MAHAKAMA KUU YAMNYIMA DHAMAMA HASSANOR
Na Happiness
Katabazi
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam,
imemnyima dhamana Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Pwani (COREFA),
Hassan Othman Hassan ‘Hassanoo’ na kuwapatia dhamana wenzake sita wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi
wa shilingi bilioni 1.1 kwa kusafirisha pembe za ndovu toka Tanzania kwenda
Hong Kong, China kwa maelezo kuwa
Hassanor anakabiliwa na kesi hiyo mpya wakati yupo nje kwa dhamana
katika kesi ya Na. 209/2011 ya tuhuma za kula njama na kuiba tani 26 za shaba
zenye thamani ya shilingi milioni 400, mali ya Kampuni ya Liberty Express Ltd
ya Dar es Salaam.
Uamuzi huo ulitolewa
jana na Jaji Zainabu Mruke ambapo alisema ombi hilo la kuomba lipatiwe dhamana
liliwasilishwa na Hassanor na wenzake sita waliokuwa wakitetewa na mawakili wa
kujitegemea Richard Rweyongeza ambaye jana hakutokea mahakamani, Majura Magafu,
Mark Antony, Charles Semgalawa na Aliko Mwamunenge na mahakama hiyo
ikayasikiliza maombi hayo Ijumaa iliyopita na upande wa Jamhuri uliokuwa
ukiwakilishwa na mawakili waandamizi wa serikali Biswalo Mganga,Faraja
Nchimbi,Lilian Itembo, Bernad Ikongora na Mutalemwa Kishenyi ambapo walikubali
mwombaji wa 2-7 wapewe dhamana isipokuwa mwombaji wa kwanza Hassanor asipewe
dhamana kwasababu emetenda kesi hiyo mpya ya uhujumu uchumi wakati yupo nje kwa
dhamana kwa kesi wizi wa Shaba Na.209/2011.
Jaji Mruke alisema baada ya kupitia hoja za pande zote mbili
amefikia uamuzi wa kukubaliana na hoja wakili wa serikali Mganga za kumnyima
dhamana Hassanor kwasababu anakabiliwa na kesi mpya wakati yupo nje kwa dhamana
ya kesi nyingine na 209/2011 kwamba kifungu cha 36 (4)(c) cha Sheria ya Uhujumu
Uchumi ya mwaka 2002, na kwamba kifungu hicho kinakataza mshtakiwa alitenda
makosa mapya wakati yupo nje kwa dhamana ya kesi ya nyingine inayoendelea
,asipewe dhamana na mahakama.
“Mimi ni jaji ninayefuata sheria kwahiyo siwezi kupindisha
sheria na kwa kuwa kifungu hicho kipo wazi kabisa basi mahakama hii inatamka
kuwa imemnyima dhamana Hassanor kwa sababu anakabiliwa na kesi nyingine na
inawapatia dhamana washitakiwa wengine ambapo kila mmoja atatakiwa kusalimisha
hati yake ya kusafiria,asaini bondi au fedha taslimu sh.Milioni 50, asitoke nje
ya mkoa bila kibali cha msajili wa Mahakama Kuu, na nyaraka hizo waziwasilishe
Mahakama ya Kisutu na kisha ziletwe kwa Msajili wa Mahakama Kuu kwaajili ya
kuakikiwa”alisema jaji Mruke.
Na kwa uamuzi huo wa mahakama, utamfanya Hassanor hivi sasa
aendelee kusota gerezani na awe anatokea
gerezani kuja katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuudhulia kesi zake hizo
mbili zinazomkabili.
Hata hivyo waombaji hao walishindwa kutimiza masharti hayo
jana wakarudishwa rumande.Baadhi ya ndugu na jamaa wa Hassanor waliokuwa
wamefika mahakamani hapo kusikiliza uamuzi huo, waliuwa wakijifuta machozi kwa
uzuni.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne , Desemba 25 mwaka 2012.
1 comment:
It's not my first time to pay a visit this web page, i am visiting this web page dailly and get nice information from here every day.Watch The Twilight Saga: Breaking Dawn - Part 2 2012
My web-site ... Watch The Twilight Saga: Breaking Dawn - Part 2 2012
Post a Comment