KESI YA IDD SIMBA,NTAGAZWA ZA AIRISHWA
Na Happiness Katabazi
KESI ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kulisababishia Shirika la Usafirishaji UDA, hasara ya Shilingi bilioni 2.3 inayomkabili Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Idd Simba jana ilitajwa mbeled Hakimu Mkazi Faisa Kahamba na kuiarishwa.
Hakimu Kahamba alisema kesi hiyo iliyokuja kwaajili ya kutajwa na anaiarisha hadi Julai 19 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kupangiwa tarehe ya usikilizwaji wa awali.
Mbali na Simba ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wazee wa Dar es Salaam, washitakiwa wengine ni Mkurugenzi Salim Mwaking’inda na Meneja Mkuu wa shirika hilo Victor Milanzi ambao wanatetewa na wakili wa kujitegemea Alex Mgongolwa na Said El Mamli na upande wa Jamhuri unawakilishwa na wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Ben Lincoln.
Wakati huo huo kesi ya kujipatia kofia,fulana zenye jumla ya shilingi milioni 74.9 kwa njia ya udanganyifu inayomkabili aliyekuwa waziri wa zamani Arcado Arcado Ntagazwa(65) na wenzake imeairishwa mahakamani hapo hadi Julai 25 mwaka huu. Na kwamba mahakama hiyo imekubali ombi la upande wa Jamhuri la kuongezewa siku 60 kwaajili ya kuendelea kufanya uchunguzi wa kesi hiyo. Washitakiwa wengine ni Senetor Mirelya (60) na Webhale Ntagazwa wanaotetewa na Alex Mgongolwa.
Aprili 23 mwaka huu, wakili wa serikali Ladslaus Komanya mbele ya Hakimu Mkazi Liad Shamshama alidai kuwa Oktoba 22 mwaka 2009 huko Msasani Mikoroshini washtakiwa hao kwania ovu walijipatia fulana 5000 na kofia 5000 zenye jumla ya thamani ya Shilingi milioni 74.9 toka kwa Noel Sevele kwa makubaliano kuwa wangemlipa Sevele kiasi hicho cha fedha katika kipindi cha mwezi mmoja tangu walipochukua vifaa hivyo lakini hata hivyo walishindwa kumlipa.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Juni 29 mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment