Header Ads

WASHITAKIWA KESI YA PONDA WAZIDI KUKANA MAELEZO WALIYOYATOA POLISI


Na  Happiness Katabazi

WASHITAKIWA nane wa kesi ya uchochezi na wizi wa malighafi za sh.milioni 59 inayomkabili Sheikh Ponda Issa Ponda jana wameendelea kujitetea na kuyakana maelezo waliyoyatoa polisi wakati walipokamatwa.

Mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa  washitakiwa hao ambao ni mshitakiwa 22,23,24,25,27,26,29 jana ambao walikuwa wakiongozwa na wakili wao Juma Nassor kutoa utetezi wao walidai kuwa wao hawakuwahi kuchukuliwa maelezo polisi na kwamba polisi walichofanya nikuwauliza majina yao tu.

Wakitoa utetezi wao walidai kuwa wao Oktoba 16 mwaka jana, walikuwa msikiti wa Shule ya Changombe Markas  kwaajili ya kuudhurulia ibada ya Itikafu ambapo walidai taarifa za kufanyika kwa ibada hiyo walizipata kupitia misikiti mbalimbali.

Hata hivyo wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka baada ya kusikiliza utetezi wa washitakiwa hao, alikuwa akiwauliza washitakiwa hao kama wana maradhi yoyote au wanaugonjwa wa kusahau ambapo washitakiwa hao wote walidai hawana tatizo lolote.

‘Hivi nyie mashahidi wote leo hii mnadai kuwa kabla ya kufikishwa mahakamani hapa Oktoba 18 mwaka jana, hakumchukuliwa maelezo polisi, hapa mahakamani kuna maelezo ya onyo ambayo mliyatoa polisi Kijitonyama wakati mkihojiwa na maelezo haya yanataja maelezo yenu binafsi, kazi zenu:

“Na washitakiwa wengine katika hizi nakala za maelezo yenu mlikiri kukamatwa katika eneo la Chang’ombe Markas  ambapo mlikuwa mkijenga msikiti wa muda , na mlikuwa na vifaa vya ujenzi kwaajili ya kujengea msikiti huo ambao mlieleza kabisa mlifikia uamuzi wa kuweka kambi katika eneo hilo kwasababu mlipata taarifa kuwa kiwanja hicho mali ya waislamu kilikuwa kimeibwa na hivyo mliamasishwa kwenda kukikomboa kiwanja hicho”alidai shahidi wa 34, Salima Abdukadirfu.Kesi hiyo inaendelea tena leo.

Wakili Kweka aliwahoji washitakiwa hao kuwa inakuwaje sasa polisi ambaye alikutana na washitakiwa kwa mara ya kwanza siku hiyo wakati wakiwahoji, kisha mapolisi hao waweze kufahamu hata maelezo binafsi ya washitakiwa hao ambapo washitakiwa hao walikuwa wakikubali majina yao  na saini yaliyokuwa yameanishwa kwenye maelezo hayo ya onyo lakini wakakanusha maelezo ya kina yaliyokuwa yameandikwa katika nakala hiyo ya maelezo ya onyo ambayo waliyayotoa polisi na yameifadhiwa mahakamani hapo kama vilelelezo.

Hata hivyo washitakiwa hao walishindwa kujibu maswali hayo ya wakili Kweka na kuishia kudai kuwa hawafahamu polisi hao wameyapata wapo maelezo yao binafsi

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Machi 12 mwaka 2013.

1 comment:

Anonymous said...

One thousand Online Payday Loan Loans-Get Online Payday Loan proper Into
Your Topper AR financeStamp Recipients: win over food Stamps To Online payday loan A
Growing security departmentStalked By 450-Year-Old debt Payday Advance Today Is Payday streamdistaff
Prison ship's officer 33 Who fell In dearest With Drugsundefendable Flipping: tender Your website And Get agile Results CanObama Online Payday Loan MADE comfortable Duff Mckagan - Maybe The Coolest
my website > payday loan

Powered by Blogger.