Header Ads

HUKUMU KESI YA MAHALU JULAI 11

Na Happiness Katabazi MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imesema Julai 11 mwaka huu, ndiyo itatoa hukumu ya kesi ya wizi na kuisababishia serikali hasara ya Euro Milioni moja inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na Grace Martin. Hayo yalisemwa jana Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Illivin Mugeta wakati kesi hiyo jana ilipokuja kwaajili ya mahakama kuwapatia mwenendo wa kesi hiyo pande zote mbili katika kesi hiyo ili pande hizo ziende kujiandaa kwaajili ya kuwasilisha maombi ya kuiomba mahakama hiyo kuwaona washtakiwa hao wana hatia au la. Hakimu Mugeta alianza kwa kusema mwenendo wa kesi hiyo upo tayari na kwamba mahakama inawapatia mwenendo huo kwa njia ya Kielektroniki na upande wa Jamhuri uliwakilishwa na wakili wa serikali Vicent Haule na upande wa utetezi uliwasilishwa na wakili wa kujitegemea Mabere Marando na mahakama ikazitaka pande hizo mbili Juni 11 , ziwasilishe majumuisho ya kuwaona washtakiwa hao wanahatia au hawana hatia kwa pamoja kwa njia ya maandishi na kwamba kesi hiyo itakuja kutajwa Juni 14 mwaka huu. Juni 8 mwaka huu, upande wa utetezi ulifunga ushahidi baada ya mshitakiwa wa pili katika kesi hiyo, Grace Martin ambaye alikuwa ni Mkuu wa Fedha na Utawala katika ubalozi hao kumaliza kujitetea na hakimu Mugeta aliairisha kesi hiyo hadi jana ambapo alisema atakuja kuzipatia mwenendo wa kesi hiyo pande zote mbili ahadi ambayo aliitekeleza jana kwa vitendo Mapema mwaka 2007 ilidaiwa na mawakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa walidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka sita, ambayo ni kula njama kutenda kosa la wizi ,kughushi vocha ya malipo ya ununuzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Italia, kughushi mkataba mikataba miwili kwaajili ya kuidanganya serikali,,walitumia risiti ya ununuzi wa jengo hilo ili kuidanganya ili waonyeshe kwa serikali kuwa walimlipa Euro milioni moja muuzaji wa jengo hilo wakati si kweli na kosa la sita ni la kuisababishia serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha za kigeni.Washitakiwa walikanusha mashitaka hayo na wapo nje kwa dhamana. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Mei 17 mwaka 2012.

No comments:

Powered by Blogger.