MAMIA YAMZIKA WAKILI STANSLAUS BONIFACE
Na Happiness Katabazi
MKURUGENZI wa Mashitaka nchini,Dk.Eliezer Feleshi amemwelezea aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa mashitaka marehemu Stanslaus Boniface(44) ,kuwa alikuwa ni mtumishi aliyejituma ,mwadilifu na aliyekuwa na ushirikiano na watumishi wa kada zote bila kujali umri wala cheo chake.
Dk.Feleshi aliyasema hayo jana katika ibada ya kuuga mwili wa marehemu Boniface iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na kuudhuliwa mamia ya watu wakiwemo wanataaluma ya sheria wakiwemo majaji, mawakili,mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema na wengine wote ambao muda mwingi waombolezaji hao walijikutaja wakishindwa kujizuia na kuanza kuangua vilio.
Katika hotuba yake hiyo Dk.Feleshi alisema katika utumishi wake Boniface alikuwa ni mwalimu kwa watu wa kada ya Sheria hasa Waendesha mashitaka kutokana na ueledi mkubwa aliokuwa nao katika fani ya sheria. Na kwamba wanachoweza kufanya ni kuheshimu tukio hilo la jana na kumwombea marehemu apate pumziko la amani.
“Boniface alipenda sana kazi ya Uwakili wa Serikali na hasa kuendesha mashtaka.Alikuwa tayari kuendesha kesi yoyote bila woga.Alikuwa msaada kwa mahakama katika kufikia maamuzi ya haki.Hii inadhiirika kwa kusoma hukumu na maamuzi ya mahakama ya mashauri ambayo aliiwakilisha serikali.
“Mfano mzuri ni hukumu ya Mahakama ya Rufaa Na. 250/2006 katika kesi ya Silivester Hillu Dawi na wenzake dhidi ya Mkurugenzi wa Mashitaka ambapo jaji Rutakangwa alimwelezea Boniface aliyekuwa akiiwakilishia serikali katika shauri hilo kuwa ni mkweli na mpenda haki”alisema Dk.Feleshi.
Alisema katika kesi hiyo Jaji Rutakangwa aliweka kanuni ya washitakiwa wanaokabiliwa na shitaka kuchangia nusu ya thamani ya mali inayohusika shtaka husika ili kupata dhamana badala ya kila mshitakiwa kutoa nusu ya thamani hiyo.
Aidha Dk.Feleshi ambaye wakati akisoma hotuba hiyo huku akionekana kulengwa na machozi, aliitaja kesi nyingine ni ya Mwenyekiti wa Timu ya Simba, Ismail Aden Rage dhi dio ya Jamhuri (rufaa na. 286/2005, ambapo jaji Mroso alieleza wazi kuwa Jamhuri iliyokuwa ikiwakilishwa na Boniface,ilikuwa imewakilishwa na mtu mwenye uwezo na msaada pale alipotamka.
“Kwa kusoma hukumu za mahakama,kila mmoja wetu ataafiki ataona uwezo wa Boniface.Pamoja na na kazi ya kuiwakiloisha serikali mahakamani ,Boniface alipenda kuwafundisha mawakili wenzake.hakuchoka kufanya kazi hiyo.alikuwa tayari kumsikiliza na kumwelekeza kila aliyemwomba ushauri wake.Leo ndugu yetu na mpendwa wetu amemamaliza safari hapa duniani.Tunamshukuru mungu aliyempa uwezo wa kufanya aliyofanya wakati wa uhai wake.
Boniface alifariki mei 27 mwaka huu, katika hospital ya regency. Na amezikwa jana katika makaburi ya Kinondoni na mamia ya watu walioongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Werema.
Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake liimidiwe.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Mei 30 mwaka 2012
No comments:
Post a Comment