MWAKALEBELA AIBWAGA TENA TAKUKURU KORTINI
Na Happiness
Katabazi
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Iringa imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imekatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa dhidi ya aliyekuwa mgombea ubunge wa Iringa Mjini(CCM), Fredrick Mwakalebe na mkewe Celina iliyokuwa ikipinga uamuzi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa ambayo ilifuta kesi hiyo hiyo ya madai ya kushawishi na kutoa ruhwa kwa sababu hati ya mashitaka ilikuwa na mapungufu.
Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Mkuya ambaye alisema rufaa hiyo iliwasilishwa mahakamani hapo na PCCB na wakili wa Mwakalebela, Alex Mgongolwa aliwasilisha pingamizi la awali ambalo liliomba mahakama hiyo iifute rufaa hiyo kwasababu hati hiyo ya rufaa ilikuwa haijaambatishwa na nakala ya uamuzi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa ambayo iliwafutia kesi hiyo wajibu rufaa kwa sababu hati ya mashitaka ilikuwa na dosari.
Mwakalebela ambaye aliwai kuwa kiongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, mwaka 2010 aligombea ubunge wa kwa tiketi ya CCM katika kura za maoni ambapo Kada mwenzie wa chama hicho Monica Mbeya alimshinda katika kura za maoni na Mbega akawa amechaguliwa kupeperusha bendera ya CCM jimboni hapo lakini hata hivyo Mbega alishindwa na jimbo hilo likachukuliwa na mbunge Peter Msigwa wa chama cha Chadema.
Ilipofika mwaka 2011, Takukuru ilimfungulia kesi hiyo ya jinai yeye na mkewe ya madai ya kutoa na kushawishi rushwa kwa wapiga kura katika kampeni za kusaka ubunge wa jimbo hilo.
Chanzo:Gazeti la
Tanzania Daima la Alhamisi, Mei 30 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment