MAHAKAMA YA KISUTU YAKAGUA KANISA LA KKKT MBAGALA LILOALIBIWA NA BAADHI YA WAISLAMU
Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, jana ilitembelea Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Jimbo la Kusini Usharika wa Mbagala ambalo washtakiwa 10 ambao ni waumini wa dini ya Kiislamu wanatuhumiwa kulifanyia uharibifu huo ambapo lililikagua kanisa hilo na ikatoa amri ya kuliruhusu kanisa lianze kufanya ukarabati wake .
Hakimu
Mkazi Waliarwande Lema ambaye anaisikiliza kesi hiyo ya unyanganyi wa
kutumia silaha ndiye aliyeongoza msafara wa washtakiwa 10, maofisa wa
Jeshi la Magereza , Polisi na wanahabari kutembelea eneo hilo ambapo
msafara ulianzia mahakama ya Kisutu kwenda katika eneo la kanisa hilo na
kujionea uharibu huo.
Hakimu Lema ambaye alikuwa akipewa maelezo ya uharibifu huo na Mhasibu
wa kanisa hilo, Bernad Maimu na Wakili Mwandamizi wa Serikali Tumaini
Kweka na wakili wa washtakiwa ambapo waliiingia hadi ndani ya kanisa
hilo na kulizunguka kanisa hilo, alisema mahakama imeishaona uharibifu
huo na inatoa amri ya kuutaka uongozi wa kanisa uendelee na ukarabati
wao na akaiarisha kesi hiyo hadi Januari 21 mwaka huu, itakapokuja
kwaaji ya mashahidi wa upande wa jamhuri kuanza kutoa ushahidi wao na
akaamuru washtakiwa hao warejeshwe rumande kwa sababu kosa la
unyang’anyi wa kutumia silaha linalowakabili halina dhamana.
Wakati
Hakimu Lema akikagua kanisa hilo na msafara aliokuwa ameongozana nao
usiopungua watu zaidi ya 40 , baadhi ya wakazi wa eneo la Mbagala Zakhiem Kata ya Chalambe ambapo ndipo lililopo kanisa hilo,walikuwa ni watu wenye utulivu na usalama uliimalishwa na wakazi hao walikaa mbali ya eneo hilo la Kanisa ambapo mahakama jana iliamia hapo.
Awali
jana asubuhi kabla ya mahakama kuamia eneo la tukio, Wakili Kweka
aliileza mahakama kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya upande wa
jamhuri kuwasomea washtakiwa hao ambao ni Hamad Sengondo, Shogo Mussa, Mashaka Iman, Hamza Mohamed, Mikidadi Sadiki, Juma Jumanne, Issa Suleiman, Hamis Masoud Ramadhan Mohamed na Mohamed Yusuf kusomewa maelezo ya awali.
Wakili Kweka akiwasomea maelezo ya awali alieleza kuwa Oktoba 12 mwaka jana, vijana wadogo wenye umri wa chini ya miaka 18 walikuwa wanacheza pamoja na kubadilishana mawazo, mmoja wa vijana hao alikojolea kitabu kitakatifu cha Waumini wa dini ya Kiislamu (Quran).
“Tukio hilo liliripotiwa kwa wakubwa hao na Kituo cha Polisi Mbagala na wakati hatua zaidi zinataka kuchukuliwa ndipo kundi la vijana walijhitokeza na kuafaamia ofisi za taasisi za serikali na nyumba za ibada za dini ya Kikristo”alidai Kweka.
Aidha alidai kuwa washtakiwa hao walikuwa ni miongoni mwa kundi lile lilofanya uharibifu huo katika kanisa hilo la KKKT Mbagala na wakati wakitekeleza uhalifu huo walikuwa
wamebeba silaha ambazo ni nondo na matofali na kuvunja ukuta wa kanisa
hilo na kisha kuvunja milango iliyokuwa imetengenezwa kwa madini ya
Alminiam, meza, mabenchi, viti vya plastiki, madhabahu, mfumo wa umeme, ,sofa seti, , makamati na na grii.
“Na kama hiyo haitoshi walichoma Altale na ofisi ya SACCO ya
kanisa hilo la ofisi ambayo ilikuwa ikitumiwa na mchungaji wa kanisa
hilo, kuvunja kwa mawe maeneo mbalimbali ya kanisa hilo ambayo yalikuwa
yametengenezwa kwa vioo ambapo vitu vyote hivyo vina thamani ya Sh
milioni 500.
“Vile vile washtakiwa hao waliiba Laptop, kinanda cha umeme, spika , saa za ukutani ambapo vitu vyotye hivyo vina thamani ya Sh milioni 20. Na katika kuakikisha watamiza
uhalifu huo walimtishia kwa silaha mlinzi wa kanisa za matofali na
nondo Michael Samwel…..na tukio hilo lililipotiwa polisi na washtakiwa
wote wakakamatwa wakafikishwa mahakamani hapo hadi leo tunawasomea maelezo ya awali”alidai Kweka.
Hata
hivyo washtakiwa hao walikana mashtaka yao na maelezo hayo na kwamba
wao siyo waliotenda makosa hayo ila wanakubali makabila,kazi na majina
yao.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Januari 7 mwaka 2013
No comments:
Post a Comment