LWAKATARE NJE KWA DHAMANA
Na Happiness
Katabazi
HATIMAYE Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, jana imempatia dhamana Mkurugenzi wa Ulinzi na
Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare na
mwenzake Joseph Ludovick wanaokabiliwa na kosa moja la kula njama utaka
kumdhuru kwa sumu Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Denis Msacky.
Hakimu Mkazi wa
Mahakama Alocye Katemana alitoa uamuzi
wa kumpatia dhamana Lwakatare na wenzake
jana saa mbili asubuhi ambapo
alisema jana kesi hiyo ilikuja kwaajili ya yeye kutolea uamuzi maombi ya
dhamana na mapingamizi ya dhamana yaliyowasilishwa mahakamani hapo Mei 13 mwaka
huu, na wakili wa washitakiwa hao Peter Kibatara na wakili wa jamhuri Prudence
Rweyongeza na Ponsia Lukosi ambapo mawakili wa jamhuri waliomba mahakama
isimpatie dhamana.
Hakimu Katemana
alisema amefikia uamuzi wa kukubalina na mawakili wa washitakiwa walioomba
mahakama iwapatie dhamana kwasababu ina mamlaka ya kufanya hivyo na kwamb anatupilia
mbali ombi la mawakili wa upande wa jamhuri uliotaka mahakama isiwape dhamana
kwasababu pingamizi hilo la upande wa jamhuri halina msingi wowote kisheria.
“Ili mshitakiwa
apate dhamana ni lazima awe na wadhamini wawili wanaotoka taasisi
zinazotambulika kisheria ambapo kila
kila mdhamini atatakiwa asaini bondi y ash.milioni 10 pamoja na washitakiwa
wenyewe,washtakiwa hao kusamilisha hati zao za kusafiria mahakamani na
kutotoka nje ya jiji la Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha
mahakama’alisema Hakimu Katemana.
Baada ya kumaliza
kusoma masharti hayo ya dhamana, Hakimu Katemana aliiahirisha kesi hiyo
hadi nyakati za saa 8:00 mchana, kwa ajili ya kuwapa nafasi upande wa mashtaka
ili kuweza kuhakiki barua zilizowasilishwa na wadhamini kama zilikuwa ni halali
kisheria au la.
Wakati upande
wa mashtaka ukienda kuhakiki barua hizo, washtakiwa hao walipelekwa
rumande kwa ajili ya kusubiri kusaini hati za dhamana ili kuweza kuachiwa
huru ama la.
Ilipofika saa nane mchana, washitakiwa hao waliingizwa kwenye chumba cha mahakama ambapo Hakimu Katemana aliaki nyaraka hizo za masharti ya dhamana na upande wa jamhuri ulikuwa hauna pingamizi, na akaamua kumpatia dhamana Lwakatare kwasababu alitimiza masharti hayo ya dhamana na alimyima dhamana Ludovick kwasababu alishindwa kutumiza masharti hayo na akaamuru Ludovick apelekwe rumande na kisha kuiarisha kesi hiyo hadi Juni 24 mwaka huu, kesi hiyo hadi Juni 24 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa.
Mei 13 mwaka huu, kesi ya msingi ya
Lwakatare ilivyokuja katika Mahakama ya Kisutu kwaajili ya kutajwa, hakimu
Alocye Katemana anayesikiliza kesi hiyo hakuwepo na mawakili wa Lwakatare Peter
Kibatara aliwasilisha ombi la kuomba mteja wake apatiwe dhamana kwasababu kosa
la kwanza la kula njama lilobaki linadhamana kwa mujibu wa sheria lakini hata
hivyo wakili wa Serikali Prudence Rweyongeza alililipinga ombi hilo kwa
madai kuwa shauri hilo lipo hatua za uchunguzi kilichopo mahakamani hapo ni jalada la tuhuma zinazowakabili
washitakiwa ambazo zipo katika hatua za uchunguzi na kwamba tuhuma hizo mwisho
wa siku zitakufunguliwa kesi rasmi Mahakama Kuu kwani Mahakama Kuu ndiyo yenye
mamlaka ya kuisikiliza hivyo huwezi mahakama haiwezi kutoa dhamana kwa kesi
ambayo haipo(Pending Trial) .
“Na kwa mazingira ya shauri linalomkabili Lwakatare hapa
Mahakama ya Kisutu,lipo katika hatua za uchunguzi na bado DPP hajafungua
kesi rasmi Mahakama Kuu, sasa tunashangaa mawakili wa washitakiwa wanawasilisha
ombi la dhamana leo hii katika mahakama hii wakati maamuzi hayo ya mahakama ya
Rufaa yapo na bado hajatenguliwa?
Rweyongeza aliomba mahakama hiyo itupilie mbali maombi ya
mawakili wa utetezi kwasababu hakuna kesi rasmi iliyofunguliwa na DPP mahakama
Kuu dhidi ya washitakiwa na kwamba shauri lililopo katika mahakama ya Kisutu
lipo katika hatua za uchunguzi.
Mei 8 mwaka huu,Jaji Lawrence Kaduri
wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,
alitoa uamuzi wa kumfutia jumla ya makosa matatu ya ugaidi baada ya kuona hati ya
mshitaka haijitoshelezi kumfungulia mashitaka hayo na hivyo kumbakizia kosa
hilo moja la kula njama na kuamuru kesi hiyo irudishwe katika mahakama ya
Kisutu kwaajili ya hatua zaidi.
Mei 21 mwaka huu, Mkurugenzi wa
Mashitaka(DPP), Dk.Eliezer Feleshi aliwasilisha ombi Mahakama ya Rufaa nchini,
linaomba mahakama hiyo iitishe mwenendo wa uamuzi huo wa mahakama kuu ambao
ulimfutia Lwakatare mashitaka hayo matatu na pia uutengue , na hadi sasa
mahakama ya rufaa bado haijapanga tarehe wala majina ya majaji wa kaunza
kusikiliza ombi hilo la DPP.
Machi 20
mwaka huu, Lwakatare na wenzake walifunguliwa rasmi kesi Na.6/2013 ya
tuhuma za ugaidi ambapo kosa la pili, tatu, na la nne yalikuwa hayana dhamana
na hivyo Mei 8 mwaka huu, Jaji Kaduri aliyafuta makosa hayo kwa maelezo kuwa
hajaona kama kuna maelezo ya kutosha ya kuwafungulia mashitaka ya aina hiyo
washitakiwa hao.
No comments:
Post a Comment