IDD SIMBA ABURUZWA KORTINI
Na Happiness Katabazi
HATIMAYE sakata la ufisadi katika Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam(UDA), jana lilifikia tamati kwa serikali kumfikisha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo Idd Simba kwa makosa ya kughushi,kujipatia fedha kwa njia ya udangayanyifu na kulisababishia shirika la Usafiri Dar es Salaam(UDA) Ltd shilingi bilioni 2.3.
Mbali na Simba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya UDA ,wengine ni Mkurugenzi Salim Mwaking’inda na Meneja Mkuu wa shirika hilo Victor Milanzi wa shirika hilo ambao wanatetewa na mawakili wa kujitegemea Alex Mgongolwa na Said El Mamry ambapo upande wa Jamhuri unawakilishwa na wakili wa Taasisis ya Kuzia na Kupambana na Rushwa,Ben Lincol.
Mbele ya Hakimu Mfawidhi Ilivin Mugeta ,wakili Lincoln alidai washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa nane.Alidai kosa la kwanza ni la kula njama ambalo linamkabili Simba na Milanzi kuwa kati ya Septemba 2 mwaka 2009 jijini Dar es salaam walikula njama na watu wasiofahamika walitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 29 cha Sheria ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa ya mwaka 2007.
Wakili Lincoln alidai shitaka la pili ni la kughushi kinyume na kifungu cha 333,335(a ) na 337 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 kuwa Simba na Milanzi kati ya septemba 2 mwaka 2009 kwa nia ya kudanganya walighushi barua ya tarehe hiyo kwa nia ya kuonyesha akaunti zote za UDA ni overdraft facilitiest, maelezo ambao sikweli.
Shitaka la tatu ni la kuamisha fedha kinyume na kifungu cha 29 cha Sheria ya kupambana na Rushwa, kwamba Simba na Milanzi kwa tarehe hiyo Simba akiwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Milanzi akiwa Meneja Mkuu wa UDA,kwa pamoja walishirikiana kuamisha fedha kwa faida yao binafsi sh 320,000,000,ikiwa ni malipo ya awali na ni sehemu ya ya malipo ya hisa za UDA ambazo walizipokea wao binafsi kupitia nyadhifa zao .
Alidai shitaka la nne ni la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kinyume na kifungu cha 302 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, ambali linamkabii Simba na Milanzi kwamba kati ya Septemba 3 mwaka 2009 na Machi 31 mwaka 2010 kwa nia ya kudanya walijipatia shilini 320,000,000 toka kwa Robert Simon Kisena wakionyesha kuwa fedha hizo pia ni malipo ya awali na sehemu ya malipo ya hisa za UDA.
Lincoln alidai kuwa shitaka la tano ambalo linamkabili Simba na Milanzi ni la kuisababishia UDA hasara kwamba kati ya Septemba 3 mwaka 2009 na machi 31 mwaka 2010 kwa nia mbaya waliajiamishia kiasi hicho cha fedha kwaajili ya matumizi yao binafsi ,wakati fedha hizo zilipaswa kuwa ni malipo ya awali ununuaji wa hisa za UDA,kitendo ambacho kilichosababisha shirika hilo lipate hasara ya 320,000,000.
Aidha alidai shitaka la sita ambalo linawakabili washitakiwa wote watatu ambalo ni la matumuzi mabaya ya madaraka kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa, kuwa septemba 2009 na Februali 2011,washitakiwa hao wakati waitekeleza majukumu yao ya kiutendaji ndani ya shirika hilo ,kwa makusudi walitumia madaraka yao vibaya kwa kuruhusu hisa za UDA 7,880,330,kwa kampuni inayomilikiwa kwa pamoja na Central gorvement na dar es salaam city council kwa makubaliano ya shilingi 1,142,643,935 bila kutangaza tenda ifanyike ,kitendo ambacho ni kinyume na sheria.
Alidai shitaka la saba ni matumizi mabaya ya madaraka ambalo linawakabili washitakiwa wote kwamba walitenda kosa hilo kwa makusudi kwa kuruhusu hisa hizo za UDA kwa kampuni inamilikiwa kwa pamoja Central govemet anda dar es salaam city council kwa Simon group Ltd bila kushirikisha central govement na dar es salaam city Council kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 74 cha sheria ya makampuni.
Shitaka la nane ni la kuisababishia hasara UDA kwa walizembea wakati wakitekeleza majukumu yao kwa kuuza kwa Simon group Ltd hisa 7,880,303 za UDA kwa shilingi 1,142,643,935 bila kuitisha vikao vya tenda ,kitendo kilichosababisha UDA ipate hasara ya shilingi 2,378,858,878.80.
Hata hivyo washitakiwa wote walikana mashitaka yote na hakimu Mugeta alisema ili wapate dhamana ni lazima wawe na wadhamini wawili watakao saini bondi ya shilingi milioni tano kila mmoja, na barua zitakazotambulika.Hivyo washitakiwa wote waitimiza masharti ya dhamana na Idd Simba alitoa hati ya mali ilisiyoamishika yenye thamani ya shilingi bilioni nane ambayo ndiyo ilitumika kuwadhamini washitakiwa wenzake.Kesi hiyo imeairishwa hadi Juni 28 mwaka huu, kwaajili ya kutajwa.
Itakumbukwa kuwa Simba alishawahi kuwa Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi (CCM),Mwenyekiti wa wazee wa Mkoa wa dare s Salaam, aliwahi kuwa mgombea urais mwaka 2005 na alijiudhuru nafasi ya uwadhiri wa Viwanda na Biashara kwa kashfa ya sukari.
Kwa upande wake Mwaking’inda aliwahi kuwa katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa dare Salaam, Diwani wa kata ya Sinza kwa muda mrefu.
CHANZO:GAZETI LA TANZANIA DAIMA LA JUMATANO,MEI 30 MWAKA 2012
No comments:
Post a Comment