KESI YA MTIKILA YAANZA KUUNGURUMA
Na Happiness Katabazi
KAMISHNA Msaidizi wa Polisi(ACP)Valentino Mulongola(49) jana aliambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kuwa Mwenyekiti wa Chama Democraty(DP)Mchungaji Christopher Mtikila ndiye aliyemuita Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kwamba ni gaidi namba moja na mhuni wa kwanza.
ACP-Mulongola ambaye ni shahidi wa kwanza upande wa jamhuri ambaye Afisa wa Upelelezi toka Makao Makuu ya Idara ya Upelelezi ya Jeshi la Polisi, alieleza hayo jana wakati akiongozwa kutoa ushahidi wake na Wakili wa Serikali Ponsian Lukosi na Ester Kyala mbele ya Hakimu Mkazi Jenevitus Dudu, ambapo kesi hiyo ya Jinai Na.768/2007 ilianza kusikilizwa rasmi ambapo pia mahakama hiyo jana ilipata fursa ya kuonyesha mkanda wa video inayoonyesha mshtakiwa akitamka maneno hayo mbele ya waandishi wa habari mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka 2007.
Alidai kuwa Novemba 2 mwaka 2007 alikuwa na cheo cha Mrakibu wa Polisi, na siku hiyo aliweza kukaa meza moja na mshtakiwa na kudai kuwa kabla ya kuanza kumhoji alikuwa amepata taarifa toka kwa wananchi na vyombo vya habari kwamba Mtikila alikuwa amefanya mkutano na waandishi wa habari na katika mkutano huo alitoa matamko ambayo kwa mujibu wa kazi yake ya kuchunguza makosa dhidi ya jamii na uhalifu mwingine, alibaini matamko yale yalikuwa yakikiuka sheria ya makosa ya jinai kwani maneno ya uchochezi dhini ya rais wanchi Kikwete.
“Baada ya kubaini maneno hayo ni ya kichochezi niliwatuma wasaidizi wangu waende katika ofisi za Chennel Ten na ITV wakatafute ile mikanda waliyomrekodi Mtikila pamoja na kuzungumza na wapiga picha waliomrekodi wakati akitoa matamshi hayo na vyombo hivyo vya habari vilitupatia mikanda hiyo…na waliponiletea mkanda nikajiridhisha kwamba matamko yale ya kumuita ‘rais Kikwete ni ni gaidi na yeye Mtikila hawezi kuvumilia kuona nchi inaongozwa na mhuni’.
“Kisha nikawatuma wasaidizi wangu wakamkamate Mtikila nyumbani kwake Ilala na walifanikiwa na wakamleta mbele yangu na nilipomhoji kuhusu tuhuma hizo alikiri kwamba ni kweli ametoa matamko yale na kama unavyojua Mtikila ni mtu wa kutoa ushirikiano alinipa ushirikiano wa kutosha na na nikaanza kumchukua maelezo yake ya onyo kwa kufuata kanuni na sheria na ninaiomba mahakama hii ipokee haya maelezo ya onyo na mkanda wa video kama vielelezo”alidai ACP- Mulongola.
Hata hivyo wakili wa utetezi Mpare Mpoki mara zote mbili alipinga kupokelewa kwa mkanda huo kwasababu hajauona na kielelezo cha pili ambacho nimaelezo ya onyo wakati kinatolewa alipinga kisipokelewe kwasababu hakina saini ya mshtakiwa ila kina saini ya shahidi.
Hata hivyo Hakimu Mkazi Dudu alitupilia mbali mapingamizi ya wakili Mpoki kwa maelezo kuwa hayana msingi na kuamuru shahidi huyo aweke mkanda huo kwenye Televisheni ambayo ilikuwa hapo mahakamani ili mahakama iweze kusikia matamko hayo na wakati mkanda huo ukiendelea kuonyeshwa ulimwonyesha Mtikila akitamka kupinga kuanzishwa kwa mahakama ya Kadhi nchi na kwamba ‘Papa Benedict alitembelewa na gaidi yaani (rais Kikwete) kwasababu nasema mimi rais Kikwete ni gaidi he is terrorist ..ni gaidi anataka kuisilimisha nchi kuwa ya kiislamu , siku zote kiongozi huyo wan chi ahadi zake zinaongozwa na imani ya dini yake “alisema Mtikila.
Shahidi huyo alimaliza kutoa ushahidi wake na Hakimu Mkazi Dudu aliarisha kesi hiyo Juni 14 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kujatwa na kwamba siku hiyo mahakama ndiyo itapanga tarehe nyingine ya kuendelea kusikiliza kesi hiyo.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi 3 mwaka 2010

No comments:
Post a Comment