UB ILIVYOJITOA KUWAFUNDA WATETEZI HAKI ZA BINADAMU
Na Happiness Katabazi
NENO ‘watetezi wa haki
za binadamu’ bila shaka siyo neno geni kwa masikioni mwa watu. Neno hilo
limekuwepo kwasababu linatumiwa na watu wanaojitambulisha kuwa wao ni watetezi
wa haki za binadamu ndani na nje ya Tanzania.
Kwa upande fulani
watetezi hao wa haki za binadamu wamekuwa wakifanyakazi nzuri ya kuwaelekeza wananchi
wasiyojua haki zao jinsi ya kuzidai kwa kufuata utaratibu na mwisho wa siku
wanancho hao wanaozingatia ushauri wa watetezi hao wa haki za binadamu wamekuwa
wakifanikiwa.
Lakini kwa upande
mwingine kuna makundi ya watu wanaojitambulisha kuwa ni watetezi wa haki za
binadamu kwanza hawana hata elimu ya kujua haki za binadamu ni zipi, zinadaiwa
kwa njia zipi na wengine wamekuwa wakijifanya watetezi wa haki za binadamu
kumbe wanatumia ngao hiyo kujificha kumbe ni wanachama wa vyama vya siasa na
wakati wakiamasisha watu kudai haki zao wamekuwa wakipenyeza ajenda zao za
kiitikadi jambo ambalo siyo sahii.
Hili kuondokana na wimbi
la wanaharakati ucharwa ambao kadri siku zinavyozidi kusonga mbele hapa nchini
linazidi kushamili,na ambapo kama wimbi hilo halitadhibitiwa Tanzania inaweza
kujikuta inaingia kwenye machafuko kwa kisingizio cha baadhi ya wanaharakati
wasiyo na elimu za ki uhanarakati kila kukicha kutoa matamko katika jamii
ambayo wakati mwingine matamko hayo yanapotosha jamii na kuleta mivutano baina
ya wananchi na serikali, Chuo Kikuu cha
Bagamoyo Dar es Salaam (UB), kinachoongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Profesa
Costa Ricky Mahalu kwa kushirikiana na Taasisi isiyoyakiserikali ya nchini
Kenya , Akiba Uhaki imezindua mafunzo ya kuwanoa wale wote wanaojiita
wanaharakati na wale wanye ndoto ya kuwa wanaharakati yatakayo chukua miezi
sita chuoni hapo kwaajili ya kuwafundisha watetezi hao wa haki za binadamu
kwanza kuzifahamu haki hizo za binadamu ni zipi, zinadaiwaje, na kisha waende
kwenye jamii kuielimisha jamii jinsi ya kuzidai haki hizo kwa njia ya amani na
utulivu na siyo maandamano yasiyo na vibali wala ghasia.
Tumeshuhudia baadhi ya
watu wanaojiita wanaharakati wakiwachochea wananchi kudai haki kile wanachoona
ni haki yao kwa kuamua kupambana na vyombo vya dola na mwisho wa siku wananchi
hao wanajikuta wakiambulia kupata madhara ya kupata vigipo au kufikishwa
mahakamani kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya maandamano haramu,kuzuia polisi
wasifanyekazi yao na kufanya mikusanyiko haramu.Na wananchi hao wakipata
madhara hayo,wale watu watu wanaojiita ni wanaharakati ambao walikuwa wakiwatuma
kufanya hivyo, wao ukaa pembeni.
Mbali na maelezo ,
mwandishi wa makala hii anasimulia hotuba zilizotolewa katika uzinduzi wa program
ya Akiba Uhaki inayotolewa na Chuo Kikuu cha Bagamoyo kwaajili ya kuwaonea
watetezi wa haki za binadamu siku ya uzinduzi wa program hiyo uliofanyika
Jumatatu usiku katika chuo hicho kilichopo Kawe Beach Dar es Salaam , ambapo
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mercy Sila alitoa hotuba yake kwaniaba ya Mkuu wa
Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza.
Sila alisema serikali inakipongeza
Chuo Kikuu cha Bagamoyo(UB), kwa
uamuzi wake wa kuanzisha kozi ya kuwanoa watu wanaojitambulisha kuwa wao
ni watetezi wa haki za binadamu katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
kwasababu kozi hiyo itasaidia watetezi wa haki za binadamu kufahamu
wanachokifanya katika jamii na kwamba kozi hiyo inakuwa ni ya kwanza kutolewa
hapa nchini.
Sila alisema program
hiyo inaendeshwa na Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) na kufadhiliwa taasisi ya
kiraia ya Haki Uhaki yenye makao makuu yake nchini Kenya, tayari
imeishapata wanafunzi kumi toka nchi za
Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda, Burundi na kwamba masomo hayo yatakuwa
yakitolewa kwa miezi sita na kuwataka wale wote wanaojiita wanaharakati hapa
nchini wafike katika chuo hicho ili waweze kufundishwa kwanza jinsi ya kufahamu
haki za binadamu ni zipi ,na haki za kijamii ni zipi na hao wanadamu wanatakiwa
wazitii sheria za nchi wakati wakizidai hizo haki zao bila shuruti.
“Tumeona katika mataifa
ya wenzetu vurugu kila kukicha na hata hapa nchini kuna baadhi ya watu
wanaojiita ni watetezi wa haki za binadamu na wamekuwa wakitumia kinga hiyo
kupotosha ukweli wa mambo ambayo yanafanywa na serikali zao kwa kisingizio kuwa
wa ni watetezi wa haki za binadamu wakati hata elimu ya kutetea hizo haki za
binadamu hawana …leo serikali inapenda kupongeza program hii kwani itasaidia
sana kuondoa mivutano na malumbano baina ya watetezi wa haki za binadamu na
serikali kwani mtu atakayepata elimu hii atakuwa ameelimika na kufahamu
haki za binadamu zinapaswa zidaiwe kwa kutumia amani”alisema Sila.
Kwa upande wake Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Profesa Costa Ricky Mahalu aliishukuru
serikali kwa kukubali kuja kuzindua program hiyo kwani programu ni yakwanza
kutolewa katika vyuo vya hapa nchini na program hiyo itawezesha kuondoa
malumbano baina ya serikali na watetezi wa haki za binadamu kwani ni wazi hivi
sasa kumeibuka watu wanaojitambulisha kuwa ni watetezi wa haki za binadamu
wakati hawana hata elimu ya huo utetezi wa haki za binadamu na wamekuwa wakitoa
baadhi ya matamko ambayo hayana mantiki katika suala zima la utetezi wa
haki za binadamu hali ambayo alisema ikiachwa iendelee italeta madhara katika
jamii.
“UB inaamini katika
elimu zaidi…hivyo UB imeona ni jambo jema kuanzisha program hiyo ya mafunzo ya
muda mfupi kwa wale wote wanaotaka na wanajiita watetezi wa haki za binadamu
waje kufundishwa masuala hayo na waadhiri waliobobea katika eneo hilo la
masuala ya haki za binadamu”alisema Profesa Mahalu.
Kwa upande wake Mkuu wa
Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Bagamoyo Dk.Natujwa Mvungi ambayo
program hiyo ya Akiba uhaki inatolewa chini ya kitivo chake alisema
jumla ya wanafunzi 10 toka katika nchi tano za jumuiya ya Afrika
Mashariki wa kozi ya Akiba Uhaki ,wameishafika hapa nchini na wanaanza
mafunzo hayo kwa muda wa miezi sita kuanzia wiki hii chuo hapo na kwamba
wanafunzi hao wamefadhiliwa ada ya kusoma kozi hiyo na taasisi isiyo ya kiserikali
yenye makao makuu yake nchini Kenya ya Akiba uhaki na kuwataka wale wote
wanaojiita ni watetezi wa haki za binadamu wakati hawana elimu ya
kuonyesha wamefudhu kozi hiyo,wasisite kuja kupata elimu hiyo chuo hapo.
Aidha Mratibu
wa Programu hiyo toka Taasisi ya Akiba Uhaki ya nchini Kenya, Kempta Ombati
alishukuru chuo cha UB, kukubali kushirikiano nao kutoa mafunzo hayo ambayo
yasaidia nchi za Afrika Mashariki kuondokana na watu wanaojiita kuwa ni
wanaharakati wakati hawana elimu ya kuzijua haki wanazozitetea na wajibu na
kwamba taasisi yake ndiyo imetoa ufadhili kwa wanafunzi hao kumi wanaotoka nchi
zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuja kuudhulia kozi hiyo katika chuo
Kikuu cha Bagamoyo na kwamba mafunzo hayo ni ya kwanza kutolewa katika vyuo vya
hapa nchini na kwamba taasisi yao itaendelea kutoa ufadhili.
0716 774494
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili , Septemba 22 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment