LEMA ATOA SABABU 18 KUTETEA UBUNGE WAKE
ALIYEKUWA mbunge wa Jimbo la Arusha
Mjini(Chadema),Godbles Lema ,amewasilisha sababu 18, kuiomba Mahakama ya Rufaa nchini, itengue hukumu ya awali iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili mwaka huu ambayo ilitengua ubunge wake.
Ombi hilo lilitolewa na
mawakili wa mwomba rufaa(Lema),Method Kimomogoro na Tundu Lissu
mbele ya jopo la majaji wa mahakama ya rufaa linaloongozwa na
Natharia Salum Massati jana wakati rufaa hiyo iliyokatwa na Lema ilipokuja
kwaajili ya kusikilizwa na ambapo ilisikilizwa na kunalizika.mawakili wa wajibu
rufaa ni Aluthe Mugwai na Modest akida na wakili Msimamizi wa uchaguzi na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni Timon Vitalis.
Wakili Kimomogoro , alieleza mahakama
kuwa rufaa yao ya mteja wake ina jumla ya sababu 18 za kupinga
hukumu iliyotolewa na jaji Gabriel Rwakibalila wa mahakama kuu kanda ya arusha
ambayo ilitengua ubunge wake baada ya kumtia hatiani kwa makosa ya kutoa lugha
za kumkashfu aliyekuwa mgombea mwenzie kwa tiketi ya CCM, Dk.Batrida Buriani na
pia hukumu ile ilimfungia Lema kwa kipindi cha miaka mitano kugombea
ubunge.
Alidai jaji Rwakibalila alijielekeza
vibaya katika hukumu yake alivyosema kuwa kesi za uchaguzi hazitawaliwi na
kanuni za sheria za Uingereza kwani kuna maamuzi ya kesi mbalimbali
yalikwishatolewa na mahakama hiyo ya rufaa na mahakama kuu hapa nchini na
yakuruhusu kesi za uchaguzi ziamliwe kwa kutumia kanuni za sheria za
Uingereza.
Hoja ya ya pili wakili Kimomogoro
alidai jaji rwakibalila alijielekeza vibaya kwa kuruhusu wajibu rufaa, wasitaje
maneno kwenye hati yao ya madai ambayo walidai ni maneno ya udhalilishaji wa
kijinsia na dini ambayo yalitolewa na mwomba Rufaa(Lema), kwenye kampeni dhidi
ya Dk.Burian.
Hoja nyingine ni kwamba hakuna
ushahidi wowote unaonyesha wajibu rufaa kweli ni walioandikishwa kupiga kura
katika jimbo la arusha mjini.
Hoja ya nyingine ni ni
kwamba jaji alikosea kisheria kusema kuwa mtu yoyote akiwemo mpiga kula ana haki
ya kufungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo ambalo yeye ni mpiga
kura na kuongeza kuwa wao wanaomba mahakama ya rufaa itamke kuwa wale wajibu
rufaa (wapiga kula wa jimbo la arusha waliofungua kesi ile),walikuwa hawana haki
ya kisheria ya kufungua kesi ile ya kupinga Ubunge wa Lema kwani mwenye haki ya
kufungua kesi ile alikuwa Dk.Batrida kwani ndiye aliyekashfiwa na kuongeza kuwa
mpiga kura hana haki ya kufungua kesi ya kupinga ubunge ule kwani
haki zao hazikuvunjwa.
Aidha katika hoja nyingine alidai
kuwa jaji yule hakutumia maamuzi ya kesi za mahakama rufaa wala
vifungu vya sheria ambazo mawakili wa pande zote mbili ambazo kesi zilie
waliziwasilisha mbele yake katika majumuisho yao ya mwisho ambapo maamuzi ya
mahakama ya rufaa katika kesi zile mahakama ilisitiza kuwa nilazima kesi
isitibitishwe bila kuacha mashaka yoyote na katika hukumu ile ya Jaji
Rwakibalila imeacha mashaka mengi na ndiyo maana mwomba rufaa
anadai jaji yule alikosea.
