Header Ads

POLISI,MAGEREZA WADAI MAKALA YA TANZANIA DAIMA ILIKUWA IKICHOCHEA UASI KATIKA MAJESHI



Na Happiness Katabazi
SHAHIDI wa pili wa upande wa Jamhuri Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, David Hoza katika kesi
ya kuandika na kuchapisha makala ya uchochezi
inayomkabili aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la
Tanzania Daima Absalom Kibanda  ambaye kwa sasa ni Mhariri Mtendaji  wa Kampuni ya New Habari na wenzie wawili,
amedai kuwa makala hiyo ya uchochezi ilisababisha
jeshi la Polisi kufanya mabaraza kwa askari wake ili
kuwaelimisha juu ya kuhepuka uchochezi huo.

Katika kesi hiyo ya msingi, Kibanda anashtakiwa
pamoja na mwandishi Samson Mwigamba na Kaimu
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi
Communication Ltd, Theophil Makunga.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu
Waliarwande Lema, shahidi huyo ambaye ni Mrakibu
Mwandamizi wa Polisi David Hoza, alidai kuwa  jeshi
hilo la Polisi lilizamika kuitisha mabaraza ya kutoa elimu
hili kuwazuia polisi wake kutekeleza ushawishi wa
kichochezi ambao alidai ulitokana na makala hiyo
iliandikwa na Mwigamba na kuchapishwa katika gazeti
la Tanzania Daima toleo la 2553.

Hoza akiendelea kutoa ushahidi wake jana  
alidai kuwa katika toleo hilo lililochapishwa  Novemba 30, 2011
kulichapishwa makala hiyo ambayo yeye aliisoma na
kubahini kuwapo kwa uchochezi hivyo kuandikia
maelezo na kuyapeleka kwa wanaohusika kwaajili ya
kufanyiwa upelelezi zaidi.

Alidai kuwa kabla ya kuanza kwa upelelezi huo,
wakiwa viongozi wa jeshi la polisi, iliwalazimu kuitisha
mabaraza ya kuelimisha polisi, na ilo lilifanyika kwa kila
ofisa wa juu anayewaongoza askari wengine .

 Hoza alitoa maelezo hayo, wakati akijibu swali alilokuwa ameulizwa na wakili wa upande  wa utetezi   Isaya
Matambo, aliyetaka kufahamu iwapo jeshi la polisi
lilichukua hatua gani baada ya kuhisi kuwa makala
hiyo ilikuwa ni ya uchochezi.
Akiendelea kujibu maswali hayo, Hoza alisema kwamba
kwa upande wake baada ya kusoma makala hiyo,
alibahini uchochezi na kwamba mwandishi alikuwa
akiwataka askari kutotii wasitii amri za wakubwa wao ili
kuhasi.
Licha shahidi huyo alikana  kuwa hakuna askari aliyewahi
kuhasi toka makala hiyo , Hoza alidai
kwamba ingeliweza kuwaathiri askari wengine
kwakuwa kilichoandikwa kilikuwa kikiwafanya askari
kuona kwamba wanakandamizwa na kuwa
washirikiane na iliyoitwa nguvu ya umma kupambana.

“Licha  mwandishi
hakuwa askari mwenye uwezo wa kutoa amri na
kufuatwa, lakini maneno yake ndani ya makala hiyo
yalijaa uchochezi dhidi ya majeshi yote ya ulinzi na
usalama.

"Na  kawaida askari polisi ufuata amri ya kisheria
inayotolewa na mkubwa wake, hiyo makala si kwamba
ilitoa amri bali ilitoa uchochezi wa kuwashawishi kwa askari
juu ya kutotii amri za wakubwa wao"alidai Hoza.

Alidai kuwa hata yeye alipoisoma ilimpa ushawishi, na
ndio maana akaona kuwa ingeliwashawishi wengine na
kuamua kuchukulia hatua ya kuandikia maelezo kwa
wakubwa wake ili ifuatiliwe.

Hoza alidai baada ya kuandika maelezo hayo, ulianza  kufanya upelelezi  ambao ulishirikisha maofisa wengine kutoka vikosi vya ulinzi na usalama ambavyo Mwigamba
alivitaja katika makala yake.

Aliongeza kuwa pia walishirikishwa maofisa kutoka
idara ya Habari maelezo, kwaajili ya  utaalamu wa
kuhusiana na masuala ya uandishi wa habari.

Kwa upande wake shahidi wa tatu katika kesi hiyo
ambaye ni Kamishna msahidizi wa jeshi la Magereza
George Mwambashi, akitoa ushahidi wake jana alidai kuwa kwa uchunguzi
aliofanya hakukuwa na askari yoyote wa magereza
aliyehasi kutokana na makala hiyo inayodaiwa kuwa
ya uchochezi.

Akitoa ushahidi huo, Mwambashi alidai  kuwa jeshi
lake pia lilifanya jitihada ya kuelimisha askari wake ili
kuwahepusha na uhasi ambao pengine ungeweza
kutokea kutokana na uchochezi huo.

Hakimu Lema   aliarisha kesi hiyo hadi  hadi Februari 14 mwaka huu,
itakapoendelea kusikilizwa tena mahamani hapo.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Januari 15 mwaka 2013

1 comment:

Anonymous said...

the early years of the 20th century, armoured cars - the military application of civil technology - were a natural way to proceed, and in fact saw action in this form in the early part of World War One. [url=http://www.ukdresshop.co.uk]Formal Dresses uk[/url]
[url=http://www.expeditionparkaca.com]canada goose jackets[/url] The best hairstyles for your hair type and length when you decide to go natural.
Which Non secular louboutin air-con possibilities 2012 may perhaps continue most with the service improvements displayed with the 2011 sort, especially virtually any Hyperfuse better with regards to minimal pounds along with breathability, although virtually any full-length Cushlon midsole along with 360 Possibilities Air-con procedure boost foam along with assure virtually any perhaps vacation. http://www.londongenuinepandora.com I would associate a knife with something that is smooth and sharp, and especially is dangerous. What designs and decorations would you like? You will discover a large selection of colors to pick from too. Overall, all music genres performed well with the Tours and the quality of the bass was rich and smooth.
The more sensible among us will get on with studies, work, love and life in general. [url=http://www.femmescanadagoose.com]Canada Goose Kensington Parka[/url] The duo is combined with a chunni or dupatta.
To view a few of your online Prevata shoe selections, click on the link above.. The leather looks nicer (unless that's an artifact of photoshopping) and the last looks more elegant. Did I say they shouldn get it done? No. [url=http://www.promkleidde.com/]vergünstigte kleider[/url]

Powered by Blogger.