JELA KWA KUJIFANYA OFISA WA TAKUKURU
Na Happiness Katabazi
MKAZI mmoja wa Dar es Salaam,Hisbert Tijjah jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kujifanya yeye ni mchunguzi toka Ofisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU).
Wakili wa serikali Janeth Ishengoma mbele ya Hakimu Mkazi Stewart Sanga alidai kuwa Agosti 7 mwaka 2006,katika ofisi za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii , kwa njia ya udanganyifu mshtakiwa alijifanya mchunguzi toka TAKUKURU na alijitambulisha kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Brandina Nyoni kuwa anauwezo wa kumsaidia kuzimaliza tuhuma za rushwa zinazomkabili kiongozi huyo huku akijua si kweli.
Hata hivyo mshtakiwa huyo alikana shtaka hilo na wakili Ishengoma aliambia mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Aidha Hakimu Mkazi Sanga alisema ilisema ili mshtakiwa apate dhamana ni lazima awe na mdhamini mmoja wa anayefanyakazi katika ofisi ya serikali ofini nyingine inayotambulika serikalini, asalimishe hati ya kusafiria mahakamani, na mshtakiwa mwenye fedha taslimu sh milioni moja au hati ya mali isiyoamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.
Hata hivyo mshtakiwa huyo alishindwa kutimiza masharti hayo ya dhamana hivyo kumfanya Hakimu Mkazi Sanga aamuru mshtakiwa apelekwe rumande hadi Juni 16 mwaka huu, ambapo siku hiyo upande wa Jamhuri utakuja kumsomea maelezo ya awali.
Chanzo:Gazeti la Tanzania la Jumanne, Juni 8 mwaka 2010

No comments:
Post a Comment