Baada ya Kimomogoro kuwasilisha hoja
hiyo iliyodai jaji rwakibalila hakutumia maamuzi ya kesi zilizowasilishwa mbele
yake na mawakili wa pnde mbili, Jaji Massati alisema alisikika akisema si lazima
jaji au hakimu atumie kesi zilizowasilishwa mbele yake na mawakili katika kutoa
uamuzi wake na kusababisha watu akuangua vicheko.
Hoja nyingine ni kwamba hukumu ile
iliegemea katika ushahidi wa mdomo tu bila ya kuwepo ushahidi wa kuunga mkono
ushahidi wa mashahidi wa mjibu rufaa, kwani mashahidi waliokuja kutoa ushahidi
walidai kuwa walimsikia Lema katika mikutano ya kampeni akitoa maeno ya
kumdhalilisha na kumkashfu Dk.Batrida lakini mashahidi hao walishindwa kuleta
CD,mkanda wa video unaomuonyesha Lema akitoa matamshi yale.
“Tulimueleza jaji Rwakibarila kuwa
mashahidi wa wajibu rufaa hawaamini na kwamba ushahidi wao ulikuwa ni wa
mazingira lakini jaji katika hukumu yake hakuna sehemu alionyesha kukubali wala
kukataa hoja yetu hii’alidai wakili Kimomogoro.
Wakili huyo alidai pia jaji yule
alikosema alivyosema Lema ana bahati akukamatwa wala kushtakiwa kwa kitendo
chake cha kutoa lugha za kashfa na udhalilisha katika mikutano ya kampeni za
uchaguzi wa mwaka 2010 na kwamba mteja wake anaiomba mahakama rufaa itamke jaji
rwakibalila alitamka neno hilo kwa bahati mbaya na kutamka kwake
neno hilo ndiko kulikomsukuma kufikia uamuzi wa kumfungia Lema asigombee kwa
kipindi cha miaka mitano.
“Kwa hoja hizo tulizoziwasilisha hapo
juu, tunaiomba mahakama ya rufani nchini itengue hukumu ya Jaji Rwakibalila
kwani ni haina vigezo wala hadhi ya kuifanya iwe hukumu na pia wanaiomba
mahakama hiyo iwaamuru wajibu rufaa walipe gharama za uendeshaji wa kesi hiyo
tangu ilipoanza mahakama kuu kanda ya arusha na sasa mahakama ya Rufaa”alidai
wakili Kimomogoro.
Kwa upande wake wakili wa Mwanasheria
Mkuu wa serikali na Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Uchaguzi, Timon Vitalis,
yeye alidai sheria ya uchaguzi haiwaruhusu wapiga kura kufungua
kesi ya kupinga ubunge wala wagombea ubunge,udiwani kutukana majukwaani na
kwamba aliyepaswa kufungua kesi hiyo ya madai ya kukashfiwa ni Dk.Batrida na
siyo wajibu rufaa ambao ni wapiga kura wa jimbo la Arusha na kwamba kesi hiyo
ilikuwa njama za kisiasa ndani yake hali iliyosababisha watu kuangua vicheko
mara kwa mara wakati akitoa hoja zake wakili huyo Mwandamizi wa
serikali.
Akipangua hoja za mawakili hao wa
mwomba rufaa, mawakili wa wajibu rufaa Mugwai na Akida walidai
hukumu ile ni sahihi na haistahili kutenguliwa kwani imekidhi matakwa ya
kisheria na kuomba mahakama hiyo ya juu nchini itupilie mbali rufaa ya
Lema.
Wakili Mugwai alianza kwa kusema
mawakili wa mwomba rufaa wa wanaipotosha mahakama walivyosema kuwa hakukuwa na
uthibitisho wowote ulionyesha kuwa wajibu rufaa walikuwa ni wapiga kura wa jimbo
la arusha mjini wakati ukurasa wa 10 katika hukumu ile zilitolewa namba za
vitambulisho vya wapiga kura ambavyo ni vya wajibu rufaa na wakati vikitolewa
mahakamani siku hiyo mawakili hao wa mwomba rufaa walikuwepo.
Kuhusu hoja ya jaji alijielekeza
vibaya kusema kuwa sheria za uingereza hazitakiwi kutumika kuamua katika kesi za
uchaguzi, wakili Mugwai alidai jaji rwakibalila yupo sahihi katika hilo kwani
hata kifungu cha 1(2) cha sheria ya Uchaguzi sura ya 343 kinasema masuala yote
ya uchaguzi yatashughulikiwa kwa kutumia sheria ya uchaguzi na kuongeza kuwa
mawakili wa Lema wametumia kesi za mahakama ya rufaa zilizoamliwa kwa Sheria ya
zamani ya uchaguzi ya mwaka 1985 wakati sheria hiyo ya uchaguzi imeishafanyiwa
marekebisho na marekebisho ya mwisho hyalifanyika mwaka 2010 .
“Hata kifungu cha 2 (3)
cha sheria ya Judicuture and application of Law(JALA), inakataza matumuzi ya
sheria za nje kutumika kuamua kesi za uchaguzi wakati nchi yetu inayosheria ya
mahususi ya uchaguzi kwaajili ya kuamua kwaajili ya kuamua kesi za
uchaguzi na kwamba jaji alikuwa sahihi kusema hilo na pia jaji alikuwa sahihi
kusema wajibu rufaa walikuwa na haki ya kufungua kesi ile na kwamba hoja hiyo ni
butu”alidai wakili Mugwai.
Hata hivyo alipinga hoja ya mawakili
wa Lema iliyodai jaji yule katika hukumu yake hakutumia kesi walizoziwasilisha
mbele yake, ambapo alidai jaji yule katika hukumu yake alitumia baadhi ya kesi
walizoziwasilisha mbele yake na kwamba hata hivyo jaji ana mamlaka ya kuchuja
kesi anazotaka kuzitumia.
Kuhusu hoja ya kuwepo kwa ushahidi wa
kuunga mkono, wakili huyo alidai hoja hiyo haina mantiki kwani
aliyewaambia katika kesi ile ulikuwa ukiiitaji ushahidi wa kuunga mkono
nani kwani mashahidi wote 14 walifika mahakamani na kutoa ushahidi wao ambapo
kila shahidi alikuwa akitoa ushahidi unaounga mkono ushahidi wa mashahidi
wengine.
Akijibu hoja ya kwamba hukumu ile
iliegemea kwenye ushahidi wa mazingira tu, wakili Mugwai alikanusha hoja na
kusema hakukuwepo na ushahidi wa mazingira kwani mashahidi waliomsikia Lema
akitoa maneno yale ya kashfa kwenye mikutano ya adhara walifika mahakamani hapo
na kutoa ushahidi wao ambapo walisema walimwona Lema akitoa maneno yale ya
kashfa.
Hata hivyo wakati wakili Mugwai
akiwasilisha hoja zake kuba baadhi ya watu wanaodaiwa ni wafuasi wa CHADEMA
ambao walijazana ndani ya chumba cha mahakama walimfyonza na kuwa wakitoa
vicheko hali iliyosababisha wakili huyo kuwaeleza majaji wawathibiti watu wenye
tabia hiyo kwani mawakili wa Lema walipokuwa wakiwasilisha hoja zao walikuwa
awafyonzwi ila yeye anavyonza na kutaka wale ambao wanakerwa nay ale
anayoyawasilisha wavyumile hata hivyo majaji hawakuchukua hatua zozote kuhusu
ombi hilo.
Badaa ya mawakili hao kumaliza kuwasilisha
majumuisho yao katika rufaa hiyo Dar es Salaam jana saa tisa alasiri ambapo
rufaa hiyo ilianza kusikilizwa tangu saa tatu asubuhi ambayo ilikuja kwaajili ya
kusikilizwa ,majaji hao waliarisha shauri hilo na kusema tarehe ya kutolewa kwa
uamuzi wa rufaa hiyo itatolewa kwa njia ya maandishi.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Desemba 5 mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment