Header Ads

DAUD BALALI ATAJWA KESI YA MRAMBA
Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imeelezwa kuwa aliyemwalika na kuiongezea mkataba wa kufanyakazi ya ukaguzi wa madini nchini Kampuni ya Alex Stewart ni serikali yenye kupitia aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu marehemu Daudi Balali na siyo aliyekuwa waziri wa Fedha Basil Mramba wala waziri wa Nishati na Madini , Daniel Yona .

Mramba ,Yona, na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Gragy Mgonja wanakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh.bilioni 11.7 kutokana na kampuni ya Alex sterwart kupewa msamaha wa kodi na Mramba bila ridhaa ya mamlaka ya mapato TRA ambapo kesi hiyo inasikilizwa na jopo la majaji John Utamwa, Sam Rumanyika na Hakimu Mkazi Saul Kinemela ambapo jana shahidi anayemtea Mramba alipanda kizimbani na kutoa utetezi wake.

Shahidi huyo ambaye ni Crecencia Mbatia(61) ambaye alikuwa na wadhifa wa Mkurugenzi wa Soko la Fedha wa Benki Kuu  na ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Timu ya watu wa tano ya majadiliano ya jinsi ya kupata kampuni ya Alex sterwart na wenzake na kuandaa mkataba wa baina ya BoT na kampuni hiyo.

Mbatia alidai kuwa hivi sasa ni mstaafu lakini mwaka 2002 akiwa na wadhifa huo aliongoza timu hiyo ya majadiliano vizuri na kwamba kamati ilifanyakazi ya kumtafuta mkaguzi wa madini kupitia Internate na kwamba  wakati wanatafuta kampuni hizo walizipata jumla ya kampuni 21 lakini kamati yake ilichagua kampuni tano  na na serikali kupitia BOT ikazindikia barua za mialiko hizo kampuni tano ilizije kwenye majadiliano lakini ni kampuni mbili tu ndiyo ziliijibu hizo barua za serikali ikiwemo kampuni ya Alex Stewart na baada ya mchakato kampuni ya Alex Stewart ndiyo ikakubaliwa kujana nchini kufanyakazi hiyo.

Mbatia ambaye alikuwa akiongozwa na wakili wa kujitegemea Herbbet Nyange kutoa ushahidi wake alidai kuwa katika kipindi chote cha kamati ya awali aliyokuwa akiingoza ikiwa inafanyakazi zake , hapakuwepo m,wakilishi toka wizara ya Fedha isipokuwa alikuwa akiwaona wanasheria toka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali ambao walikuwa wakishiriki katika vikao vya timu hiyo ya majadiliano.

‘Hata hivyo timu yangu haikuweza kufanya majadiliano na kampuni ya Alex Stewart kwasababu mwakili wa kampuni hiyo alivyofika katika timu yangu alisema haoni haja ya kufanya majadiliano kuhusu bei na gharama za uendeshaji na timu hiyo kwani tayari gavana Balali kwaniaba ya BOT na serikali nzima ilikuwa tayari imeishamtumia barua ya mwaliko ikionyesha jinsi atakavyofanyakazi na gharama za uendeshaji”alieleza Mbatia.

Akijibu maswali aliyokuwa akiulizwa na wakili wa Yona, Elisa Msuya, shahidi huyo huku shahidi huyo akisoma kielezo cha 11  ambacho kielelezo hicho ni barua ya BoT kwenda kwa Kampuni hiyo ambapo Gavana Balali anaiandikia barua kampuni hiyo ya kuiarifu kuwa imeiongezea tena mkataba wa miaka miwili  ambaye jana alimaliza kuongozwa kutoa ushahidi wake na upande wa utetezi.

Hata hivyo upande wa jamhuri unaongozwa na wakili mwandishi wa serikali Oswald Tibabyekomya, Shadrack Kimaro uliomba mahakama iarishe kwa muda kesi hiyo ili waweze kwenda kujiandaa na maswali ya kumuuliza shahidi huyo.

Jaji Utamwa aliarisha kesi hiyo hadi leo ambapo shahidi huyo atakuja kuhojiwa na upande wa jamhuri.

Novemba 2008 ilidaiwa mahakamani hapo na mawakili wa upande wa jamhuri kuwa washitakiwa hao wanakabiliwa na makosa ya matumuzi mabaya ya madaraka na kuisasababishia serikali hasara ya Sh.bilioni 11.7.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano,Septemba 19 mwaka 2013.

No comments:

Powered by Blogger.