Header Ads

TAHADHARI YA BABU WA LOLIONDO


Na Happiness Katabazi
JUMATATU wiki hii gazeti moja siyo Tanzania Daima, lilimnukuu aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa la Kiinjiili la Kilutheli nchini(KKKT), Ambilikile Mwasapile akisema kuwa wananchi wajiandae kupokea muujuzi mpya kutoka kwake.


Mwasapile kwa jina maarufu ‘Babu wa Loliondo’ pamoja na kutoa ahadi hiyo pia aliwashutumu baadhi ya viongozi wa makanisa na waganga wa kienyeji ambao wamekuwa wakikimbiwa na wateja wao kuwa ndiyo wamekuwa wakimchafulia jina lake.

Sote tungali tukikumbuka kuwa mapema mwaka huu maelfu ya watanzania na raia wa kigeni waliliminika katika makazi ya babu huyo kule Kijijini Samunge mkoani Arusha kwaajili ya kupatiwa tiba ya magonjwa sugu iliyokuwa ikitolewa kwa gharama ya Sh 500/- na babu huyo ambapo babu huyo aliwaaminisha wagonjwa hao kuwa dawa yake inawaponya wagonjwa waliokuwa na imani na haitawaponya wagonjwa ambao hawatakuwa na imani.

Binafsi sina taaluma ya kitabib, mahabara wala siyo mtumishi wa dini hivyo ndiyo maana sitaki kukubali kwamba dawa ya babu huyo kuwa haikuwaponya au imewaponya wagonjwa waliokunywa dawa yake ‘Kikombe cha Babu’ kwasababu kati ya watu watano ambao ninawafahamu na waliniaga wakati wanakwenda kunywa dawa kwa babu huyo, hadi leo wameshindwa kunieleza wamerudi mahabara na kupimwa na kukutwa maradhi yaliyokuwa yakiwasumbua yametoweka.

Vyovyote iwavyo, Mtazamo wangu wa leo si kutaka kupingana na ahadi ya babu aliyoitoa mapema wiki hii kuwa wananchi wajiandae kupata muujiza mpya kutoka kwake, la hasha mibinafsi baada ya kusikia ahadi hiyo ya Babu wa Loliondo nimebaki kujiuliza je muujiza huo unaotarajiwa kutolewa na babu huyo, Je muujiza huo utolewa kwa njia ya dawa ya mitishamba ambayo itawalazimu wahusika kuitumia kwanjia ya kuinywa?
Basi kama muujiza unaotarajiwa kutolewa na Babu wa Mwasapile atautoa kwa njia hiyo ya dawa, tafadhali sana kabla ujaanza kutoa dawa hiyo nakuomba uwaite faragha watafiti watatifi wa madawa toka taasisi za serikali ili uwaeleze ili waweze kuifanyia utatifi kwanza kabla ya wewe kuanza kutoa huduma hiyo kwa wananchi.

Kwani tungali tukikumbuka kuwa dawa yako ya awali”kikombe cha babu’ ulianza kuwapatia wagonjwa na wakanywa kabla haijafanyiwa utaifiti na wataalamu wa Taasisi ya Utafiti NIMR na Taasisi cha ya Chakulia na Dawa, wagonjwa walipojitokeza kwa wingi ndipo serikali kupitia taasisi hizo nazo zikafunga safari na kwenda kuchukua sampo za dawa ya babu huyo na kwenda kuifanyia utafiti kama inafaha kwa matumuzi ya binadamu.

Itakumbukwa kuwa mengi yamesemwa kuhusu dawa hiyo ya babu kuwa dawa hiyo haitibu na imesababisha wagonjwa wengi kupoteza maisha yao, binafsi sina ushahidi na hilo.

Ila angalizo langu kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuwa nayo imeshamsikia babu wa Loliondo akijinasbu kuwa anatarajia kutoa muujiza mwingine, ni vyema basi ikawatuma kimya kimya maofisa wake kwenda kuzungumza na babu huyo ili awaeleze mapema ni muujiza wa aina gani anatarajia kuutoa na utawalenga wananchi wa makundi gani.

Ili serikali iweze kujipanga sasa kuweza kutoa msaada wake pindi itakapoitajika kutoa msaada pindi muujiza huo utakapoanza kutolewa kwani ikumbukwe kuwa muujiza huo unahusu maisha ya watanzania na Kikatiba kila Mtanzania ana haki ya kuishi na kila mwananchi ana haki ya kulindwa.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
0716 774494
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Oktoba 18 mwaka 2011.

6 comments:

joema said...

kweli kabisa umenena dada
watu wengi sana wamekufa kwa kuacha kutumia dawa za hospital na kunywa kikombe cha babu.
na kama hizo dawa ni za ukweli mbona ilE misururu ya magari na watu waliokuwa wanaenda kupata kikombe wako wapi?
je ni kweli wagonjwa wameisha ?jibu hapana ni vile wamegundua ni utapeli tu hatuna haja ya kuficha vitu vya wazi tena serikali ingekuwa makini ilitakiwa kumchukulia hatua ni vile serekeli yenyewe imejaa ushirikina ndio maana ata viongozi wa ngazi za juu na usomi wao wote wameenda kunywa mimaji yanayoambiwa ni dawa wajinga ndio waliwao.
mimi sijasoma sana lakini bila ata kwenda shule darasa moja tumia tu akili za kuzaliwa hivi ni dawa gani ((tena namnukuu amesema ameoteshwa na mungu )))iwe na mashart KIBAO utafikiri ramri ya waganga wa kienyeji ,et kikombe lazima yeye tu achote dawa na kuwawekea wengine na hairuhusiwi kumchukulia mtu ebu fikiria hilo! si utapeli jamani ? hivi kwanini watu wanakuwa waoga kudiscuss uozo wa hizo dawa na maisha ya watu waliopotea wengine wakiachwa polini maiti zao kama wanyama kwa nini tunaogopa kuliongelea hilo au ni vile wengi mmekunywa dawa hivyo mnaona aibu kwakweli mimi binafsi inanikera sana, ndio leo nafungua blog yako nilipopeluzi habari za babu nikajisikia kukereka na kuumia sana kwani kuna ninaowajua wamekufa mara baada ya kwenda kwa babu sababu kubwa sio babu ni ile hali ya kudanganyana kuwa anatibu mtu anatumia muda mwingi njiani barabara mbaya chakula hakuna na huduma muhimu hakuna then mauti yanatokea kwa kweli TUSILEANE KWA UOZO inaboa KUONA KILA MTU ANAOGOPA KUONGELEA HILI WOTE WANAKAA KIMYA AU KUONGEA KIMYAKIMYA.

Anonymous said...

If you are going for finest contents like myself, only pay
a visit this web site all the time as it presents quality contents,
thanks

Also visit my website ... diet plan for women

Anonymous said...

Good info. Lucky me I discovered your blog by accident
(stumbleupon). I have bookmarked it for later!

my site ... http://www.egoldbars.com (sgzuidwest.nl)

Anonymous said...

Can I simply say what a comfort to uncover a person that genuinely knows what they are discussing on the
net. You actually realize how to bring an
issue to light and make it important. More
people have to read this and understand this side of the story.
It's surprising you are not more popular because you certainly have the gift.

Here is my blog post; Author's external home page.
..

Anonymous said...

This article gives clear idea in support of the new viewers of
blogging, that in fact how to do blogging and site-building.


Also visit my weblog Learn Additional Here

Anonymous said...

Howdy, I think your web site might be having browser compatibility problems.
Whenever I take a look at your blog in Safari, it looks fine however,
when opening in Internet Explorer, it's got some overlapping issues. I just wanted to provide you with a quick heads up! Apart from that, great blog!

Look into my webpage Stock market

Powered by Blogger.