RUFAA YA DPP,MAHALU HAKIELEWEKI
Na Happiness
Katabazi
MAHAKAMA Kuu
Kanda ya Dar es Salaam, jana ilijikuta ikishindwa kaanza kusikilia rufaa
iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), Dk.Eliezer Feleshi dhidi ya
aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia na Grace Martin kwa sababu mwenendo wa kesi hiyo iliyokuwa
ikiendeshwa awali katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu haujawekwa kwenye
jarada la rufaa ambalo linaanza kutumiwa na Mahakama Kuu kuendeshea rufaa hiyo.
Jaji John
Utamwa alisema kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya kaunza kusikilizwa lakini kwa
bahati mbaya jarada la rufaa hiyo ndani yake haina rekodi ya kesi ya uhujumu
uchumi iliyokuwa ikiwawakabili wajibu rufaa yaani (Mahalu na Grace), ambao
Agosti 9
mwaka jana walishinda kesi hiyo ya uhujumu
uchumi na wizi wa Euro zaidi ya milioni mbili.
Alisema
sababu ya pili mawakili wa wajibu rufaa, Mabere Marando na Alex Mgongolwa
wanaudhuru hivyo anaiarisha rufaa hiyo hadi Novemba 11 mwaka huu, itakapokuja
kwaajili ya kusikilizwa.
Agosti 9
mwaka huu, Hakimu mkuu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu , Ilvin
Mugeta aliwaachilia huru Mahalu na Grace Martin kwa maelezo kuwa upande wa
jamhuri umeshindwakuthibitisha kesi yao.Na muda mfupi baada ya hukumu hiyo
kutolewa DPP hakulidhishwa na hukumu hiyo akakata rufaa Mahakama Kuu kupinga
hukumu hiyo.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Septemba 3 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment