SERIKALI YAMUANIKA IDD SIMBA MAHAKAMANI
Na Happiness Katabazi
UPANDE wa Jamhuri katika kughushi,kujipatia fedha kwa njia
ya udanganyifu na kulisababishia Shirika la Usafiri Dar es Salaam(UDA), Mwenyekiti
wa Bodi ya shirika hilo Idd Simba na wenzake umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu Dar es Salaam kuwa Simba alitumia
sehemu ya fedha za mauzo ya hisa zilizouzwa kwa Kampuni ya Simon Group Limitedkununulia gari lake binafsi.
Mbali na Simba washtakiwa
wengine ni Mkurugenzi wa Bodi ambaye aliwai kuwa Diwani wa Sinza na Katibu
Mwenezi wa CCM,Mkoa wa Dar es Salaam, Salim Mwaking’inda na Meneja Mkuu wa
Shirika hilo la Usafiri Victor Milanzi ambao walifikishwa kwa mara ya kwanza
mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo Ilvin Mugeta ,Mei 29
mwaka jana.
Wakili wa serikali Awamu
Mbagwa alianza kwa kuikumbusha mahakama kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya
upande wa jamhuri kuwasomea maelezo ya awali washtakiwa hao ambapo aidai kuwa Agosti 31, 2009,
Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Simon Group Limited, Robert Kisena
aliwasilisha barua yake ya kusudio la kununua hisa 49 za serikali kwa
uongozi wa UDA.
Mbagwa alieleza kuwa Septemba 2 mwaka 2009, mshtakiwa wa tatu(Milanzi) ambaye
alikuwa ni Meneja Mkuu wa UDA alisaini barua ikiielekeza Simon Group,
kuwasilisha malipo ya awali ya Sh milioni 400 kama ishara ya dhamira ya kununua
hisa hizo.
“Pia barua hiyo ya Kisena iliielekeza kampuni ya Simon Group kuweka fedha hizo katika akaunti binafsi namba 0210001002, inayomilikiwa na Simba katika
benki ya Bank M, tawi la Sea View….. na
barua hiyo ilieleza zaidi kuwa malipo
hayo ya awali ya sh.milioni 400 yangejumuishwa katika ununuzi wa hisa hizo .”,
alidai .
Alidai kuwa barua hiyo ilielekeza kuwa fedha hizo ziingizwe
katika akaunti hiyo Simba ambaye ni Mwenyekiti wa Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, kwa maelezo kuwa akaunti za UDA zilikuwa na madeni mengi wakati
mshtakiwa huyo akifahamu maelezo hayo ni ya uongo.
Wakili huyo alieleza kuwa kutokana na maelekezo hayo ya
washtakiwa, Septemba 3, 2009, Kisena kwa niaba ya Simon Group aliingiza Sh
milioni 250 katika akaunti namba
0210001002 iliyoko Benk M, Tawi la Sea View, inayomilikiwa na mshtakiwa wa
kwanza (Idd Simba).
Wakili hiyo alidai kuwa fedha hizo zilihamishwa kutoka katika akaunti namba 2046600338 inayomilikiwa na Robasika Agro
Products iliyoko katika Benki ya NMB, kampuni ambayo Simon Group Limited ni mwanaisa
wake na kwamba baada ya baada ya fedha
hizo kuingizwa katika akaunti hiyo, siku
hiyohiyo mshtakiwa wa kwanza, Simba, alitoa Sh milioni 100 kwa kutumia hundi namba 125293.
Alidai na kwamba siku iliyofuata, Septemba 4, 2009, Simba, alihamisha fedha hizo kutoka katika
akaunti yake namba 0210001002, kiasi kingine cha Sh milioni 100 kwenda katika akaunti namba 0150000381 inayomilikiwa na kampuni ya
Africarriers Ltd, katika Bank M.
“Kiasi hiki kilichohamishiwa kwa Africarriers kilikuwa ni
sehemu ya malipo ya ununuzi wa gari aina ya Toyota Landcruser VX lenye
namba za usajili T 561 BCX, ambalo hivi sasa limesajiliwa kwa jina la mshtakiwa
wa kwanza yaani Simba.”, alisisitiza Wakili Mbagwa.
Alidai kuwa awali kabla ya kuingizwa kabla kwa kiasi cha Sh
cha Sh .milioni 250 , akaunti ya mshtakiwa ilikuwa na kiasi cha Sh 3,329,242.88
tu.
Kwa mujibu wa Wakili Mbagwa, Novemba 26, 2009, Kisena
aliingiza kiasi cha Sh Milioni 30 katika akaunti namba 6033500127 inayomilikiwa na Pride
Tanzania, Makambako, NMB, na baadaye Sh milioni 20 kwa maelekezo ya mshtakiwa wa kwanza.
Aliongeza kuwa kiasi hicho cha fedha baadaye Desemba
4, 2009 na Januari 27, 2010,
zilihamishiwa katika akaunti namba 4081300002, inayomilikiwa na Pride
Tanzania, makao makuu ya NMB, mwisho wake zinakaingizwa katika akaunti binafsi ya mshtakiwa wa kwanza
namba 0210001002 na mchakato huu wote ulifanyika kwa maelekezo ya Idd Simba..
Aliongeza kuwa baadaye Januari 22, 2010, Kisena aliingiza
tena sh.milioni 20 katika akaunti namba
0210001002 ya mshtakiwa wa kwanza na hivyo kufanya jumla ya kiasi cha fedha
zilizoingizwa na Kisena kwa niaba ya kampuni ya Simon Group Limited, katika
akaunti binafsi ya mshtakiwa kama malipo ya utangulizi ya ununuzi wa hisa za
UDA ni Sh milioni 320….na hata hivyo fedha hizi zote hazikufikishwa kwenye akaunti za UDA badala yake ziliishia kutumiwa
vibaya na mshtakiwa wa kwanza na wa tatu Simba na Milanzi.”
Alidai kuwa baada ya hayo yote kuwa yameshafanyika, Januari
28, 2010 katika mkutano wa Bodi ulifanywa na mshtakiwa wa kwanza, Simba na wa
pili, Mwaking’inda, kwa makusudi na wakijua, walipitisha uamuzi wa kuuza hisa
7,880,303 za UDA kwa Simon Group, ambazo hazikutolewa kwa mauzo.
Alidai kuwa uamuzi huo wa Bodi ulofikiwa bila kufuata
utaratibu wa zabuni yenye ushindani.
Wakili Mbagwa alidai kuwa kutokana na uamuzi huo, Februari 11, 2010, mshtakiwa wa kwanza na wa tatu kwa kutumia vibaya nafasi zao, walisaini mkataba wa makubaliano ya mauzo na Simon Group, ya hisa 7,880,303 ambazo hazikuwa katika mchakato wa kuuzwa.
Alidai kuwa hisa hizo ziliuzwa kwa bei ya Sh.1,142,643,935,tu
kwa bei ya Sh145 kwa kila hisa ambayo alidai kuwa ilikuwa ni chini ya bei ya
soko kwa wakati huo ambapo bei ilikuwa Sh 1513 kwa kila hisa na matokeo washtakiwa waliisababishia UDA hasara Sh 8,422,076,940
(Sh8.4 bilioni).”, alisisitiza Wakili Mbagwa.
Mshtakiwa wa kwanza, Simba alikiri kuwa kweli anamiliki
akaunti hizo zilizotajwa katika benki hizo na kwamba Kisena aliingiza katika
akaunti zake jumla ya Sh milioni 320 , kwa nyakati tofauti.
Hata hivyo alikana kutumia sehemu ya fefha hizo kwa ajili ya
kununulia gari na kwamba fedha hizo hazikuwa sehemu ya malipo ya uuzwaji wa
hisa za UDA.
“Si kweli mheshimiwa
hakimu , ni uzushi na uwongo kuwa hizo Sh milioni 320 zilizoingizwa katika akaunti zangu zilikuwa
malipo ya awali au ya aina yoyote ya katika ununuzi wa hisa za UDA.”, alidai
Idd Simba hata hivyo bila kufafanua kuwa zilikuwa ni za nini.
Pia Idd Simba alikiri kuwa kulikuwa na hisa 15 milioni za
UDA na kwamba serikali ilikuwa ikimiliki asimilia 49 ya hisa hizo, lakini akasisitiza
kuwa uuzwaji wa hisa hizo kwa Simon Group ulifuata utaratibu wa kawaida na
kwamba uamuzi wa kuuza hisa hizo
haukutolewa na yeye na washtakiwa wenzake bali ulitolewa na Bodi nzima ya UDA.
Pia Simba akiri taarifa binafsi za utambulisho wake
yakiwemo majina, vyeo na akaunti
mbalimbali anazozimiliki katika benki mbalimbali.
Washtakiwa wenzake pia walikiri maelezo ya utambulisho wao
binafsi kama majina na nafasi zao kama watendaji wa UDA lakini wakakana
mashtaka yanayowakabili.
Hakimu Mugeta aliairisha kesi hiyo hadi Kesi hiyo hadi
Februari 4 na 5, mwaka huu, kesi hiyo itakapoanza rasmi kusikilizwa kwa
mashahidi wa upande wa jamhuri kuanza kutoa ushahidi wao.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa,Januari 4 mwaka 2013
3 comments:
I all the timе emailed this web ѕіte post page to all my аsѕοciates, ѕince if liκe tо read it
аfteгωаrd my friends will tοo.
The Big Bang Theory Season 6 Episode 12 The Egg Salad Equivalency
Also visit my blog :: The Big Bang Theory Season 6 Episode 12 Free Stream
I feel this іѕ amοng the most vital information for
mе. And i'm happy reading your article. But want to observation on some basic issues, The website style is wonderful, the articles is truly nice : D. Good task, cheersElementary Season 1 Episode 11 Dirty Laundry
Take a look at my web blog Elementary Season 1 Episode 11 Free Stream
Hello, yup thiѕ piece οf wгitіng is in fact pleasant and I
hаve leaгned lоt of things from it on the
topic of blogging. thаnks.httρ://upсoming.
уahoo.сom/evеnt/10692582/IL/Chicago/Watch-CSI-Νеw-Yoгk-Ѕeason-9-Episodе-11-onlinе-CοmmаndΡ/Chicago-Theаtre/
Here is my webpage CSI: New York Season 9 Episode 11 Free Stream
Post a Comment