Header Ads

TISA WANG'ANG'ANIWA NA MAHAKAMA WIZI FEDHA ZA POLISI

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam ,imewaachiria huru  wawili katika kesi ya wizi  Sh 330,000,000 mali ya Jeshi la Polisi baada ya kuwaona hawana kesi ya kujibu lakini imewataka washitakiwa tisa wapande kizimbani wajitete baada ya kuwaona wana kesi ya kujibu.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Jenevitus Dudu ambaye alisema kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa mbele yake na  mashahidi  21 wa upande wa jamhuri ambao walikuwa wakiwalishwa na wakili wa serikali Lasdilaus Komanya na Lugua.

Hakimu Dudu alisema baada ya kupitia ushahidi huo na hoja za mawakili wa upande wa jamhuri waliomba mahakama iwaone wanakesi ya kujibu washitakiwa wote wakati mawakili wa kujitegemea Alex Mushumbusi na Karegero Karegero na Ambokile Mwakaje amefikia uamuzi wa kumwachiria huru mshitakiwa sita Fortunatus Boniface Biseko    na wanane   Deogratias Fidelis Lumato ambaye anatetewa na wakili Mushumbusi kuwa hawana kesi ya kujibu kwasababu.


Hakimu Dudu alisema washitakiwa ambao wamepatikana na kesi ya kujibu ni Vedastus Limbu Mafuru,
Kennedy Agumba Achayo
,Adelaida Lwekoramu,
Luciana Vedastus Limbu,
Agnes Robert Maro,
Mkika Gideon Nyasebwa na.Edna Kadogo   Amos Kabisi Hangaya,
Joshua Aseno Onditi,
  na kwamba wataanza kujitetea mfululizo kuanzia Juni 24 hadi 28 mwaka huu.

Mwaka 2010 ilidaiwa na upande wa jamhuri kuwa washitakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ya Na. 40/2010 kuwa wanakabiliwa na kosa la kula njama, kughushi na wizi  wa kiasi hicho cha fedha   kwenye akaunti inayoitwa Police Retention Collection Account No. 2011000015 kwenye benki ya NMB Meatu.
  
Washtakiwa baadhi yao walikuwa wafanyakazi wa NMB Meatu Tawi la Mwanhuzi na wengine walikuw wafanyabiashara.

Chanzo:www.katabazihappy.blogspot.com, Juni 12 mwaka 2013.


No comments:

Powered by Blogger.