Header Ads

VIONGOZI WA AINA HAWAFAI




Na Happiness Katabazi

HAPA nchini hivi sasa kwa kasi ya aina yake umezuka mtindo unaofanywa na baadhi ya viongozi wa makanisa ya kuwaalika baadhi ya wanasiasa kuudhulia katika makanisa hayo kwaajili ya kuongoza shughuli za harambee.

Na katika harambee hizo tumeshuhudia baadhi ya wanasiasa hao wanaoarikwa kuongoza harambee hizo au kuudhulia misa mbalimbali, ugeuza harambee hizo kuwa majukwaa ya kuwapiga vijembe wanasiasa wenzao ambao wanahasimiana kisiasa na wengine wemekuwa wakiwaita wanaisasa wenzao ambao nao wamekuwa wakienda makanisani humo kuwa ni mafisadi ambao wamekuwa wakitumia makanisa hayo kujisafisha katika tuhuma hizo za ufisadi zinazowakabili.

Binafsi sipingi viongozi hao wa makanisa kuwaalika wanasiasa kwenda kuongoza shughuli mbalimbali makanisani na sipingi wanasiasa kwenda kuudhulia harambee hizo.

Licha tayari kuna taarifa zisizopendeza ambazo bado hazijathibitishwa kuwa kuna baadhi ya viongozi wa dini kwa tamaa ya fedha na wengine tayari wameishakuwa kwenye kambi za wanaotajwa kuwania rais mwaka 2015 wamekuwa wakimwalika mwanasiasa mwenye nguvu ya fedha ambaye wanaamini wakimwita kwenye harambee zao atawachangishia fedha nyingi na hivyo harambee yao itakuwa imefana kwani watakusanya fedha nyingi.

Na hivyo wale wanasiasa ambao hawana nguvu ya kifedha wamekuwa hawapewi kipaumbele cha kualikwa na viongozi hao wa makanisa.

Kumekuwepo na taarifa kuwa nao hao wanasiasa wamekuwa wakifanya ushawishi kwa njia wanazozijua ili waweze kualikwa kwenye makanisa ambayo yanawafuasi wengi ili waweze kuudhulia kwenye ibada na baada ya ibada kumalizika, viongozi wa makanisa uwapa fursa ya kuhutubia na hapo ndiyo wanasiasa hao hawa ambao wanatufanya sisi waumini ni majuha tusiojua wanachikitafuta huko makanisani ni nini ,upata fursa ya kuwarushia makombora ya maneno ya shombo mahasimu wao wa kisiasa kwa kuwaita ni mafisadi hawafai kuwa viongozi.

Kwa kweli hali hii inasikitisha na kutisha kwani unapoona taifa lina viongozi wa kisiasa hasa wale wa chama tawala (CCM), wamekuwa vinara wa kucheza mchezo huo hatari wa kwenda kufanya ghiliba za wazi makanisani, ni hatari sana na hali hii isipotokomezwa ni wazi ipo siku Mungu atachoka kuona waumini wake wanafanyiwa ghiliba na usanii na wanasiasa hawa makanisani na hivyo ataamua kuwaadhibu wanasiasa hao na makuwadi wao, na wasije kulia na mtu.

Yaani tumefika mahali pabaya sana kama nchi hivi sasa, zile tabia zetu za kihuni, ujanja ujanja,usanii na utapeli na uongo tulizokuwa tunazifanyia nje ya nyumba za ibada hivi sasa shetani ametutawala mioyoni mwetu atuziogopi tena nyumba hizo za ibada , tumevaa ujasiri na kuamua kuziingiza tabia hizo za kishetani ndani ya nyumba za ibada tena bila wasiwasi .

Kwanza minashangaa sana ni kwanini hawa wanaotajwa na wapambe wao kuwa watagombea urais katika uchaguzi mkuu ujao,mbona wameanza vurugu za kampeni mapema kiasi hiki tena kwa njia ya kujitafutia lana kwa mwenyezi mungu kwani wanaanza kampeni zao kwa kutumia makanisa?

Hivi urais wa Tanzania umekuwa ni rahisi rahisi kiasi hiki?

Baadhi ya wapambe wa hao wanaotajwa kutaka kugombea urais wamekuwa wakinieleza kuwa wanachelewa kulala kwasababu mara kwa mara wamekuwa wakikutana kwenye vikao vyao vya siri kwaajili ya kuimarisha kambi zao na kupanga mikakati ya kuwadhoofisha maadui wa kambi yao kwa njia tofauti ikiwemo njia ya kuwaibulia tuhuma kupitia vyombo vya habari.

Ieleweke wazi mchezo huu ni hatari kwa umoja wa taifa letu kwani utaanza kuleta matabaka ya kidini.

Binafsi napingana na hao wanasiasa ambao wamekuwa wakialikwa na makanisa hayo kwenye shughuli hizo halafu wakifika kwenye shughuli hizo wanaanza kurusha vijembe kwa mahasimu wao kisiasa licha hawawataji majina lakini mtu mwenye akili timamu na anafuatilia vijembe hivyo,utabaini wazi mwanasiasa huyu anampiga kijembe mwanasiasa fulani ambaye hayupo kwenye kundi lake linalomuunga mkono katika harakati zake za kusaka ukubwa.

Hivi kanisani si ni mahali pakuongelea mambo ya mungu,kutubu kama ulivyafanya mambo mabaya ili usamehewe na kumshukuru mungu kwa baraka na hiyo ndiyo hasa maana ya ibada.

Leo hii wanasiasa wetu hao ambao kwa mujibu wa watu wao wa karibu na wapo wanatueleza kuwa vinara hao na wapambe wao ambao wanapishana kwenye makanisa tofauti kuwa wameanza kampeni za kusaka urais wa mwaka 2015,wawapo kwenye ibada hizo wanatoa hotuba za kuwapiga vijembe mahasimu wenzao wa kisiasa hali inayofanya tujiulize kama kweli tunaamini kanisani ni mahali ambapo watu wanaenda kumshukuru mungu,kutubu na kumsifu mungu, ,sasa hizo dondo za kisasa zinazotolewa na wanasiasa hao zinaingiaje?

Kama Yesu alivyosema kuwa ya Kaisali mpe Kaisali na ya Mungu mpe Mungu.Ufisadi na mbio hizo za urais mnaziingizaje makanisani? Yaani ni sawa na mdudu kaingiaje kwenye kokwa la embe?

Biblia inasema Mtu hataishi kwa mkate tu ila neno la mungu. Lakini pia tunatambua mwanadamu hawezi kuishi kwa neno la mungu tu na ndiyo maana tunatafuta na kisha tunatoa sadaka na dhaka kwenye nyumba zetu za ibada.

Kwa hiyo mkate tunaoupata sisi binadamu baada ya kuutafuta, uutoa kwenye nyumba zetu za ibada kwa njia ya sadaka na dhaka na hiyo ni sehemu pia ya ibada ya kufanya nyumba zetu za ibada ambazo uendeshwa kwa neno la mungu au Mtume Mohamad kwa njia ya ibada.

Kwa hiyo hata watumishi wa mungu wanaopokea sadaka hizo zile zinazotolewa kiwango kikubwa cha waumini wao hasa hao wanasiasa zinatoka katika mapato halali ya waumini wao wanaozileta makanisani na hizo harambee.

Kama watumishi hao wa mungu watasisitiza kupokea mapato tuu,basi mwisho wa siku makanisa yatajikuta yakipokea sadaka ambazo zimepatikana kwa njia ya kihalifu.

Mtu maisha yake yote kasoma kamaliza ,akaajiliwa kuwa mtumishi wa umma,akaacha kazi hiyo akajiunga kwenye medani ya siasa kama Mbunge,waziri,mjumbe wa NEC.Kote huku mapato yake yanajulikana.

Ghafla mtu wa aina hiyo anajifanya (raimu sana)yaani mtu mwema anaibukia katika makanisa tofauti anachangia mamilioni ya shilingi,mapato ambayo yakikusanywa yanazidi kipato chake kinachotambulika na mamlaka ya vyombo husika.

Ni lazima sasa tujiulize hiyo ziada imetoka wapi? Na hoji hilo kwa sababu tusije tukafika mahali wahalifu wakafadhili shughuli za kijamii kwa mbwembwe na wakaheshimika na wale na watu wenye maadili na wasiyo na uwezo wa kifedha wakaonekana ni watu wa ovyo kwa kuwa tu hawana fedha za ziada ya kutoa kwenye harambee makanisani.

Maana siku zote mtu ambaye hana fedha yaani maskini anaonekanaga ni mtu asiye na akili kabisa kwasasa kila jambo analotaka kufanya hawezi kulifanya kwasababu ya kukosa fedha ya kulifanya na mwishowe anaishia kuonekana hana akili.

Nafikiri taasisi zetu za dini zijiulize thamani ya makanisa yao,baadhi ya waumini wao na wasiyowa waumini wao kuwachangia mapesa mengi bila taasisi hizo kujiuliza mapato halali ya ziada ya hao wanaoongoza harambee makanisani ambazo taarifa zinadai ,hiyo ni mbinu moja wapo wa kujisafishia njia ya kuwania urais mwaka 2015.

Ieleweke kuwa makanisa na misikiti yanapaswa yapokee mapato halali siyo haramu.Makanisa kukubali kupokea mapato kutoka kwa ambao ikaja kubainika ni mapato haramu ,makanisa yatakuwa nayo yameshiriki kwa njia moja au nyingine kutenda uhalifu huo(accomplice).

Aidha vyombo vyetu vya dola ambavyo vinaendeshwa kwa gharama kubwa na kodi za wananchi kufanyakazi zake ili pia viweze kuwachunguza watu wenye mapato ya ziada,hadi wananchi wanashtukia. Je havilijui hili? Na kama imelijua hilo,vimechukua hatua gani?

Mungu ibariki Tanzania, mungu Ibariki Tanzania

0716 774494

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Februali 8 mwaka 2012

1 comment:

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Dada umepigilia msumari kwenye kichwa cha nyoka. Hakuna maudhi ninayopata kusikia utumbo na upupu wa wachunaji wanaojiita wachungaji kama Antony Lusekelo ambaye hana tofauti na changudoa linapokuja suala la kuchumia tumbo. Bado hawasikii wanajikomba wakati rais aliishawashushua kuwa wengi ni wauza unga. Hebu uliza huo utajiri wa kuendesha migari ya bei mbaya na kuvaa suti na dhahabu wameupata wapi kama siyo majambazi waliojificha kwenye majoho?

Powered by Blogger.