Header Ads

HUKUMU YA MARANDA NI LEO

Na Happiness Katabazi MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, leo inatarajiwa kutoa hukumu katika kesi ya wizi wa shilingi 2.2 katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), inayomkabili Kada wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Rajabu Maranda na mpwa wake Farijala Hussein. Hukumu hiyo ambayo inatarajiwa kusomwa na Jopo la Mahakimu wakazi linaoongozwa na Jaji Fatma Masengi, Catherine Revocate na Kayoza inakuja baada ya Aprili mwaka huu washtakiwa hao wanaotetewa na wakili wa kujitegemea Majura Magafu wakati upande wa Jamhuri unawakilishwa na mawakili wa serikali Timon Vitalis na Arafa Msafiri kumaliza kujitetea jopo hilo kuipanga tarehe ya leo kuwa ndiyo watatoa hukumu ya kesi hiyo. Endapo hukumu hiyo itatolewa leo na mahakama hiyo, itakuwa ni hukumu ya pili katika ya jumla ya kesi 11 za EPA zilizofunguliwa mahakamani hapo kwa mpigo kuanzia Novemba 2008 na Mkurugenzi wa Mashitaa (DPP), Dk.Eliezer Feleshi kwa washtakiwa tofauti.Maranda na Farijala walifunguliwa jumla ya kesi tano tofauti. Hukumu ya kwanza ilitolewa Mei 23 mwaka jana, ambapo jopo la mahakimu wakazi lilokuwa likiongozwa na Focus Bambikya, Saul Kinemela na Ilvin Mugeta walimuhukumu Maranda na Farijala kwenda jela miaka mitano kwa makosa ya kujipatia ingizo la shilingi bilioni 1.8 toka Benki Kuu, na hadi sasa washtakiwa hao wanaishi katika gereza la Ukonga. Ikiwa leo hukumu hiyo itatolewa katika kesi hiyo ya pili dhidi ya washtakiwa hao, washtakiwa hao watabakiwa wakikabiliwa na kesi tatu ambazo zimefikia hatua ya kuendelea kusikilizwa. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Mei 17 mwaka 2012.

No comments:

Powered by Blogger.