Header Ads

KAJALA ATIWA HATIANI,WEMA SEPETU AMLIPITIA FAINI YA SH.MIL 13




Na Happiness Katabazi

HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imewahukumu kwenda jela miaka nane au kulipa faini ya Sh.milioni 13 msainii wa Filamu nchini, baada ya kumtia hatiani katika makosa ya kula njama kuamisha umiliki wa nyumba, na kuamisha umiliki wa nyumba iliyokuwa iliyokuwa imezuiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali isiuzwe.

Hukumu hiyo iliyolewa jana na Hakimu Mkazi Sundi Fimbo ambapo alianza kwa kuikumbusha mahakama hiyo kuwa Kajala na Faraja Chambo walikuwa wakikabiliwa na makosa matatu yaliyofunguliwa mapema mwaka jana mahakamani hapo..

Makosa hayo ni kosa la kwanza ni   la kula njama kinyume na kifungu cha 34 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007, ambako washitakiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo la kula njama la kuhamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi, Salasala eneo ambalo halijapimwa jijini Dar es Salaam.

Shitaka la pili ni kwamba, Aprili 14 mwaka 2010 walihamisha isivyo halali umiliki wa nyumba hiyo, ambayo walikuwa wakiimiliki kwenda kwa Emilian Rugalia, ambaye ndiye walimuuzia kinyume na kifungu cha 34(2)A(3), cha Sheria ya TAKUKURU ya mwaka 2007, na shitaka la tatu ni la kutakatisha fedha, ambalo walilitenda siku hiyo ya Aprili 14 mwaka 2010, huku wakijiua ni kinyume cha sheria hiyo.

Hakimu Fimbo alisema baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili, alisema upande wa Jamhuri umeweza kuithibitisha kesi hiyo na hivyo mahakama hiyo imemtia hatiani Kajala katika kosa la kwanza na la pili tu wakati Chambo amepatikana na hatia katika makosa yote matatu.

Alisema katika kosa la kwanza Kajala na Chambo watatakiwa walipe faini ya Sh.milioni tano kila mmoja au kwenda jela miaka mitatu. Kosa la pili watatakiwa walipe faini ya Sh.milioni nane  aukwenda jela miaka mitano kwa kila mmoja.

Aidha katika kosa la tatu ambayo ni Chambo ndiyo amekutwa na hatia  atatakiwa alipe faini ya Sh.milioni 200 au kwenda jela miaka mitano na kwamba adhabu hizo hazitakwenda pamoja.Hivyo Kajala peke yake  amehukumiwa kwenda jela jumla ya miaka nane  au kulipa jumla ya Sh.milioni 13 .

“Mahakama imewakutana na hatia washitakiwa wote  katika kosa la pili kwasababu ushahidi umethibitisha kuwa washitakiwa wote  walikuwa wakifahamu kuwa kuwaliwa na hati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliyokuwa imezuia nyumba yao waziize kwasababu Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa ilikuwa ikidai kuwa nyumba hiyo imepatikana kwa njia ya utakatishaji fedha,lakini wao wakakaidi amri hiyo wakaamua kuiuza”alisema Hakimu Fimbo.

Akilichambua kosa la kwanza, alisema pia upande wa jamhuri umeweza kulithibitisha  kwasababu kosa la pili limeweza kuthibitishwa .

Kuhusu shitaka la tatu, hakimu huyo alisema amemwachilia huru Kajala kwasababu upande wa jamhuri umeshindwa kuthitisha Kajala alishiriki vipi katika upatikanaji wa fedha haramu  kwasababu ilidaiwa kuwa Chambo alizipata fedha haramu katika maelezo ya onyo  kuwa alizipata fedha za kujengea nyumba hiyo wakati akiwa mfanyakazi wa Benki ya NBC.

‘Na kwa mujibu wa maelezo ya onyo ya Chambo ambaye ni mume wa Kajala, alikiri  kuwa wakati akiwa mfanyakazi wa benki ya NBC alikuwa akichukua fedha na kuzituma kwa baadhi ya watu wa ofisi ya TTCL ,watu ambao hawakuwa wakistahili kulipwa na baada ya vyombo vya dola kuanza kumfuatulia akaamua kuizua nyumba yake hiyo”alisema hakimu Fimbo.

Hata hivyo baada ya hukumu kutolewa wasanii wa filamu nchini walikuwa wamefika mahakamani hapo kufuatilia hukumu ya kesi hiyo, walikusanyika katika viunga vya mahakama hiyo na kuanza kujadiliana ili wachangishane fedha lakini msanii Wema Sepetu aliwataka wenzake wasichanganishane fedha ,badala yake yeye analipa Sh.milioni 13 na akaondoka katika eneo hilo na kisha kurejea mahakamani hapo saa saba mchana na kulipa faini hiyo na kisha kuondika na Kajala ,wakati Chambo akirudishwa gerezani kwani alishindwa kulipa fidia hiyo na pia anakabiliwa na kesi nyingine ya utakatishaji fedha mahakamani hapo.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Machi 26 mwaka 2013.

2 comments:

Anonymous said...

Asante Happy kwa simulizi/uandishi ulionyooka, hata mie ambae kidogo sikuwepo mahakamani na sikujua alishtakiwa kwa nini sasa nimeelewa..
Pamoja

Anonymous said...

Kazi nzuri, ila uwe unafanya proof reading kabla ya ku-publish,..
otherwise kila kitu kilo sawa

Powered by Blogger.