Header Ads

MWENENDO KESI YA MRAMBA TAYARI

Na Happiness Katabazi

HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, umesema kuwa mwenendo wa kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 11.7 inayomkabili aliyekuwa waziri wa fedha Basil Mramba na wenzake, umekamilika.

Hayo yalisemwa jana na Jaji John Utamwa aliyekuwa anasaidiwa na mahakimu wakazi Saul Kinemela na Sam Rumanyika wakati kesi hiyo ilipokuja kwaajili ya kutajwa na kuangalia mwenendo wa kesi hiyo kama umekamilika.

Jaji Utamwa alisema hatimaye mwenendo wa kesi hiyo umekamilika na kwamba anatoa siku saba kwa mahakama hiyo ziwe zimeishazipatia pande mbili katika kesi hiyo mwenendo huo wa kesi ambao umechukua muda mrefu kuandaliwa.

Jaji Utamwa alisema upande wa utetezi utapaswa uwasilishe majumuisho yao ya kuwaona wanakesi ya kujibu au la Machi 27, nao upande wa jamhuri uwasilishe majumuisho yao kwa njia ua maandishi Aprili 17 na endapo upande wa utetezi unataka kuwasilisha majumuisho ya nyongeza uwasilishe Aprili 30.

Aidha alisema kesi hiyo itakuja kwaajili ya kutajwa Machi 26 na kwamba Mei 2 itakuja kwaajili ya jopo hilo kuangalia kama hizo amri za mahakama zimetekelezwa.

Januari mwaka jana upande wa Jamhuri katika kesi hiyo unawakilishwa na upande Naibu Mkuruegenzi wa Mashtaka Stanslaus Boniface na Shadrack Kimaro ulifunga ushahidi wake na hivyo kesi hiyo kwa kipindi chote hicho hadi jana kesi hiyo ilikuwa inakuja kutajwa mahakamani kwasababu mwenendo wa kesi hiyo ulikuwa bado haujakamilika kuandaliwa.

Mbali na Mramba washtakiwa wengine ni aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona na Katibu Mkuu Mstaafi wa wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonjwa ambao wanakabiliwa na makosa ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali harasa ya shilingi bilioni 11.7.

Katika hatua nyingine upande wa Jamhuri katika kesi ya kukutwa na simu gerezani inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu, Amatus Liyumba ulishindwa kumsomea maelezo ya awali mshtakiwa huyo kwasababu wakili wa mshtakiwa huyo Majura Magafu hakuwepo mahakamani na hivyo Hakimu Mkazi Stewart Sanga akaiairisha kesi hiyo hadi Machi 15 mwaka huu.

Chanzo:Gazeti la Tanzania la Jumamosi, Februali 18 mwaka 2012

No comments:

Powered by Blogger.