MAHAKAMA YA RUFAA YAKWAMISHA RUFAA YA ZOMBE
Na Happiness
Katabazi
MAHAKAMA ya
Rufaa nchini jana ilishindwa kuanza kusikiliza rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi
wa Mashtaka(DPP), Dk.Eliezer Feleshi dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa
Mkoa wa Dar es Salaam (ACP), Abdallah Zombe na wenzake kwa sababu jaji mmoja
Semistockles Kaijage anayeunda jopo la majaji watatu anaumwa.
Rufaa hiyo
ambayo ilikuja kwa ajili ya kuanza kusikilizwa chini ya jopo la majaji wa tatu
wanaongozwa na Jaji Natalia Kimaro anayesaidiwa na Catherine Oriyo Semistocles
Kaijage .
Upande wa
mwomba rufaa(DPP), unawakilishwa na jopo la mawakili waandamizi wa serikali
saba ambao ni Mgaya Mtaki, Timon Vitalis,Edward Kakolaki, Angaza Mwipopo,
Prudence Rwenyongeza ,Alexanda Mzikila
na Peter Njike .
Wakati
mawakili wajibu rufaa ambapo Zombe anatetewa na wakili maarufu nchini Richard
Rweyongeza na washtakiwa wengine wanatetewa na mawakili Majura Magafu, Denis
Msafiri, Deodoras Ishengoma ambao walisema wapo tayari kwaajili ya usikilizwaji
wa rufaa hiyo.
Jaji Kimaro
akiarisha rufaa hiyo alisema mwana jopo mmoja (Kaijage) ni mgonjwa hivyo rufaa
hiyo haitaweza kusikilizwa jana na kwamba anaiarisha hadi pale pande hizo mbili
zitakapojulishwa kwa maandishi na uongozi wa mahakama tarehe nyingine ya kuja
kuisikiliza.
Agosti
17 mwaka 2008, Mahakama Kuu Kanda ya Dar
es Salaam, ilitoa hukumu ya kihistoria ya kesi ya mauji ya watu wanne iliyokuwa
ikimkabili Zombe na wenzake ambapo jaji Salum Massati ambaye hivi sasa ni jaji
wa mahakama ya rufani aliwaachilia huru Zombe na wenzake ambao walikuwa
wakikabiliwa na kesi hiyo kwa maelezo kuwa upande wa jamhuri ulishindwa kuleta
ushahidi mzuri ambao ungewea kuishawishi mahakama hiyo iwaone washtakiwa hao
wana hatia.
Baada ya
hukumu hiyo ya mahakama kuu, DPP hakulidhishwa na hukumu hiyo akaamua kukata
rufaa mahakama ya rufaa kupinga hukumu hiyo Septemba mwaka 2008 kupinga hukumu
hiyo ambayo kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya mahakama ya rufaa,rufaa hiyo
ilikuwa imepangwa kuanza kusikilizwa jana lakini ikashindikana.
Mbali na Zombe, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Christopher Bageni, Ahmed Makele, WP 4593 PC Jane Andrew, D 1406 Koplo Emmanuel Mabula, D 8289 DC Michael Shonza, D. 2300 Abeneth Saro, D.4656D/Koplo Rajabu Bakari na D.1317D/XP Festus Gwasabi na jana washtakiwa wote walifika mahakamani hapo.
Washitakiwa hao walidaiwa kuwa Januari 14, mwaka 2006 waliwaua wafanyabiashara watatu wa madini wa wilayani Ulanga, mkoani Morogoro; Ephraim Chigumbi, Sabinus Chigumbi na Mathias Lukombe pamoja na dereva teski Juma Ndugu, mkazi wa Dar es Salaam kwa madai kuwa walikuwa majambazi.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Desemba 12 mwaka 2012
No comments:
Post a Comment