Header Ads

MATATIZO YA UZAZI YAKABILIWE KWA MBINU MPYA

WAPENZI wasomaji wa safu hii leo tena nawakaribisheni kwenye safu hii ili muwezi kushiriki nami katika kujadili, kutafari mada ambazo nimekuwa nikiziibua na kuzijadili kupitia safu hii.

Wiki ,ya pili imepita sasa toka niliandika makala iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho “Malaria inakubalika Tanzania”.Napenda kuwashukuru wote walionipigia simu na kunitumia ujumbe mfupi wa kunipongeza kuhusiana na makala hiyo na pia napenda kumshukuru msomaji mmoja ambaye alijitambulisha yeye ni mpenzi wa makala zangu ila kwa makala hiyo alitoautiana na mimi kwasababu neti zile za Olyset zimewekwa kinga za kutosha na kwamba haziruhusu kupitisha mbu anayeambukiza ugonjwa wa maralia ila zinaruhusu kupitisha mbu ambaye anaambuzika matende.

Nilipingana wazi wazi na msomaji huyo ambaye alijitambulisha yeye ni mtaalamu na mkazi wa Tanga kwa kumweleza wazi mfuko ulioifadhia chandarua hicho cha Olyset, umeandika kwamba chandarua hicho kimewekwa dawa inayozuia mbu yoyote asiweze kusogelea kwenye neti hiyo.Hivyo msomaji huyo alivyonieleza hayo nilimtaka arejee mfuko wa kuifadhi chandarua hicho kimeandikwa nini. Na wasomaji wangu hiyo ndiyo demokrasia ya kuruhusu wasomaji kunikosoa kwa hoja na vielelezo na si vinginevyo.Nawashukuru sana .

Lakini leo katika safu hii nitazungumzia mada mpya ambayo kadri siku zinavyozidi kwenda imeanza kuonekana ni tatizo ambalo limeanza kutanuka katika jamii yetu ya Tanzania , hali inayopeleka baadhi ya watu kuanza kuhoji kwamba kupotea kwa uwezo wa jamii kuzaa, ni janga la taifa?



Katika vinjari zake ndani ya Jamii, Fukuto la Jamii , limekumbana na tatizo la kijamii linaloainisha kwamba watu watatu kati ya watu 10 niliozungumza nao wamesema jamii imeanza kupoteza kuzaa.

Hii ina maana kwamba kati ya watu wakiwa wanawake au watu 10 wakiwa wanaume, sita kati ya jumla ya watu 20 hawazai.

Kutozaaa kwa watu hao sita, hakujulikani kumesababishwa na nini.Baadhi yao wamedai kwamba wanapimwa vipimo vya uzazi mahospitalini na wanabainika hawana tatizo lolote linaloweza kuwazuia kupata ujazito na kisha kuzaa watoto.

Kwa kuwa jambo hili lina makandokando yake ni vigumu kwa Fukuto la Jamii kujua kama juhudi zote za kitalaamu zingefanyika wengi kati ya hao sita wangepata watoto.

Lakini idadi ya watu wa tatu kati ya kumi inaashiria asilimia 30 ,kiwango ambacho ni cha juu mno kwa tatizo kama hili. Wataalamu wa afya watanisahihisha nikiwa nimekosea lakini isingetemewa tatizo hili lizidi asilimi 1 hadi 1.5.

Fukuto la Jamii , linaona hili ni eneo linalogusa uhai wa jamii na uendelevu wake hivyo ni eneo nyeti linalostahili kutupiwa macho kitalaamu zaidi.

Itafurahisha tukijua wanajamii bado wanauwezo wa kuzaa bila matatizo pale inapoitajika.Kushindwa kuzaa panapohitajika,ni tatizo na kero, mateso kwa wanandoa na wale waliofikia umri wa kuzaa.

Wengi wanaopatwa na tatizo hili usononeka kimya kimya na ulichukulia kama ni tatizo binafsi , bahati mbaya, kulogwa na mkosi.

Lakini hili ni jambo ambalo jamii kwa pamoja inawajibika kuguswa naloi na kulitafutia ufumbuzi.Ni vyema utafiti ufanywe na wataalamu wa sekta ya afya na tiba kujua ukubwa wa tatizo lenyewe na kujaribu kupata chanzo chake.

Je ni mfumo wa maisha na wanajamii kwa maana ya vyakula, vinjwaji, madawa, uchafuzi wa mazingira, hewa chafu,nk.?

Je ni uwepo wa madini au vichocheo vingine vya kiasili au visivyo vya kiasili ndivyo vinasababisha tatizo hilo au ni ukahaba, utoaji mimba wa kupindukia wa baadhi ya wanawake enzi wakiwa wasichana, ulevi wa pombe, utumiaji wa dawa za kulevya au kutozifuata mila na desturi zilizowekwa na mababu zetu nk?

Haya yote ya yapo ndani ya jamii yetu lakini si vyema wanajamii kuwa wavivu katika kufikiri kuchukua njia ya mkato au kutoa majibu ya mkato kuhusu tatizo hili ambalo hivi sasa tunashuhudia ndoa nyingi zikisambaratika muda mfupi baada ya kufungwa ukiuliza sababu ni mmoja wa wanandoa hao hana uwezo wa kuzaa.Inauzunisha kweli.

Mungu ibariki Tanzania , Mungu ibariki Afrika.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Juni 20 mwaka 2010

No comments:

Powered by Blogger.