Header Ads

JAMHURI YAOMBA WAKILI MAGAFU AONYWE

Na Happiness Katabazi

UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya wizi sh bilioni 1.8 fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu ya Tanzania, umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, itoe onyo kali kwa wakili wa wa utetezi, Majura Magafu, kwa sababu amekuwa akitumia mbinu za makusudi kuchelewesha kesi.


Kesi hiyo inamkabili Mweka Hazina wa CCM Mkoa wa Kigoma, Rajabu Maranda na Farijara Hussein ambao wanatetewa na Magafu.

Ombi hili lilitolewa jana na Wakili Kiongozi wa Serikali, Stanslaus Boniface, aliyekuwa akisaidiwa na Wakili Mwandamizi Fredrick Manyanda na Kimaro mbele ya jopo la Mahakimu Wakazi linaloongozwa na Saul Kinemela, Focus Bampikya na Elvin Mugeta ambapo aliiambia mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja jana kwa shahidi wa tatu wa utetezi kutoa ushahidi.

Wakili Kiongozi Stanslaus aliambia mahakama wao wako tayari kuendelea na kesi hiyo lakini cha kushangaza wakili Magafu na shahidi huyo juzi na jana hawakutokea mahakamani na wala hajawasilisha taarifa zozote.

“Waheshimiwa mahakimu, Magafu ni ofisa mahakama wa siku nyingi taratibu zote za kutoa udhuru anazijua lakini ameshindwa kufanya hivyo badala yake wateja wake(washtakiwa)kizimbani wanakuja kueleza mahakama kuwa eti walimtafuta wakili wao huyo na wakamkuta katika hospitali ya Amana akisubiri tiba lakini chakushangaza huyo wakili wao ameshindwa kuleta vyeti mahakamani kuonyesha anaumwa:

“Sisi tunasema hii ni mbinu mpya inayotumiwa na wakili huyo kuchelewesha kesi za EPA zisimalizike haraka na kwa wakati kwani hapo awali waliwasilisha nia ya kukatia rufaa Mahakama Kuu uamuzi wa mahakama hii uliowaona washtakiwa hao wanakesi ya kujibu,na wakati wakiwasilisha nia hiyo ya kukata rufaa wakili Magafu alikuwa anafahamu fika sheria inakata uamuzi huo kukatiwa rufaa, na kesi hii ilisimama kwa miezi kadhaa bila kuendelea na baadaye akaamua kuondoa nia hiyo….sisi upande wa Jamhuri tunaomba mahakama hii itoe onyo kali kwa upande wa utetezi kwani sisitunaamini wanatumia mbinu hizo kwaajili ya kuchelewesha kesi hii isimalizike kwa wakati ….sisi tumeishachoka na hizi kesi tunataka zimalizike haraka.

Kiongozi wa jopo Hakimu Mkazi Kinemela alikiri kesi hiyo kuwa ni ya muda mrefu na kuahidi kuyafikisha kwenye uongozi wa mahakama ili yapatiwe ufumbuzi na kuiahirisha kesi hadi Julai 26-31 itakapoendelea kusikilizwa.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Juni 26 mwaka 2010

2 comments:

Anonymous said...

Unԁеniably consider that that you sаid.
Yоur favourite justіficаtion appeareԁ to be at the web the simpleѕt
thіng to take note оf. I sаy to you, I dеfіnitеly get annoyed whilе othеr
folks thinκ about worries that they јust don't recognize about. You managed to hit the nail upon the highest and defined out the entire thing without having side effect , folks could take a signal. Will probably be back to get more. Thanks

Also visit my site personal loans

Anonymous said...

Attractiѵe component to content. I just stumbled
upon yοur site and in аcсeѕѕion capital to ѕаy
thаt I get іn fact lοvеd aссount youг blog
рoѕtѕ. Any way Ӏ will be subsсribing on your fееԁs and еven Ι fulfillment уou
get аdmission to persistentlу faѕt.

Lоok at mу blοg - unsecured personal loans

Powered by Blogger.