza kutafsiriwa kama ni kubwagwa kwa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, kutokana na hatua ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa kukubali kupanda kizimbani na kumtetea Mahalu dhidi ya serikali, tukio ambalo ni la kwanza katika historia ya nchi hii. Hukumu hiyo ya kihistoria ya kesi ya uhujumu uchumi Na.1/2007 ilitolewa jana Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo Ilvin Mugeta.
Agosti 2: Mahakama yasema mgomo wa walimu ni batili
Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi jijini Dar es Salaam, imesema mgomo wa walimu ni batili kwasababu haukuzingatia matakwa ya kifungu cha 84(1),(2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazi ya mwaka 2004 na uliandaliwa kwa dhamila mbaya. Jaji Sophia Wambura ndiye aliyetoa uamuzi huo ambapo katika uamuzi wake huo pia aliwataka walimu wote kurejea mara moja kazini.
Julai 18:Kakobe akwaa kisiki mahakamani
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBC) Zakaria Kakobe dhidi ya wachungaji wa tatu wa kanisa hilo waliomfungulia kesi ya ubadhirifu wa fedha za kanisa hilo. Kesi hiyo namba 79/2011 ilifunguliwa Mei 26 mwaka 2011 na wachungaji watatu wa kanisa hilo, Mchungaji Deuzidelius Patrick, Angelo Mutasingwa na Benedict Kaduma. Wachungaji hao wanamtuhumu Askofu Kakobe kuwa amekuwa akifanya ubadhirifu wa fedha wa kanisa hilo Sh.bilioni 14 14 na anakiuka matakwa ya Katiba ya kanisa hilo.
Julai 24: Maranda,Farijala wafungwa tena
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kwa mara ya pili tena imemuhukumu Kada wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Rajabu Maranda na mpwa wake Farijala Hussein imewahukumu kwenda jela miaka mitatu kila mmoja kwasababu imewakuta na hatia ya makosa sita likiwemo kosa la kujipatia Shilingi bilioni mbili kwa njia ya udanganyifu toka katika Akaunti ya Madeni ya Nje(EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania kwa njia ya udanganyifu.
Sambamba na kutiwa hatiani na mahakama hiyo pia Mwenyekiti wa jopo la Mahakimu Wakazi waliokuwa wakisikiliza kesi Jaji Fatma Masengi alitoa hukumu yake peke yake inayotofautiana na wanajopo wenzie ambao ni Hakimu Mkazi Projest Kayohza na Catherine Revocate ambayo iliwaachiria huru washitakiwa na ambapo hukumu ya Jaji Masengi imebaki kuwa katika kumbukumbu za mahakama na hukumu ya mahakama ni ile iliyotolewa na mahakimu hao wawili kwasababu sheria inasema wengi wape.
Julai 13:Aliyemjeruhi Dk.Ulimboka kortini
MTU mmoja ambaye ni raia wa Kenya,Joshua Mulundi(21) alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu , akikabiliwa na makosa ya kumteka na kutaka kumuua Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk.Steven Ulimboka. Wakili wa serikali Ladslaus Komanya mbele ya Hakimu Agnes Mchome, alidai kuwa Mulundi ambaye makazi yake Murang'a nchini Kenya anadaiwa kuwa Juni 26 mwaka huu, akiwa eneo la Leaders Club alimteka Dk. Ulimboka. Komanya alidai shitaka la pili ni kuwa Juni 26 mwaka huu, akiwa katika eneo la Msitu wa Mwabepande Tegeta, Dar es Salaam kinyume na sheria mshitakiwa huyo alijaribu kumsababishia kifo Dk. Ulimboka. Hakimu Mchome alisema mshtakiwa hatakiwi kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo, kwani Mahakama Kuu ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Julai 11:Ndoa ya Dk.Slaa yapingwa mahakamani
Mke wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Rose Kamili Slaa nee Sukum amefungua kesi ya madai kati ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akiomba mahakama hiyo imzuie mumewe Dk.Willibrod Slaa asifunge ndoa na mchumba wake Josephine Mushumbusi.
 
Julai 11:Mahalu hana hatia-Mawakili
Aliyekuwa  Balozi wa Tanzania nchini Italia Profesa Costa Mahalu na Meneja Utawala na Fedha, Grace Martin wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, isiwaone wanahatia katika kesi ya wizi wa Euro Milioni tatu kwasababu upande wa Jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi wa kutenda makosa hayo.
 
Julai 12:Mahalu ana hatia-Serikali
Upande wa Jamhuri katika kesi wizi wa Euro milioni mbili inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na Grace Martin wamiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, iwaone washitakiwa hao wana hatia kwa sababu washitakiwa wameshindwa kuleta ushahidi mathubuti ambao unaonyesha hawakutenda makosa hayo.
 
Julai 10:Rais wa Madaktari afikishwa mahakamani
Rais wa Chama cha Madaktari nchini(MALT), Dk.Namala Mkopi jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,chini ya ulinzi mkali wa polisi akikabiliwa na makosa mawili likiwemo kosa la kudharau amri halali ya Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi.
 
Julai 2:Vigogo Suma JKT kortini
Mkurugenzi wa Shirika Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) Kanali Ayoub Mwakang’ata na maofisa wenzake sita wa jeshi hilo jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka saba ya kula njama na matumizi mabaya ya madaraka. Mbali na Kanali Mwakang’ta washitakiwa wengine ni Luteni kanali Mkohi Kichogo,Luteni Kanali Paul Mayavi,Meja Peter Lushika,Sajenti John Lazier,Meja Yohana Nyichi na Mkurugenzi wa Miradi ya Matrekta wa SUMA JKT-Luteni Kanali Felex Samillan. Mawakili toka ofisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa(TAKUKURU), Dominsian Kessy na Ben Lincoln walidai mbele ya Hakimu Mkazi Alocye Katemana na kuwa kosa la kwanza ni la matumizi mabaya ya madaraka kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007, inayowakabili washitakiwa wote. Wakili Kessy alidai kuwa Machi 5 mwaka 2009 katika chumba cha mikutano cha ofisi ya SUMA JKT Dar es salaam,wakiwa ni wajumbe wa bodi na Bodi ya Tenda ya SUMA JKT kwa makusudi walitumia madaraka yao vibaya kwa kutoa maamuzi ya bodi hiyo ambayo yaliyoonyesha yametolewa na TAKOPA kwa madhumuni ya kununua magari na vifaa vya ujenzi bila kupata idhini ya kutoka Bodi ya ya Wakurugenzi ya TAKOPA.
 
Julai 23:Tindu Lissu ashinda kesi ya kupinga ubunge wake
Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma imetupilia  mbali kesi ya kupinga ubunge wa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki CHADEMA,Tundu Lissu kwa maelezo kuwa mbunge huyo kesi hiyo haina mantiki yoyote.
Julai 17; Vigogo wa Deci wana kesi ya kujibu
WAKURUGENZI watano wa Taasisi ya Kusimamia na Kuendesha Upatu (Deci), wanaokabiliwa na kesi ya kuendesha shughuli za upatu bila kibali wamepatikana na kesi ya kujibu dhidi ya mashtaka yanayowakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Julai 28:Vigogo Bodi ya PSPT kortini
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Watalaam wa Manunuzi na Ugavi (PSPT), Clemence Tesha na wenzake jana walijikuta wakifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wakikabiliwa na makosa ya matumizi mabaya ya madaraka.
Juni 4:Mbunge Badwel  kortini kwa rushwa
Mbunge  wa Jimbo la Bahi(CCM), Omary Ahmed Badwel(43) jana alijikuta akifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), kwa makosa ya rushwa ya shilingi Milioni moja toka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Jonathan Liana.Kesi hivi sasa imefikia hatua ya mashahidi wa upande wa jamhuri kuendelea kutoa ushahidi wao.
Juni 27:Mramba,Yona na Mgonja wana kesi ya kujibu
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaona mawaziri wa zamani Basil Mramba,Daniel Yona na Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja kuwa wana kesi ya kujibu.
Mei 8:Garce Martin atoa utetezi
Mshtakiwa wa pili katika kesi ya uhujumu,Grace Martin ameiomba mahakama ya Kisutu imuone hana hatia kwa mashtaka yote yanayomkabili kwasababu hakutenda makosa hayo wakati akiwa na wadhifa wa Meneja Utawala na Fedha wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia.
Mei 7:Rais Mkapa amkaanga JK mahakamani
RAIS mstaafu, Benjamin Mkapa, jana aliikaanga serikali ya Jakaya Kikwete mahakamani akidai kuwa hakuna ubadhirifu wowote uliofanywa na aliyekuwa Balozi wa Italia, Prof. Costa Mahalu, katika ununuzi wa jengo la ubalozi nchini humo.
 
Akiongozwa na wakili wa utetezi, Alex Mgongolwa, baada ya kuapa alieleza kuwa kati ya mwaka 1995-2005 akiwa Rais alifahamu ununuzi wa jengo la ubalozi nchini Italia kwa euro 3,098,741.40, na kuwa hata aliyekuwa Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye ni Rais wa sasa, Jakaya Kikwete alikubaliana na ununuzi huo.
Mkapa ambaye ni shahidi wa Mahalu katika kesi hiyo alisema mwaka 2003 yeye ndiye aliyekwenda mjini Rome-Italia kulizindua jengo hilo la kisasa, Profesa Mahalu akiwa balozi.
 
“Serikali yangu iliarifiwa bei na taratibu za kulinunua na mimi kama Rais wa nchi nilitaarifiwa kuwa muuzaji alitaka malipo yafanywe mara mbili tofauti katika akanti zake …na mimi kwa niaba ya serikali yangu nikatoa idhini linunuliwe kwa mtindo huo nilioutaja hapo juu,” alidai Rais Mkapa.

Mei 2: Dk.Mahanga ashinda kesi
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kupinga ubunge wa Mbunge wa Jimbo la Segerea(CCM), Dk.Makongoro Mahakanga iliyokuwa imefunguliwa na alikuwa mgombea kiti hicho kwa tiketi ya (Chadema), Fred Mpendazoe kwa maelezo kuwa kesi hiyo haina mantiki kisheria na mahakama hiyo kumtangaza Dk.Mahanga kuwa ndiye mbunge halali wa jimbo hilo.
Mei 29:Mamia wamzika wakili Stanslaus Boniface
Mkurugenzi  wa Mashitaka nchini,Dk.Eliezer Feleshi amemwelezea aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa mashitaka marehemu Stanslaus Boniface(44) ,kuwa alikuwa ni mtumishi aliyejituma ,mwadilifu na aliyekuwa na ushirikiano na watumishi wa kada zote bila kujali umri wala cheo chake. Dk.Feleshi aliyasema hayo leo katika ibada ya kuuga mwili wa marehemu Boniface iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na kisha mwili wa marehemu ulizikwa katika makaburi ya Kinondoni.
Mei 29:Idd Simba aburuzwa kortini
Hatimaye  sakata la ufisadi katika Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam(UDA), lilifikia tamati kwa serikali kumfikisha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo Idd Simba kwa makosa ya kughushi,kujipatia fedha kwa njia ya udangayanyifu na kulisababishia shirika la Usafiri Dar es Salaam(UDA) Ltd shilingi bilioni 2.3. Mbali na Simba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya UDA ,wengine ni Mkurugenzi Salim Mwaking’inda na Meneja Mkuu wa shirika hilo Victor Milanzi.
Mei 27:Wakili maarufu Stanslaus Boniface Jembeafariki
Mkurugenzi  Msaidizi wa ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, Stanslaus Boniface Makulilo (44) ‘Jembe’ amefariki ghafla usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashitaka nchini(DPP), Dk.Eliezer Feleshi alilithibishia Tanzania Daima jana asubuhi kutokea kwa kifo hicho ambapo alisema bado ofisi yake na taifa limepata pigo kubwa lakuondokewa na gwiji hilo la uendeshaji wa mashitaka hususani ya jinai hapa nchini na kwamba mchango wake mzuri katika uendeshaji wa kesi hususani za jinai hautasaulika na utaenziwa.
Dk.Feleshi alikuwa akizungumza na gazeti hili kwa uzuni alisema Jumamosi jioni Boniface ambaye pia alikuwa Msimamizi wa Uendeshaji wa Kesi zenye maslahi kwa umma, aliingia Dar es Salaam, akitokea Moshi kwaajili ya kutoa mafunzo ya jinsi ya uendeshaji wa mashitaka kwa maofisa wa Idara ya Uhamiaji akiwa mwenye afya njema na alirejea nyumbani kwake Kinondoni lakini ilipofika usiku wa siku hiyo hali yake ilibadilika ghafla na kukimbizwa katika Hospitali ya Regency kwaajili ya matibabu.
Mei 31:Kajala alia asema Segerea siyo sehemu ya matanuzi
Msanii  wa filamu nchini, Kajala Masanja, jana alimwaga machozi na kuujia juu upande wa jamhuri katika kesi inayomkabili ya utakatishaji fedha haramu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, akiushinikiza ulete mashahidi haraka kwani mahabusu anakoishi siyo sehemu ya starehe. Kajala alitoa shinikizo hilo mbele ya Hakimu Mkazi, Sundi Fimbo, muda mfupi baada ya wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rsuhwa (TAKUKURU), Leonard Swai, kuikumbukusha mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja jana kwa ajili ya upande wa jamhuri kuanza kutoa ushahidi wao, lakini akadai hilo halitaweza kufanyika, kwa sababu hajaja na mashahidi na anaomba kesi hiyo iahirishwe. Baada ya wakili huyo kumaliza kutoa maelezo hayo, ndipo Kajala akanyosha kidole na kuomba ruhusa ya mahakama ili aweze kuzungumza jambo. “Mheshimiwa hakimu, hivi huyu wakili wa serikali anafikiri kule Segerea ninakoishi kwa sasa ni sehemu ya starehe? Mahabusu kunatisha, wewe wakili wa serikali lete mashahidi kesi isikilizwe,” alidai Kajala huku akitokwa na machozi.
Mei 24:Mnyika ambwaga Ngumbi kortini
Hatimaye  Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imepigilia msumari wa mwisho kwa kusema kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya (Chadema), John Mnyika ndiye mbunge halali wa jimbo hilo na matokeo ya uchaguzi ya jimbo hilo yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi Novemba mwaka 2010,yalikidhi matakwa ya kisheria.
Aprili 30:Mahakama yatengua ubunge wa Aeshi Hillal
Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga imetengua ubunge wa aliyekuwa mbungu  wa Jimbo la Sumbawanga Mjini(CCM), Aeshi Hillali ililiyokuwa imefunguliwa na aliyekuwa mgombea wa Chadema, katika uchaguzi mkuu uliopita ambaye alikuwa akiomba mahakama hiyo mvue ubunge kwasababu alishindwa kwa hira.
Aprili 23: Waziri Ntagazwa kortini kwa udanganyifu
Aliyekuwa  Waziri mwandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu tofauti Arcado Ntagazwa(65) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kwa kosa moja tu la kujipatia kofia,fulana zenye jumla ya thamani ya shilingi milioni 74.9 kwa njia ya udanganyifu.
Aprili 5:Lema avuliwa ubunge na mahakama
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetoa hukumu ya kumvua ubunge aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini(Chadema), baada ya kumtia hatiani kwa makosa ya kutoa lugha ya udhalilisha katika kampeni za uchaguzi mkuu wa jimbo hilo mwaka 2010.
Machi 27: Hakimu Waliarwande Lema akataliwa na Jamhuri
Mawakili  wa Serikali katika kesi ya jinai Na.149/2010 ya utakatishaji fedha haramu ya zaidi ya Shilingi bilioni 3.8 inayomkabili Afisa wa Mamlaka ya Mapato(TRA), Justice Katiti na wenzake,katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, jana waliwasilisha ombi la kumuomba Hakimu Mkazi anayesikiliza kesi hiyo Waliarwande Lema ajitoe kwenye kesi hiyo kwasababu hawana imani naye.
Machi 27:Mawakili Mramba hana kesi ya kujibu
Aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imuone hana kesi ya kujibu na afutiwe kesi inayomkabili ya matumuzi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya Shilingi bilioni 11.7 kwasababu upande wa Jamhuri katika kesi hiyo umeshindwa kuthibitisha kesi yake bila kuacha mashaka.
Machi 22:Mtikila amkataa hakimu Fimbo
Ikiwa  ni siku chache baada ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Sundi Findo, atoe uamuzi wa kumuona Mwenyekiti wa chama cha Democratic(DP), Mchungaji Christopher Mtikila ana kesi ya kujibu katika kesi ya kuchapisha na kusamba waraka wa uchochezi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete , Mtikila amewasilisha mahakamani hapo ombi la kumuomba hakimu huyo ajitoe kwenye kesi yake ya jinai Na.132/2011 kwasababu hawezi kumtendea haki.
Machi 15: Kajala kortini kwa utakatishaji fedha
Msanii  wa filamu nchini, Kajala Masanja na mumewe,  walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na makosa ya utakatishaji fedha haramu.
Machi 15:Mashahidi 10 kumvaa Liyumba
Upande wa Jamhuri katika kesi ya kukutwa na simu gerezani inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania, Amatus Liyumba umeiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kuwa unatarajia kuleta jumla ya mashahidi 10 na vielelezo 10 katika kesi hiyo siku itakapoanza kusikilizwa.
Machi 13:Mtikila anaswa kesi ya kumwita JK gaidi
Hatimaye  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imesema Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Part(DP), Mchungaji Christopher Mtikila ana kesi ya kujibu katika kesi ya kuchapisha na kuusambaza waraka wa uchochezi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete.
Machi 7:Kibanda abadilishiwa hati ya mashtaka
Upande  wa Jamhuri katika kuchapisha makala ya uchochezi inayomkabili Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda na mwandishi Samson Mwigamba jana ulishindwa kuwasomea maelezo ya awali washtakiwa hao na badala yake umeibadilisha hati ya mashtaka na pia kumuongeza mshtakiwa mmoja ambaye ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Comunication, Theophil Makunga.
Machi 31:JK alinipa idhini ya kununua jengo la ubalozi-Mahalu
Aliyekuwa  Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Rais Jakaya Kikwete ndiye aliyempatia mamlaka ya kisheria (Special Power of Attoney) ya kununua jengo la Ubalozi wa Tanzania nchi Italia kwa kutimia njia ya mikataba miwili kwa thamani ya Euro 3,098,034.Mahalu alitoa madai hayo wakati akimaliza kutoa ushahidi wake leo.
Februali 23: Washtakiwa kesi ya Samaki wa Magufulijela miaka 30
Mahakama  Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeandika  historia mpya kwa hatua yake ya kuwatia hatiani washtakiwa wawili wa kesi ya uvuvi haramu katika Ukanda wa Tanzania maarufu ‘Kesi ya Samaki wa Magufuli’ na kuwahukumu kwenda jela jumla ya miaka 30 au kulipa faini ya jumla ya Shilingi bilioni 22.

Sambamba na hilo mahakama hiyo imeridhia ombi Kiongozi wa jopo la mawakili wa serikali lilokuwa likiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali Biswalo Mganga aliyekuwa akisaidiwa na Dk.Deo Nangela ,Prosper Mwangamila na Hamidu Mwanga aliloliwasilisha chini ya kifungu cha 351 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 , ambalo aliomba mahakama hiyo itoe amri ya meli hiyo kutaifishwa na serikali ya Tanzania.

Februali 20:Dowans yaibwaga tena Tanesco
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali ombi la Shirika la Umeme (TANESCO) lilokuwa linaomba mahakama iwaruhusu kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa nchini kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyotolewa Septemba 28 mwaka jana,ambayo iliruhusu tuzo ya Kampuni ya Dowans iliyopewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuhuhishi wa migogoro ya Kibiashara(ICC) isajiliwe hapa nchini kwasababu hiyo haina mamlaka ya kuwaruhsu kwenda katika mahakama hiyo ya juu nchini.
Januari  23: Jela kwa kuiba Power Windor mahakamani
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ,imemhukumu kifungo cha miaka  mitano jela, Deogratius  Owiso baada ya kumkuta na hatia ya kuiba Power windor  katika gari lenye usajili Na.T 331 BHY aina ya Toyota Land  Cruser mali ya Adrian Muyungi, lilokuwa limeegeshwa katika eneo hilo la mahakama hiyo.
Januari 13: Mgombea urais wa upinzani Burundi afikishwa mahakamani Kisutu
Aliyekuwa  mgombea urais wa chama kimoja cha upinzani nchini Burundi, Alex Sinduhnje, jana alifikishwa katika mahabusu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, lakini hata hivyo hakuweza kupandishwa kizimbani.
Januari 11:Wanafunzi UDSM  waenda jela kwa kukosa dhamana
Wafunzi  wanne kati ya 51 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wanaokabiliwa na kesi ya kufanya mkusanyiko haramu wamepelekwa rumande baada ya kushindwa kukamilisha masharti ya dhamana waliyopewa.

Waliopelekwa rumande ni Elias Mwambapa, Alphonce Lusako, Moris Denis na Jabir Ndimbo ambao walishindwa kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja wa kuaminika na kusaini hati ya dhamana ya Sh 1 milioni kwa kila mshtakiwa.
Januari 10:Hamad Rashid atia kitanzi CUF kortini
Hatimaye  mbunge wa Wawi Hamad Rashid Mohamed(CUF), na wenzake 10 jana waliwasilisha maombi madogo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wakiomba mahakama hiyo itamke kuwa uamuzi wa Baraza la Uongozi Taifa la chama hicho uliomvua uanachama yeye na wenzake ni batili.
Januari 10: Raia wa Burundi kortini kwa kukutwa na risasi 682
Raia  wa Burundi, Ismail Stefano (39) jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka ya kukutwa na silaha mbili aina ya SMG na risasi 682.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika;
Simu: 0716 774494
Blog:www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook: happy katabazi
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatatu. Desemba 31 mwaka 2012.
 

No comments:

Powered by Blogger.