Header Ads

HUKUMU 'KESI YA SAMAKI WA MAGUFULI' LEO

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo inatarajiwa kutoa hukumu dhidi ya raia wa tano wa wa China wanaokabiliwa na kesi ya uvuvi haramu katika ukanda wa Tanzania kwa kutumia meli ya Tawariq 1 maarufu kama ‘Kesi ya Samaki wa Magufuli’.


Washtakiwa hao Hsu Chin Tai, Zhao Hanguing, Hsu Shang Pao, Ca’ Dong Li na Chen Rui Hai wanatetewa na mawakili wa kujitegemea Ibrahim Bendera na John Mapinduzi.

Hukumu hiyo inayotarajiwa kusomwa na Jaji Agustine Mwarija leo kufuatia washtakiwa hao kumaliza kujitetea Novemba 21 mwaka huu, ikiwa siku chache baada ya mahakama hiyo kuwaona washtakiwa hao watano wanakesi ya kujibu na kuwaachilia huru washtakiwa 31 kwasababu mahakama iliona hawana kesi ya kujibu.

Machi 2009 washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kisha kesi hiyo ikahamishiwa Mahakama Kuu wakikabiliwa na makosa ya kuvua samaki bila leseni, kuharibu mazingira katika kina kirefu cha ukanda wa Bahari ya Hindi eneo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Februali 23 mwaka 2012.

No comments:

Powered by Blogger.