LWAKATARE KUPEWA,KUNYIMWA DHAMANA LEO?
Na Happiness
Katabazi
MAHAKAMA ya
Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,leo inatarajia kutoa uamuzi wa kumpa au
kumnyima dhamana Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama cha Demokrasia na
Maendeleo(Chadema), Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph wanaokabiliwa na kosa
moja la kula njama kutaka kumuua kwa sumu Mhariri Mtendaji wa gazeti la
Mwananchi, Denis Msack.
Hayo
yamesemwa jana na Hakimu Mkazi Alocye Katemana muda mfupi baada ya wakili
mwandamizi wa serikali Ponsian Lukosi kuikumbusha mahakama kuwa kesi hiyo jana
ilikuwa imekuja kwaaajili ya kutajwa.
Hakimu
Katemana alisema anaiarisha kesi hiyo hadi leo ilikuja kuja kutoa uamuzi wa
maombi ya dhamana yaliyowasilishwa na mawakili wa Lwakatare, Peter Kibabatara
na Abdalah Safari Mei 13 mwaka mbele ya
Hakimu Mkazi Sundi Fimbo, wakati yeye alipokuwa likizo na mawakili wa upande wa
jamhuri walipinga washitakiwa hao wasipewe dhamana.
Mei 13 mwaka huu, kesi ya msingi ya
Lwakatare ilivyokuja katika Mahakama ya Kisutu kwaajili ya kutajwa, hakimu
Alocye Katemana anayesikiliza kesi hiyo hakuwepo na mawakili wa Lwakatare Peter
Kibatara aliwasilisha ombi la kuomba mteja wake apatiwe dhamana kwasababu kosa
la kwanza la kula njama lilobaki linadhamana kwa mujibu wa sheria lakini hata
hivyo wakili wa Serikali Prudence Rweyongeza alililipinga ombi hilo kwa madai kuwa shauri
hilo lipo hatua za uchunguzi kilichopo
mahakamani hapo ni jalada la tuhuma zinazowakabili washitakiwa ambazo zipo
katika hatua za uchunguzi na kwamba tuhuma hizo mwisho wa siku zitakufunguliwa
kesi rasmi Mahakama Kuu kwani Mahakama Kuu ndiyo yenye mamlaka ya kuisikiliza
hivyo huwezi mahakama haiwezi kutoa dhamana kwa kesi ambayo haipo(Pending
Trial) .
“Na kwa mazingira ya shauri linalomkabili Lwakatare hapa
Mahakama ya Kisutu,lipo katika hatua za uchunguzi na bado DPP hajafungua
kesi rasmi Mahakama Kuu, sasa tunashangaa mawakili wa washitakiwa wanawasilisha
ombi la dhamana leo hii katika mahakama hii wakati maamuzi hayo ya mahakama ya
Rufaa yapo na bado hajatenguliwa?
Rweyongeza aliomba mahakama hiyo itupilie mbali maombi ya
mawakili wa utetezi kwasababu hakuna kesi rasmi iliyofunguliwa na DPP mahakama
Kuu dhidi ya washitakiwa na kwamba shauri lililopo katika mahakama ya Kisutu
lipo katika hatua za uchunguzi.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Juni 11 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment