MAHAKAMA YA RUFAA YATENGUA HUKUMU YAKE
Na Happiness Katabazi
HATIMAYE jopo la majaji watano wa Mahakama ya Rufaa nchini limetungua hukumu
iliyotolewa na jopo la majaji watatu wa mahakama mwaka 2011 ambayo ilikuwa ikimtaka mtu yoyote anayepinga
ubunge wa mbunge aliyepo madarakani kuwasilisha kwanza mahakamani ombi la
kuomba mahakama impangie kiwango cha kulipa dhamana ya kufungua kesi za
uchaguzi ngazi ya ubunge.
Uamuzi huo wa ambao imeandika historia mpya katika tasnia ya
sheria ya nchini, ulitolewa jana mchana na jopo la majaji watano wa Mahakama ya
Rufaa Dar es Salaam, Januaria Msofe, William Mandia, Salum Massati, Angela
Kileo, Nataria Kimaro ambao walisema wamekubaliana na hoja za wakili wa
kujitegemea Herbet Nyange ambaye aliomba
mahakama itoe tafsiri ya kifungu cha 111 cha Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010,
kinachomtaka anayefungua kesi ya uchaguzi ya kupinga matokeo ya ubunge, kwanza
alazimike kuwasilisha ombi mahakamani la kuomba mahakama impangie kiasi cha
kulipa dhamana kabla ya kesi ya msingi kuanza kusikilizwa.
Jaji Msofe alisema jopo lake lilisikiliza hoja za wakili
Nyange kuhusu kuomba tafsiri ya kifungu hicho na kuipitia hukumu iliyotolewa
mwaka 2011 na jopo la majaji watatu wa mahakama hii, alisema wamekubaliana na
hoja wakili Nyange ya kwamba ni kweli uamuzi wa rufaa ile ya jopo la majaji wa
tatu ulikuwa na makosa.
“Kwa sababu hiyo jopo hili la majaji watano leo linatangaza
kuwa limetengua uamuzi wa majaji wenzetu wa tatu ambayo ulikuwa unamtaka mtu
yoyote anayewasilisha ombi la kupinga ubunge wa mbunge kuwasilisha kwanza ombi
la kuomba pangiwe kiwango cha kulipa dhamana ya kuendesha kesi yake ya kupinga
ubunge;
“Hivyo jopo letu linatamka kuwa kuanzia sasa mtu yoyote
anayeta kufungua kesi ya kupinga ubunge hatalazimika tena kuanza kuwasilisha
ombi mahakamani la kuomba apangiwe kiasi cha kulipa hivyo badala yake jopo hili
linatoa ruhusa kwa mtu mwenye uwezo wa kifedha wa kulipa dhamana ya kufungua
kesi ya kupinga kesi afungue kesi ya kupinga ushindi wa ubunge moja kwa moja na
kwa yule mtu ambaye hana huwezo wa kifedha wa kuweka dhamana ya fedha mahakamani
kama anavyoakiwa na sheria ya uchaguzi kulipa kwanza Sh.milioni tano, basi mtu
huyo awasilishe ombi mahakamani la kuomba apunguziwe kiasi hicho cha fedha
kwaajili ya dhamana ya kesi”alisema Jaji Msofe.
Aidha jaji huyo alisema baada ya mahakama yake kutoa uamuzi
huo jana , mahakama yake imesema itaanza kusikiliza rufaa iliyokatwa na Chiriko
dhidi ya Lugora katika tarehe ambayo itakuwa imepangwa na uongozi wa mahakama
ya rufaa.
Wakili Nyange ambaye
anamtetea mwomba rufaa katika rufaa ya ubunge wa jimbo la Mwibara, Chiriko Haruni Davidi wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) dhidi
ya Mbunge wa Mwibara Bunda, Mkoani Mara, Kangi Lugora, wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), ambapo Chiriko anapinga ubunge wa Lugora anatetewa na wakili Melkizedeck Lutema na Mwanasheria Mkuu wa Serikali anayetetewa
na wakili wa serikali Wakili wa Serikali
Mkuu, Obadia Kameya akimwakilisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali alioupata mwaka 2010 kuwa ushindi wake
ulikuwa umekiuka sheria ya uchaguzi.
Wakati Chiriko akikata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa
na jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo katika rufaa ya kesi ya uchaguzi iliyokuwa imefunguliwa
na Katani A. Katani (Chadema) dhidi ya
Mbunge wa jimbo la (Tandahimba), Juma Njwayo ya mwaka 2011. Naye Lugora alikata rufaa mahakamani hapo akipinga hukumu hiyo iliyompa ushindi.
Lugola katika rufaa yake , pamoja na mambo mengine, anadai
kuwa mlalamikaji katika kesi ya msingi, Chiriko alilipa gharama za kufungua
kesi hiyo bila kuiomba Mahakama impangie kiwango alichopaswa kutoa, kinyume cha
kifungu hicho cha 111 cha Sheria ya Uchaguzi.
Wakili wa Lugora, Lutema akiongezea nguvu hoja yake alirejea
uamuzi wa Mahakama ya Rufani katika
rufaa ya Katani A. Katani wa Chadema, dhidi ya Mbunge wa Tandahimba, Juma
Njwayo ya mwaka 2011.
Ambapo kwa mujibu wa uamuzi wa jopo la majaji watatu wa
mahakama hiyo katika kesi hiyo iliyotolewa uamuzi wake mwaka 2011, walitupilia mbali rufaa hiyo ya Katani
kutokana na mlalamikaji kuwasilisha dhamana ya kesi bila kuomba mahakama
impangie kiwango, kinyume cha kifungu hicho cha 111cha Sheria ya Uchaguzi.
Mei 17 mwaka huu, wakili wa Chiriko, Nyange, alidai kuwa
uamuzi wa rufaa ya Katani haukuwa sahihi na kwamba mahakama haikutafsiri vizuri
kifungu hicho.
Wakili Nyange alidai
kuwa uamuzi huo unakiuka marekebisho ya mwaka 2002 ya Sheria ya Uchaguzi ya
mwaka 1985, na kwamba unabadili msimamo wa mahakama hiyo ambao umekuwepo tangu
mwaka 2006, bila kuubainisha msimamo huo wa mahakama hiyo.
Chanzo:Gazeti la Gazeti la Tanzania Daima
la Jumamosi, Juni Mosi mwaka 2013.
1 comment:
At the same time brewer provides you with unique features attractive believe accomplish the
coffee enjoyment each time. The patient with good feeling sick, vomiting is as well
get injured through the process of coffee bean can also be happier drinking lemon juice and green tea.
All your little associates 're remarkably super understanding of sickly variations inside air flow for that reason even the tiniest differ through the temperatures ph amount will definitely extremely impact on that in the hazardous method as well as, it's wise that you don't placement whatever thing citrus to that were designed to simply turn citrus from the composting not unlike milk products, peelings range acid vegetables as with lemons so a melon. Should selected the many plunger and as a result screen method may be out of an media before you carry out. These types imagination might a fact before you style your espresso coffee by using the Gaggia Improvement Espresso Machine.
Here is my blog post: mr coffee 12 cup programmable coffeemaker
Post a Comment