UPELELEZI KESI YA PAPA MSOFFE BADO
Na Happiness Katabazi
UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya mauaji inayomkabili
mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Marijani
Abdubakari Msoffe(50) maarufu kwa jina la “Papa Msoffe chuma cha reli akishiki
kutu’ ’ jana umeieleza tena Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa
upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Wakili Mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka mbaele ya Hakimu
Mkazi Agnes Mchome alianza kwa kuikumbusha mahakama kuwa upelelezi wa shauri
hilo bado haujakamilika na kwamba wanaomba tarehe ya kutajwa.
Hakimu Mchome alikubaliana na ombi hilo na akaiarisha kesi
hiyo hadi Januari 9 mwaka huu,itakapokuja kwaajili ya kutajwa na ninaamuru
mshtakiwa arejeshwe gerezani.
Agosti 10 mwaka huu, Msoffe ndiyo alifikishwa mahakamani
hapo kwa mara ya kwanza ambapo wakili wa Kweka alidai kuwa mshtakiwa huyo ana
kabiliwa na kosa la moja la kuua kwa kukusudia ambalo ni kinyume na kifungu
cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu
ya mwaka 2002. Kuwa Novemba 6 mwaka 2011 huko Magomeni Mapipa Papa Msoffe
anayetetewa na wakili wa kujitegemea Majura Magafu alimuua Onesphory Kituli.
Hata hivyo Hakimu Mchome alimtaka Msoffe asijibu chochote
kwasababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na kwamba ni
Mahakama Kuu ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Desemba 28 mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment