Header Ads

OMBI LA LULU KUSIKILIZWA MEI 28

Na Happiness Katabazi MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imesema Mei 28 mwaka huu, ndiyo itasikiliza ombi msanii wa Filamu nchini Eizabeth Michael ‘Lulu’anayekabiliwa na kesi ya mauji ya msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba linaloomba mahakama hiyo , iamuru Mahakama ua Hakimu Mkazi Kisutu kulishughulikia ombi la msanii huyo lililokuwa likiomba kesi hiyo isikilizwe katika mahakama ya watoto kwasababu mshtakiwa huyo ana umri wa chini ya miaka 18. Kwa mujibu wa hati ya wito wa kuitwa mahakamani iliyotolewa na mahakama hiyo kwa mawakili wa pande mbili jana, inaonyesha Jaji Dk.Fauz Twaibu ndiyo amepangwa kulisikikiza ombi hilo Na. Na.46/2012 ambalo limewasilisha Mei 15 mwaka huu, mahakamani hapo na wakili kiongozi anayemtetea Lulu, Kenned Fungamtama chini ya hati ya dharula iliyokithiri. Kwa mujibu wa ombi la Lulu,anadai kuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Augustina Mmbando wiki iliyopita alikataa kulitoa uamuzi ombi la mawakili wa Lulu lilokuwa likidai kesi hiyo iamishiwe katika mahakama ya watoto kwasababu mshitakiwa huyo ana umri chini ya miaka 18 na badala yake hakimu huyo akasema mahakama hiyo haina mamlaka ya kutolea uamuzi ombi hilo na kuwashauri mawakili hao kuwasilisha ombi hilo Mahakama Kuu. Kwa mujibu wa hati hiyo ya madai wakili Fungamtama walidai kuwa hakimu Mmbando alijielekeza vibaya kwa kukusema kuwa mahakama ile ilikuwa haina mamlaka ya kusikiliza ombi lao kwahiyo wanaiomba mahakama Kuu imwelekeze hakimu huyo asilikize ombi lao na alitolee maamuzi na kuwa endapo Mahakama Kuu itabaini vinginevyo basi mahakama hiyo ya juu itoe tafsiri ya umri yake kuhusu ombi hilo. Mei 7,2012 mawakili hao waliwasilisha ombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakiiomba mahakama hiyo iamuru kesi ya msanii huyo isikilizwe katika mahakama za watoto wakidai kuwa bado ni mtoto. Mawakili hao walidai mahakamani hapo kuwa msanii huyo ana umri wa miaka 17 na kwamba kwa maana hiyo yeye bado ni mtoto na kesi yake haipaswi kusikilizwa katika mahakama za kawaida kama mtu mzima. Hata hivyo mawakili hao waligonga mwamba baaada ya mahakama hiyo kusema kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kutolea uamuzi ombi hilo na kuwashauri mawakili hao wapeleke ombi hilo katika mahakama kuu kwasababu mahakama ya kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza. Katika uamuzi wake, Mkazi Augustina Mmbando anayesikiliza kesi hiyo alisema kesi hiyo bado iko kwenye upelelezi na kwamba kulingana na jinsi ilivyo isingekuwa busara kuamua hoja yoyote. Hata hivyo upande wa Jamhuri kupitia wakili wa serikali mwandamizi Elizabeth Kaganda ulipinga maombi hayo na kudai kuwa bado wanaendelea na upelelezi wa kesi hiyo na hivyo kuomba wapewe muda zaidi. Wakili Kaganda pia alidai kuwa hata jina linaloonekana katika cheti cha kuzaliwa cha mshtakiwa huyo linasomeka kama Diana Elizabeth wakati mshtakiwa huyo ametajwa mahakamani hapo kama Elizabeth Michael. Akijibu hoja hiyo, wakili Fungamtama alikiri jina hilo kusomeka Diana Elizabeth na kudai kuwa ni jambo la kawaida hasa kwa wakristo kuwa na majina mawili. Mbali na Kibatala na Fungamtama mawakili wengine wa wanaomtetea mshitakiwa huyo ni Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) Joaquine De- Melon a Fulgence Massawe. Kesi ya msingi iliyofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, itatajwa tena Mei 21 mwaka huu.Na Lulu upo rumande kwa kosa la mauji linalomkabili halina dhamana kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Mei 19 mwaka 2012.

No comments:

Powered by Blogger.