Header Ads

UPELELEZI KESI YA JERRY MURRO WAKAMILIKA-SERIKALI

Na Happiness Katabazi

HATIMAYE UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya kuomba rushwa ya Sh milioni 10 inayomkabili aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1), Jerry Muro na wafanyabiashara wawili uiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kwamba upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.


Mbali na Murro washtakiwa wengine ni Edmund Kapama na Depgratius Mgasa.Murro anatetewa na mawakili wa kujitegemea Richard Rweyongeza na Pascal Kamala ambapo hata hivyo jana mawakili hao hawakutokea mahakamani.

Wakili wa Serikali Matha Misonge mbele ya Hakimu Mkazi Gabrile Mirumbe aliikumbusha mahakama kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya kutajwa na kuongeza kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na wanaiomba mahakama ipange tarehe ya kwaajili ya usikilizwaji wa awali.

Baada ya kusema hayo Hakimu Mirumbe alisema anaairisha kesi hiyo hadi Juni 14 mwaka huu, ambapo siku hiyo upande wa mashtaka utakuja kuwasomea maelezo ya awali washtakiwa.Hata hi

Februlia 5 mwaka huu, washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza na kusomewa mashtaka matatu ya kula njama za kutaka kupokea rushwa kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Michael Karoli Wage.Kati ya mashtaka matatu yaliyofunguliwa dhidi yao, Murro anakabiliwa na mashtaka mawili.

Wakili Kiongozi wa Serikali, Stanslaus Boniface, akisaidiana na Wakili Kiongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ben Lincoln, alidai kuwa katika shtaka la kwanza, watuhumiwa hao wanadaiwa kula njama kwa mujibu wa kifungu cha 32 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.

Inadaiwa kuwa mnamo Januari tano mwaka huu, jijini Dar es Salaam, Murro na wenzake, walikula njama kwa nia ya kutenda kosa linalohusiana na rushwa kinyume cha sheria.

Katika shtaka la pili, inadaiwa kuwa Januari 29 mwaka huu, wakiwa katika Hoteli ya Sea Cliff, washtakiwa waliomba rushwa ya sh milioni 10 toka kwa Wage ili habari zake kuhusu ufisadi, zisitangazwe kwenye kituo cha televisheni cha TBC1.

Aidha, shtaka la tatu ambalo linawahusu Kapama na Mgasa ni la kujipachika wadhifa wa uongo ilidaiwa kuwa Januari 29 mwaka huu, katika Hoteli ya Sea Cliff, jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao wakiwa na lengo la kumlaghai Wage, walijitambulisha kuwa ni waajiliwa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), huku wakijua si kweli.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Juni 1 mwaka 2010

No comments:

Powered by Blogger.