MAHAKAMA YAMFUNDISHA SHERIA MTUHUMIWA WA KUMJERUHI DK.ULIMBOKA
Na Happiness
Katabazi
MAHAKAMA ya
Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemweleza mtuhumiwa anayedaiwa kumteka na
kumjeruhi aliyekuwa Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk.Steven
Ulimboka, Joshua Mulundi kuwa mamlaka
hiyo haina mamlaka ya kuilishinikiza Jeshi la Polisi likamilishe upesi upelelezi wa kesi hiyo na kesi nyingine.
Kauli hiyo
ilitokewa jana na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ilvin Mugeta dakika chache baada ya Mulundi ambaye ni raia
wa Kenya kumuomba Hakimu mkazi anayesikiliza kesi yake Agnes Mchome amruhusu akamuone Mugeta ili amueleze
matatizo yake hayo ambayo awali alishamweleza hakimu Mchome.
Itakumbukwa
kuwa jana kesi ya Mulundi ilikuwa imekuja kwaajili ya kutajwa mbele ya Hakimu
Mchome na wakili Mwandamizi Tumaini Kweka aliambia mahakama kuwa upelelezi wa
kesi hiyo bado haujakamilika na hakimu huyo akaiarisha hadi Januari 23 mwaka
huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa na kuamuru mshtakiwa arudishwe rumande.
Baada ya
Kweka kutoa maelezo hayo mbele ya Hakimu Mchome, ndipo Mulundi aliomba ruhusa
aongee ndipo akaanza kumueleza hakimu huyo kuwa yeye hivi sasa yupo kwenye
mgomo wa kutokula kwasabababu anashindwa kuelelewa ni kwanini upande wa
mashtaka unachelewa kukamilisha upelelezi na kwamba anataka balozi wa Kenya
nchini hapa afike mahakamani.
Hata hivyo
hakimu Mchome alisema ameyasikia madai yake ila kwa mujibu wa sheria mahakama
ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza
kesi yake na kwamba mahakama yenye mamlaka ya kusikiliza kesi yake ni Mahakama
Kuu .
“Kama ni
hivyo basi naomba hakimu Mchome unipe idhini niende kumuona kiongozi
wako(Mugeta)’aliomba Mulundi.
Ombi ambalo
lilikubaliwa na hakimu Mchome ambapo askari magereza walimsindikiza mshtakiwa
huyo hadi ofisini kwa hakimu Mugeta ambapo alifika na kuanza kumueleza madai
hay ohayo hayo aliyiokuwa amemweleza hakimu Mchome na kwamba anaomba Mugeta amuite balozi wa Kenya mahakamani na
awalazimishe upande wa mashtaka umalize upelelezi wao.
Hata hivyo
hakimu Mugeta akimjibu mshtakiwa huyo alisema hivi ; “mahakama haina mamlaka ya
kulishinikiza jeshi la polisi likamilishe upelelezi na kwamba kuna taratibu zinatakiwa zifuatwe
za kumuita balozi wan chi husika kuja mahakamani”alisema hakimu Mugeta na
mshtakiwa huyo akarudishwa rumande.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa,Januari 11 mwaka 2013
No comments:
Post a Comment