Header Ads

UTETEZI KESI YA MAHALU WAFUNGWA

Na Happiness Katabazi MSHTAKIWA wa pili katika kesi ya wizi na kuisababishia serikali hasara ya Euro Milioni Moja, Grace Martin ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imfutie kesi yeye na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu kwa madai kuwa inayowakabili ni kusingiziwa na upande wa Jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi unaonyesha wametenda makosa hayo. Grace ambaye alikuwa ni Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi huo ambaye jana alitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkuu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ilvin Mugeta huku akiongozwa kutoa ushahidi wake na wakili wa kujitegemea Cuthbert Tenga na kisha upande wa utetezi katika kesi hiyo ukaifunga kesi yake rasmi, alidai kuwa kwa mujibu wa hati ya mashtaka, inaonyesha wanakabiliwa na makosa sita ambayo ni kula njama kutenda kosa la wizi, kosa la pili ni la kughushi vocha ya malipo ya ununuzi wa jengo hilo kwa serikali ya Tanzania, waliwasilisha mkataba wa pili kwaajili ya kuidanga serikali,Mahalu alitumia risiti ya manunuzi ya jengo la ubalozi wa Italia kuidanga serikali kuwa alimlipa muuzaji wa jengo hilo ,wizi na kosa la sita ni la kuisababishia serikali hasara. Grace ambaye baada anayomuuliza ambapo alieleza kuwa kuhusu shtaka la pili ambalo Jamhuri inadai Mahalu aligushi vocha alieleza kuwa shtaka hilo ni la uongo kwani shahidi wa tatu wa upande wa Jamhuri ambaye alikuwa ni Financial Attachie wa ubalozi, Stephano Migwano katika ushahidi wake uliorekodiwa na mahakama hii alieleza kuwa ni yeye ndiye aliandaa vocha hiyo na kwamba vocha hiyo haikugushiwa na kwamba ndiyo iliyotumika kumlipa mwenye jengo na siyo kama inavyodaiwa na mawakili wa serikali kuwa iligushiwa. Mshtakiwa huyo alieleza kuwa kuhusu shtaka la nne kuwa Mahalu alitumia risiti ya malipo kuidanganya serikali kuwa zile fedha zilizotumwa na serikali katika ofisi ya ubalozi kuwa alizitumia kumlipa mwenye jengo; alidai kuwa Migwano alipofika mahakamani hapa kutoa ushahidi wake aliitoa risiti hiyo ya malipo kama kielelezo na kilipokelewa kama kielelezo cha nane na akasema kuwa yeye ndiye aliyemlipa muuzaji wa jengo hilo kupitia akaunti mbili tofauti. Ilipofika wakati wa upande wa serikali Lukosi na Haule kumuuliza maswali kwa zaidi ya mara nne mawakili hao walijikuta wakimuuliza maswali Grace ambayo wao walidai maswali yao yanatokana na ushahidi ulitolewa na Grace na nyaraka mbalimbali lakini,mawakili hao walijikuta Grace akiyakana maelezo hayo waliyoyatumia kumuuliza maswali kuwa hakuyasema hali na pia hali hiyo ikamlazimu Hakimu Mugeta naye kuingilia kati na kuanza kurejea kumbukumbu za ushahidi ulitolewa na mshtakiwa huyo ambaye alikuwa ameurekodi. Hata hivyo wakili Lukosi alimhoji Grace akuwa anahusiano gani na ukoo wa Maro ambao anatoka mke wa rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Anna ambapo mshitakiwa alikiri kuwa ukoo wa Maro ni majirani kule kwao Mkoani Kilimanjaro na wanashirikiana katika mambo ya kijamii.Hata hivyo swali hiyo lilimuamsha Marando ambapo alimuuliza Grace kuwa juzi Rais Mkapa alikuja mahakamani kutoa ushahidi wake na kwanini Lukosi hakumhoji Mkapa kuhusu hilo na kuongeza kuwa ni kwanini Grace ana hojiwa maswala ya mke wa mtu kwanini?na kuongeza kuwa mambo ya mke wa mtu aulizwe mumewe lakini tunashangaa upande wa Jamhuri haukumuuliza Rais Mkapa hilo na huyo Anna Mkapa anaingiaje kwenye kesi?Swali ambalo Grace alieleza kuwa anashangazwa kuulizwa swali hilo na kusababisha watu kuangua vicheko mahakamani. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 16 mwaka huu Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Mei 9 mwaka 2012.

No comments:

Powered by Blogger.