MSHTAKIWA-NAJUA SIRI NYINGI ZA MWINYI
Na Happiness
Katabazi
MTUHUMIWA
anayedaiwa kumuibia rais mstaafu All
Hassan Mwinyi sh.milioni 37,440,000 , Abdallah Nassor Mzombe(40) zikiwa ni kodi ya pango katika nyumba
mbili zinazomilikiwa na rais huyo mstaafu, jana ameomba Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imentedee haki kwani hakunda makosa hayo.
Mzombe
aliyatoa maombi hayo jana mbele ya Hakimu mkazi Jenevitus Dudu wakati
alipopanda kizimbani kutoa utetezi wake, alidai kuwa kwanza alikuwa akifanya
shughuli nyingi za wazi na za siri za rais Mwinyi ambazo hata watoto wake wa kuwazaa hawazijui
na kwamba anashangazwa kuona leo hii anashtakiwa kwa makosa ya kumuibia kiasi
hicho cha fedha rais huyo Mstaaafu.
“Mheshimiwa
hakimu mimi sina crown,sina fedha na hao wapangaji waliokuja kutoa ushahidi
kuwa walinipa kodi mimi sikumpelekea Mwinyi ni waongo na sijawahi kugombana nao
isipokuwa mpangaji mmoja tu ambaye tangu mwanzo nilimuona kama nimkorofi…..na
kwakuwa Mwinyi ni kiongozi mkubwa ni wazi mashahidi hao wanaweza wakawa
walishinikizwa kuja kutoa ushahidi wa kuja kunikandamiza mimi kwasababu wakipewa
maelekezo ya kuja kufanya hivyo hawawezi kushindwa epangwa kuja kunikandamiza
ila minasema sina madaraka, fedha na mashahidi ambao nilikuwa nategemea waje
kunitolea ushahidi wananipiga chenga kwasababu wapo karibu sana na mzee
mwinyi….kikubwa hapa naomba mahakama initendee haki ‘alidai Mzombe huku
akiangua kilio.
Mzombe
ambapo wakati akitoa utetezi wake alikuwa akiangua kilio na kulitaja jina la
Mungu wake, alidai kuwa ameanza kufanya kazi za Mwinyi tangu mwaka 1996 na
kwamba Mwinyi amekuwa akimuamini mno na kwamba hakukuwa na mshahara maalumu
aliokuwa akilipwa na Mwinyi kwani Mwinyi alikuwa akimchukulia kama mwanae.
“Mzee Mwinyi
aliniamini sana na hata mambo mengine ambayo amekuwa akituma nifanye siwezi
kuyasema hapa mahakamani kwani hata watoto wake hakuwai kuwashirikisha …mzee
hizo nyumba mbili mnazodai leo eti mimi nimemuibia kiasi hicho cha fedha si
kweli kwani huyu mzee Mwinyi amekuwa akinipa zaidi ya Sh.milioni 300 niende nikamnunulie majumba, mashamba, nikamjengee
majumba naninazipokea mamilioni hayo ya fedha tena bila kuniandikisha sehemu
naenda kulipa kwa wahusika na kisha nanunua majumba na hayo mashamba na
kuandika jina la Mwinyi.
“Hivi wewe
mwendesha mashtaka naomba nikuulize, unaujua husiano wetu na Mwinyi wewe au unaongee?usitake niseme mengi
hapa..hivi unafahamu kuwa Mwinyi nilishakaa na Mwinyi tukajifungia na kuongea
na kukubaliana kwamba ninavyomfanyia shughuli zake hizo kwa uaminifu tena bila
hata watoto wake hawajui kwamba ipo siku ataninunulia nyumba lakini hadi leo
hiyo nyumba hajaninunulia:
“Sasa uenda
kesi hii ndio hayo malipo ya kutaka kuninunulia nyumba ambayo aliyoniadi
akaamua kunizulia janga hili la kesi tena nimekuja kukamatwa siku ya tatu hapa
dar es Salaam,tangu nitoke kijijini Kwetu Songea kumzika mama yangu mzazi na
huyo Mwinyi anamfahamu fika mama yangu’alidai Mzombe huku akiangua kilio.
Kuhusu wizi
wa fedha za kodi nyumba hizo za Mikocheni na Msasani ambazo ni jumla ni Mil.37,
Mzombe alisema kwanza anashangazwa na tuhuma hizo kwani ni rais Mwinyi ndiye
aliyempa hela za kwenda kumnunulia nyumba hizo nay eye mshtakiwa akaenda
akazitafuta akazinunua yeye mshtakiwa kwa jina la Mwinyi na kisha Mwinyi
akajakuzikagua na akampa maelekezo kuwa nyumba hizo ni kwaajili ya kuwapangisha
watu na kwamba akampa maelekezo kuwa ukarabati wa nyumba hizo utafanywa na kodi
za wapangaji wenyewe na kwamba yeye mshtakiwa ndiye atakuwa msimamazi.
Alieleza
kuwa yeye ndiye aliyeenda kuwatafuta madalali na kuwapa kazi ya kutafuta
wapangaji na kwamba nyumba ya mikocheni iilikuwa na wapangaji wa nane na kila
mmpangaji anapotoa kodi ,basi kodi ile anaenda kumuonyesha mzee mwinyi na
mwinyi anampa idhini ya kuendelea na ukarabati katika eneo la mpangaji husika
na kwamba fedha zilizokuwa zikisalia anamrudishia mwinyi na kwamba alikuwa
hawezi kumshinikiza Mwinyi waandikishiane
kwani Mwinyi alikuwa akimchukulia kama mwanae .
Na kwamba
ndiyo maana katika kodi ya nyumba ya Msasani iliyolipwa katika awamu ya tatu
ambacho ilikiwa ni sh.milioni sita ,mwinyi alimpatia ili aweze kuongezea
kununulia gari lake binafsi la kutembelea lakini hata hivyo gari hilo
limegongwa kwa sasa.
“Naomba
mahakama itambue, Mwinyi alikuwa akinichukulia kama mwanae na familia yake
inanifahamu na hata watoto wake wakitaka kununua mashamba walikuwa wananitumia
mimi naenda kuwatafutia mashamba wananipa fedha naenda kuwanunulia naandika
majina yao…ndiyo maana hakuna mahali popote panapoonyesha mwinyi alikuwa
ananilipa mshahara kiasi gani au aliniajiri, Mwinyi alinichukulia kama mtoto
wake licha kuna baadhi ya mambo alikuwa akinishirikisha mimi na watoto
hawajui….nitaendelea kumheshimu ila
sijamuibia na mungu ananiona na kwakuwa mimi sina fedha, sina madaraka
naomba mahakama hii initendee haki na sikusudii kuleta mashahidi kwani
mashahidi niliyokuwa nimepanga kuwaleta wananikwepa kwasababu mashahidi hao
wapo karibu na mzee mwinyi hivyo naomba kufunga ushahidi wangu’alidai Mzombe
huku akiangua kilio.
Baada ya kusema hayo hakimu Dudu alisema
hukumu ya kesi hiyo ataitoa Februlia 12
mwaka huu, na kwamba kesi hiyo itakuja kwaajili ya kutajwa Januari 24 mwaka
huu.
Oktoba 9 mwaka jana, rais All Hassan Mwinyi alifika mbele
ya Hakimu Dudu na kutoa ushahidi wake lakini hata hivyo wanausalama ambao
walikuwa wakimlinda waliwazuia waandishi wa habari kuingia ndani ya chumba cha
mahakama kumuona au kusikiliza ushahidi uliokuwa ukitolewa na Mwinyi lakini
jana waandishi wa habari tuliruhusiwa kuingia kusikiliza kesi hiyo.
Kwa
mujibu wa hati hiyo ya mashitaka ambayo waandishi wa habari za mahakama
walifanikiwa kuipata mahakamani hapo jana ,upande wa Jamhuri unadai Mzombe anadaiwa kufanya makosa hayo kinyume
na kifungu cha 258 na 273 (b) (e) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Sura ya 16
ya mwaka 2002.
Siku
hiyo ya Agosti 21 mwaka huu, ilidaiwa
kuwa kati ya Januari Mosi, mwaka
2011 na Julai 2012 huko Mikocheni , Mzombe akiwa Wakala wa rais huyo
mstaafu, alimwibia Sh 17,640,000 ambazo ni pato la kodi ya nyumba
yake iliyopo eneo la Mikocheni wilaya ya Kinondoni.
Iliendelea
kudai kuwa kiasi hicho cha fedha ambacho Mzombe alimwibia rais Mwinyi kilikuwa
ni kodi ya pango la nyumba namba 481, iliyopo kwenye ploti A ,huko
Mikocheni ya mwaka 2011/2012 na 2012/2013.
Aidha
Mbali anadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, mwaka 2011 na Julai 10, mwaka
huu huko Msasani Village wilaya ya Kinondoni, mshtakiwa huyo
alimwibia tena rais huyo mstaafu Sh 19,800,000 ambayo ilikuwa ni kodi ya
nyumba namba 55 iliyopo kwenye Kitalu C .
Iliongezwa
kudaiwa kuwa kiasi hicho cha fedha kilikuwa ni kodi ya pango la nyumba hiyo la
mwaka 2011/2012 na 2012/2013, hata hivyo mshitakiwa huyo alikana
mashitaka yote na yupo rumande hadi
oktoba 22 mwaka,itakapokuja kuendelea kusikilizwa.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Januari 11 mwaka 2013
ch
No comments:
Post a Comment