HUKUMU YA RUFAA YA WAFUASI WA PONDA YAWEKWA KIPORO
Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam,
jana ilishindwa kutoa hukumu ya rufaa iliyokatwa na wafuasi 52 wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za
Kiislamu ,Sheikh Issa Ponda Issa, ambapo Machi 21 mwaka huu, Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, iliwahukumu adhabu ya kifungo cha mwaka
mmoja jela, wameiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kwa maelezo kuwa
bado haijaiandaa hukumu hiyo.
Jaji Salvatory Bongole alisema ni
kweli rufaa hiyo ilikuja jana kwaajili ya yeye kuitolea hukumu lakini
ameshindwa kutoa hukumu hiyo kwasababu tangu Septemba 2 hadi Oktoba 4 mwaka
huu, anasikiliza vikao vya kesi ya mauji hivyo ameshindwa kuandaa hukumu hiyo
na badala yake anaiarisha kesi hiyo hadi Oktoba 21 mwaka huu ambapo siku hiyo
atakuja kuitolea hukumu na akaamuru waomba rufaa warejeshwe gerezani.
Agosti 12 mwaka huu, rufaa hiyo
ilianza kusikilizwa rasmi na jaji huyo ambapo wakili wa waomba rufaa Mohammed Tibanyendera aliomba ,mahakama hiyo iwachilie huru Salum
Bakari Makame na wenzake 51 na itengue hukumu iliyotolewa na Hakimu Mkazi wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Sundi Fimbo baada ya kuwakuta na hatia ya
makosa ya matatu ya kula njama,kufanya mkusanyiko haramu na kukaidi amri ya jeshi la polisi iliyowataka wasiaandamane kwenda ofisini kwa
Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), Dk.Eliezer Feleshi kushinikiza ampatie dhamana
Ponda ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya wizi wa malighafi zenye thamani ya
Sh.milioni 59 ambaye alihukumu kifungo cha mwaka mmoja jela.
Tibanyendela alidai kuhusu kosa la
kwanza la kula njama kwa mujibu wa rekodi ya hukumu, ile hakuna ushahidi
unaonyesha washitakiwa walikutana mahali kokote kupanga njama ya kutenda kosa
hilo lakini wanashangazwa na Hakimu Fimbo kuwatia hatiani kwa kosa hilo kwa
shahidi kwanza hadi wa 10 ambao ni maofisa wa polisi walieleza mahakama kuwa
waliwakamata washitakiwa hao katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam
Februali 15 mwaka huu.
Wakili Tibanyendera alikilichambua
kosa la kula njama kutenda kosa kinyume na kifungu 384 cha Sheria ya Kanuni ya
Adhabu ya mwaka 2002, kosa la pili ni la kufanya mkusanyiko haramu kinyume na
kifungu cha 74 na 75 cha sheria hiyo ambavyo vinasomwa pamoja na kifungu
cha 43(2)(4) na 46 cha Sheria ya Jeshi la Polisi ya mwaka 2002.
‘Kwa masikitiko makubwa tu
nasema kosa la kula njama halikuthibitika, na hakimu Fimbo alikosea
kuwatia hatiani kwa kosa la kula njama kwa kutumia kifungu hicho cha 384 cha
sheria ya Kanuni ya adhabu. Na kwa mujibu wa kifungu cha 46 cha Sheria ya Jeshi
la Polisi ya mwaka 2002,inasema wazi kabisa mtu anayekutwa a hatia ya kutenda
kosa la mkusanyiko haramu atapaswa alipe faini ya Sh.50,000 au kwenda jela
miezi mitatu au vyote pamoja:
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Septemba 21 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment