Header Ads

MNYIKA AMBWAGA NG'UMBI KORTINI

Na Happiness Katabazi HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imepigilia msumari wa mwisho kwa kusema kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya (Chadema), John Mnyika ndiye mbunge halali wa jimbo hilo na matokeo ya uchaguzi ya jimbo hilo yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi Novemba mwaka 2010,yalikidhi matakwa ya kisheria.
Kesi hiyo ilifufunguliwa aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM), Hawa Ng’umbi aliyekuwa akitetewa na wakili wa kujitegemea Issa Maige dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliyekuwa akitetewa na wakili Kiongozi wa serikali Justus Mulokozi, John Mnyika aliyekuwa akitetewa na Edson Mbogoro na Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo. Kwa mujibu wa hati ya madai ya kesi hiyo ya madai Na. 107/2010, mlalamikaji(Ng’umbi)alikuwa anaomba mahakama hiyo itamke kuwa uchaguzi wa Jimbo la Ubungo ulikuwa ni batiri kwasababu haukuwa huru na haki, taratibu za uchaguzi zilikiukwa kwani kuna baadhi ya fomu hazikujumlisha matokeo, pia Mnyika aliingiza Laptop kwenye chumba cha kuhesabia kura na kwamba alizitumia laptop hizo kujiongezea kula, Mnyika aliingiza watu watano katika chumba cha kujumlishia kura wakati watu hao hawakuwa na kibali cha kuingia ndani ya chumba hicho,pia Mnyika alimtolea maneno ya alimkashifu kwa kumita fisadi kwani alipokuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake(CWT) Kinondoni, aliuza kifisadi nyumba za jumuiya hiyo na kwamba kuna baadhi ya kula zimeongezeka. Hukumu hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa shauku kubwa ndani na nje ya Dar es Salaam na kuudhuliwa na mamia ya wafuasi wa chama cha CCM na Chadema ilisomwa jana na Jaji Upendo Msuya ambaye aliketi katika kiti cha enzi na kuanza kuisoma hukumu hiyo kwa lugha ya Kiingereza. Jaji Msuya alianza kwa kulichambua dai la kwamba mdaiwa wa pili(Mnyika) aliingiza Laptop binafsi katika chumba cha kujumlishia kura ambazo zilimuongezea kura hewa 14,857 ambazo hazikuwa zimehesabiwa, ambapo jaji huyo alisema mlalamikaji katika kesi hiyo alileta jumla ya mashahidi wa tatu lakini mashahidi wote hao walishindwa kuthibitisha dai hilo. Alisema kwa mujibu wa Kanuni za Mahakama kifungu cha 50(1) na kanuni zake kinasema vifaa vyote vya uchaguzi vitakiwa visambazwe na Tume ya Uchaguzi kwa Msimamizi wa uchaguzi ,Kamishna au Mkurugenzi wa Uchaguzi na wao watatoa maelekezo yanatoondana na matumizi na usambazi wa na jinsi ya kuviifadhi vifaa hivyo maalum kwaajili ya uchaguzi. “Hoja katika dai hili ni je Laptop hizo zilitumika kuongezea kura au la..lakini mahakama baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili umeona Ng’umbi ameshindwa kutoa vielezo au kuleta ushahidi wa kuunga mkono dai lake hilo la kwamba kompyuta hizo mali ya Mnyika ambazo kisheria hazikupaswa kutumika kujumlishia kula, zilitumika ndani ya chumba hicho kujumlishia kula na kwa sababu hiyo mahakama hii itapilia mbali dai hilo kwasababu sheria na maamuzi mbalimbali ya mahakama ya Rufaa yanatamka wazi kuwa ni jukumu la mlalamikaji kuthibitisha madai yake”alisema Jaji Msuya. Aliendelea kuchambua hoja ya kura 14,857 kuwa ni hewa, jaji huyo alisema amelazimika kuzifanyia mahesabu idadi za kura walizopata ambapo alisema Mnyika alipata kura 66,742, Ng’umbi 50,554 jumla ya kura hizo ni 117,286 na wagombea wengine 14 toka vyma vingine walipa kura 15,210 kwa hiyo jumla ya kura zote walizopigiwa wagombea wote 16 ilikuwa ni 132,496. “Baada ya kufanya mahesabu ya kura hizo nimebaini ya kuwepo kwa tofauti ya kura 353 kati ya jumla ya kura zilizopigiwa chama cha Chadema na CCM..kwa hiyo tofauti hapa ni asilimi 0.3 ya jumla ya kura halali zilizopigwa ambazo kwa mawazo yangu zinafanya kuwepo kwa dosari za kibinadamu katika kielelezo cha kwanza; “Kuhusu mnadai ya upande wa utetezi ambao walielezea hizo kura 14,857 zinazobishaniwa na mdaiwa zinaweza kuhesabiwa kwa jumla ya wagombea 16 ambao walipata 132,496 ambapo kura halali zilizopigwa ni 117,639 ,kura zilizoaribika ni 2,184 unapata jumla kura 14,857. “Katika akili yangu nimetafakari dai hili ,pia nimezingatia mazingira ya kujumlishia kura yaliyoelezwa na pande zote katika kesi hii,nimezingatia muda wa kazi na kielelezo kilicholetwa na upande wa utetezi nimekubali kielelezo hicho ni sahihi na kwamba dosari hiyo ya kura 14,857 haikuweza kufanywa na laptop hizo na kwamba katika utetezi wake Mnyika hakupinga kuingia na laptop hizo ndani ya chumba alidai aliingia nazo kwaajili ya kuhakiki kura ambazo zilishahesabiwa na maofisa wa NEC ….kwa maelezo hayo hapo juu mahakama hii inasema hata sheria haikatazi wakala wa mgombea kuingia laptop kwenye chumba cha kujumlishia kura na pia Ng’umbi ameshindwa kuleta wataalamu wa kompyuta waje kutoa ushahidi ambao ungeonyesha laptop hizo zilitumika kujumlishia kura na kwa maana hiyo ombi hilo nimelikataa ”alisema Jaji Msuya. Kuhusu dai kuwa Mnyika aliingiza watu zaidi ya nane ambao hawakustahili kuingia kwenye chumba cha kujumlishia kura, jaji huyo alisema Ng’umbi ameshindwa kutoa ushahidi unaonyesha watu hao waliingia kwenye chumba hicho na hata kama waliingia kwenye chumba hicho waliathiri vipi taratibu na kanuni za uchaguzi wa jimbo hilo. Jaji Msuya alisema kuhusu dai kwamba Mnyika alimkashifu Ng’umbi katika mkutano wake wa adhara alioufanya Septemba mwaka 2010 ambayo alidai alimuita ni fisadi kwasababu aliuza nyumba za UWT ,alisema pia mlalamikaji huyo ameshindwa kuthibitisha dai hilo kwani lilijikita katika misingi ya ushahidi wa kusikia ambao hautakiwi mahakamani. “Kwa kuitimisha mahakama hii imetupilia mbali madai yote ya mlalamikaji kwasababu ushahidi alioutoa wakati akijitetea kwenye kesi hii ulikita katika ushahidi wa kusikia ambao mahakama kamwe haiwezi kuupokea ushahidi huo wa kusikia na kwa maana hiyo mahakama hii kwa kauli moja ina mtangaza Mnyika kuwa ndiye mbunge halali wa jimbo la Ubungo na kwamba taratibu zote za uchaguzi zilifuatwa “alimaliza Jaji Msuya na kusababisha kulipuka kwa nderemo na vifijo toka kwa wafuasi wa Chadema. Baada ya kumalizika kusomwa kwa hukumu hiyo, wanachama hao wa Chadema walimbeba juu juu Mnyika na kumtoa nje ya viwanja vya mahakama huku wakionyesha juu alama ya V na wakiimba Chadema,Chadema. Lakini hukumu hiyo ilipokelewa kwa uzuni kwa upande wa wanachama wa CCM, ambao walimsindikiza Ng’umbi mahakamani hapo ambapo walionekana kupooza na wafuasi wa Chadema walipomaliza kuondoka katika viwanja hivyo, ndiyo wafuasi wa CCM huku wakiwa wameongozana na Ng’umbi nao waliondoka katika eneo la viwanja hivyo kimya kimya. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Mei 25 mwaka 2012.

4 comments:

Anonymous said...

Same exact afternoon set up mortgages will be a variety of online payday
loans offered for one few weeks period of time
inside urgent situations. Many people don’t
necessitate a evidence of situations’ unexpected emergency,
neither of them they need surety, credit file neither other stuff.
You might strategy a secondary, certain important expenses and also take care of your business interest obligations – Very same evening installation lending products will allow you to in a circumstances.
At present all of these financial products can be found via the internet.


Check out my page :: pożyczka na dowód

Anonymous said...

Same exact time fitting up financial products will be a
form of pay day loans supplied for any calendar month interval during disaster occasions.
Some people don’t involve all the proof of situations’ critical, neither of the two
needed surety, credit ratings neither other stuff. It's possible you'll package a
holiday, a lot of valuable expenditures or covers your business bills –
Very same evening payments lending products can
assist you in a cases. At this time these funds are offered on the internet.


Look into my web-site pożyczka bez bik

Anonymous said...

Similar working day payment lending products really are a variety
of payday loans provided in a four week period stage
within catastrophe conditions. They will don’t demand the proof of situations’ catastrophe, neither they
might need surety, credit history not other stuff.
You'll system if you want a, a lot of necessary purchase or perhaps include your home business fees – Same exact day time setting up lending options can assist you in a occasions. These days those financial products are available on the net.

My page :: pożyczki pozabankowe

Anonymous said...

Same evening installation financial products are actually a sort of
pay day loans offered for your week length around
emergency situations. These don’t involve any
proof situations’ sudden, niether they might
require surety, credit score not other stuff. You can prepare a vacation, a number of significant expenditures or even insure your home
business purchases – Equal day time installation loans will let you in different
instances. Currently such fiscal loans can be
bought on the web.

my web site; kredyt bez bik

Powered by Blogger.